Kigogo
JF-Expert Member
- Dec 14, 2007
- 20,508
- 6,146
- Thread starter
- #21
Mimi naomba nianze kwa kuwatetea vijana wetu...kushindwa kwao kujibu maswali vizuri mbele ya kadamnasi ya watazamaji wa TV karibia Afrika nzima,hakumaanishi kwamba vijana wale hawana uwezo. Mara nyingine tension ya kuwa quizzed mbele ya TV waweza kuingia kiwewe,na hio sio kwao tu,wapo watu wazoefu waliowahi kujikanyaga kwenye kujibu maswali (mfano Obama wakati wa moja ya debate zake na bibi Clinton wakati wa primaries za US aliwahi kuchemsha). Labda huko nimekwenda mbali,tuangalie humuhumu kwenye jamii forum ni wangapi wanahofu ya kujikanyaga kwa hoja zao kiasi kwamba wanaamua kushiriki katika mijadala kwa kutumia majina ya bandia~mimi nikiwa mmoja wao).
That said nirejee kwenye hoja ya msingi kuhusu kushuka kwa viwango vya elimu. Nakubaliana na wote kwamba ni kweli viwango vyetu vimeshuka na responsibility ya kushuka viwango hivyo ni makundi (3).
1) serikali (kwa kutoweka na kusimamia viwango vya elimu-hali hii imepelekea mashule kutokuwa na waalimu bora; vitabu vya kufundishia; maabara za sayansi na miundombinu inayofaa.
2) Jamii (kwa kushindwa kutoa kipaumbele katika masuala ya elimu. Jamii ingekuwa proactive katika kuchangia elimu, kufanya tathmini ya viwango na kutoa ushauri sahihi na kujitolea kufundisha vijana wetu pale ambapo kuna pengo la waalimu. Jamii ya Kenya, Ghana-ime institutionalize zoezi la kuchangia elimu over and above serikali inavyofanya (harambee), wakati wenzetu wana fundraise kwa ajili ya kupata fees za kusomesha watoto sisi tuna fundraise kugharimia harusi za watoto. Ukiachilia NGO chache kama Haki elimu, wanajamii hatuna utamaduni wa kutoa constructive criticism/ideas juu ya kuboresha elimu na pia kama. Jamii hatujaweza kujitolea kuwasaidia wanafunzi wetu...while tumekazania kuwataka makondakta wawasaidie wanafunzi kusafiri kwenye mabasi,sijawahi kusikia wanachama wa chama cha mainjinia kikijitolea kufundisha hesabu kwa wanafunzi wetu katika kipindi cha likizo, sijaona tukijitolea as community service ku spend 20hours per year kwenda kufundisha shule ya kijijini kwetu au mtaa wetu. Laiti kila msomi Mtanzania angejitolea masaa 20 tu kwa mwaka kuwafundisha vijana wetu...walau tungepiga hatua. Ukiangalia masaa tunayotumia kwenye vikao vya harusi,kitchen party,sherehe zenyewe, misiba, socializing kwenye vilabu kwa wastani kwa mwaka yanazidi masaa ishirini tunayoongelea. Hatuhitaji kusubiria volunteers kutoka Korea na Peace Corps waje, tuanze wenyewe...
Kundi la mwisho ni la wazazi. Hivi kweli mzazi unahitaji serikali ije nyumbani kwako kusimamia homework za watoto wako? Wangapi tuna spend muda nyumbani kukagua maendeleo ya shule ya watoto wetu na kutoa mwongozo? Katika hili twaweza kuwasamehe wale wazazi ambao hawakupata fursa ya kusoma, lakini wapo wasomi wengi tu ambao hawana muda wa kusimamia watoto wao?
Kwa hali hiyo tatizo la viwango vya elimu linatokana na sababu pana zaidi ambazo sote tuna wajibu wa ku play our part.
Kama unadhani wale vijana wa Arusha uwezo wao mdogo, subiria miaka 12 ijayo, mtakapowaona vijana walio product za hizi shule za kata zenye waalimu walioandaliwa kwa mfumo wa fast-tracking...huko kutakuwa worse zaidi.
My worries sio vijana hao kushindwa kushiriki katika competition ya ZAIN, bali nahofia kama watamudu ushindani katika fursa za kazi,pale watakapokuwa wanashindana na wenzao wa Afrika Mashariki
sijakuelwa?yaani wanashindwa kujibu kwa kuwa na tensio wanaonekana kwenye TV??mbona wanaweza kuongea kwa simu?SIJAKUELEWA