ZAIN vipi tena Usumbufu huu?

GM7

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
492
24
Jamani wanaJF, hasa mnaotumia mtandao huu wa Zain.
Leo kumetokea tena usumbufu ambao siupendi kabisa. Usumbufu uliotokea leo ni wakati kujaza vocha zao kwenye simu utakuta vocha haikubali badala unapata meseji "Nambari ya vocha haipo" wakati iko sahihi kabisa, mara baadaye inakwambia "tatizo halijulikani" Hivi ZAIN kumpa mteja ujumbe kama huo inakuwa na maana gani?

Wakati usumbufu huo ukiendelea upande vocha za kukwangua. kuna ile huduma mbadala ya kuhamisha salio kutoka zain kwenda zain inayojulikana kama Me2u. Na yenyewe ukijaribu kuitumia na yenyewe haikubali.
Kwanini Zain mwafanya hivyo? Kama kuna tatizo la kiufundi ni vema wakatuma ujumbe wenye heshima kwa wateja. Kwa mfano wangetoa ujumbe kama huu "Samani ndugu mteja kuna tatizo la kiufundi jaza vocha yako baada ya muda fulani"
 
Pole sana mi kero yangu kwa zain ni huduma kwa wateja unaweza piga simu iliupate msaada hawapokei..
 
Tena hilo ndio kabisaaaa, ni tatizo la kila siku. We unapata tatizo la kimtandao sasa unapiga namba ya huduma kwa wateja simu hazipokelewi au ikipatikana utakuta maelezo mengi yanayochukua muda mrefu bila mafanikio. Zain eeeeeee hebu muliangalie hili.
 
Imeshakutokea mara ngapi namna hiyo?

Licha ya tatizo hilo, huku kwetu mbagala tangu siku ile ya mabomu, tunaotumia simu za double line, hatuwapati, tumelazimika kubadili line maana inayoshika ni line ya tigo peke yake, labda kwa wale wenye single line.
 
kama huna line ya zain kanunue ujaribu...utapata jibu, unaweza piga simu hata li-saa unajibiwa na computer eti wako busy au baada ya dk 15 inakatika kama wana wateja sana si waajiri wafanya kazi wa kutosha...isingekuwa hiki kimodem cha internet nimekinunua kutoka kwao line yao ningesha tupa ni baki na tiGO maana voda nao mafisadi tu...
 
Back
Top Bottom