Zanzibar kwa jicho la Mbara

rugumisa

Member
May 29, 2012
38
9
Kwa mtu msomi wa sheria kama mimi ninayejua sheria za kimataifa sitakataa kwamba hili nchi iitwe nchi inabidi vitu vikuu vitatu vifuatavyo viwepo(i) serikali,(ii)jeshi na (iii)kutambulika kimataifa.Mipaka ya nchi sio Muhimu maana Israel ni nchi lakini haina mipaka rasmi.Na Ukubwa sio Muhimu maana vaticani ni nchi na ina hekari mia tisa tu na monaco pia ni nchi.Lakini hoja yangu ni hili huwe nchi inabdi utambuliwe na nchi nyingine kimataifa ndio maana Taiwan sio nchi maana haitambuliwi kimataifa.
Mimi hizi thread za Zanzibar wanaolalamika zinanikera.kwanza mji magharibi(ambao unasifiwa umeendelea kuliko yote) karibia asilimia 88 ni slum yote.Jiulize sehemu fukara kama Pemba itakuwaje?Maeneo yaliyopangika ni Mbweni,Mpendae,kilimani,michenzani na kikwajuni na BUbuu.Juzi nimepita mitaa ya Jang'ombe hapa zanzibar kwa mguu karibu nilie kwa jinsi watu walivyo mafukara.Yaani nyumba zimebanana sana hata ambulance au gari la kuzima moto haliwezi kupita.nikajiuliza swali moja hivi wizara ya makazi na mipango miji inashindwa kuplan kamji kadogo kama haka hambako hakana watu hata laki sita(maana idadi ya watu inafikia karibia milioni moja)
Watu wa zanzibar badala ya kuongea jinsi ya kujinasua na ufukara wao kila kukicha kwenye vikao vya kahawa ni Muungano tu.Cha kusikitisha zanzibar nzima huwezi kuilingalisha kiukubwa wa eneo na kiuchumi na mkoa mdogo kama kilimanjaro!Mfano kutoka mji mkongwe hadi Nungwi ni mwendo wa usiofika masaa mawili,mji mkongwe mpaka Mkimkazi ni kama masaa moja na nusu.kwa kifupi ukichukua gari yako masaa matano unamaliza kutembelea mikoa yote ya unguja Unguja kusini,Unguja kaskazini na mji magharibi.
Na mapato ya ndani ni kidogo ichi kisiwa ni mdogo sana kwamfano misharaha ya wafanyakazi wa serikali ya mapinduzi serikalini ni laki moja.Na unakuta mtu pamoja na mshahara mdogo anaoa wake watatu!wafanyakazi wanaofanya serikali ya Muungano ndio wanapata mishahara mikubwa.
Na ni sehemu ambayo watu hawashughuliki na kilimo wala ufugaji.Kila kitu wanaagiza bara na nchi za pakistani na uarabuni.lakini kila siku wanalilia kama wana mafuta.
Kama mtu anabisha hoja yangu haje kunipinga maana ninaishi Zanzibar na ninaona ufukara mkubwa uliopo kwenye huu mji.
 
Kama utafanya utafiti hasa kwa Zanzibar na tanganyika basi utakuta wazanzibari wanaishi maisha bora kuliko Tanganyika.

Zunguka zanzibar nzima huwezi kukuta vibanda vya nyasi vinaishi watu, zanzibar hivyo hufugia mbuzi tu. sisemi wanauwezo lakini afadhali kuliko Tanganyika kwa ujumla wake.

Umetueleza viwango vya mishahara lakini hukutuambia hata bei ya vitu hata sukari ambayo inazalishwa bara basi zanzibar ni nafuuu, halkadhalika umeme ni nafuu kuliko bara, c ment pia na vyengine vigi tu.

ukiangalia idadi ya wakaazi wazanzibar na maisha wanayo ishi basi ni zaidi ya mara mbili kwaubora kulinganisha na maisha ya watanganyika wengi.
 
Na cha kusikitisha watu wa kawaida elimu ni ndogo sana.Huu mji wa zanzibar maeneo ya mjini kuna nyumba zilizoezekwa na nyasi.Watu badala ya kuongelea jinsi ya kujikwamua na umasikini wao kila mahali wanaongelea tu Muungano?Wao kila kitu wanalaumu Tanganyika.hata leo Muungano ukivunjika watabaki tu kuwa mafukara.Wenzao wakina Bakhresa na zakaria wametajirika kupitia huu muungano
 
Back
Top Bottom