DOKEZO Airtel wamebuni wizi mpya wa kuuza vocha ambayo haijaanza kutumika

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

2013

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
11,358
6,059
Huu ni mtindo mpya ambao Airtel wamebuni ili kuwaibia wateja, tumezoea kuibiwa MB's zetu zinapunguzwa kiaina na wakati mwingine unapokea meseji kuwa bando limeisha hata kabla halijaisha au haujalitumia vizuri.

Lakini sasa wamekuja na mbinu nyingine ya kuwaibia wateja kupitia kuwauzia "Tozo" ya vocha ambayo ukishaikwangua na kuiweka unapokea ujumbe kuwa hiyo vocha bado haijaanza kutumika.

Ukiwapigia simu Airtel huduma kwa wateja wanakushauri uirudishe dukani uliponunua, au uende ofisini kwao.

Yaani kama ulikua safarini ukainunua wilaya moja, ulazimike kupanda basi kumrudishia mwenye duka vocha yako uliyokwangua. Bila kujali muda unaopoteza. Au ni wakati gani wa dharura umenunua vocha. Hata kama ni usiku na maduka yalishafungwa. Kitu kinachoongeza mashaka kama utataka kununua nyingine ili uambiwe pia haijaanza kutumika.

Yaani hii dharau badala ya wao kurahisisha huduma kwa mteja wanakutaka uende tena ofisini. Na ukizingatia Airtel hawana ofisi kila kijiji. Yaani ufunge safari na nauli ya 2000 kwenda mjini kubadili vocha ya Tsh. 1000 ambayo ilikataa kuingia kwa madai haijaanza kutumika. Lakini zipo sokoni zinauzwa kama njugu.

Hali inayoleta usumbufu kama kupoteza vocha yenyewe, muda na gharama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom