Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,988
Zaidi ya Wafanyakazi 400 wanaoshiriki katika ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge Railway – SGR) Awamu ya 2 (Lot 2) kipande cha Morogoro - Makutupora chenye urefu wa Kilometa 422 wameshiriki mgomo kwa kile kinachodaiwa kutoafikiana na uongozi wa Mkandarasi Mkuu Yapi Merkezi kuhusu suala la malipo na muda wa kufanya kazi.
Taarifa kutoka Dodoma zinaeleza kuwa kwa siku kadhaa kumekuwa na mvutano kati ya uongozi wa Yapi na Wafanyakazi hao kuhusu malipo na muda wa kufanya kazi.
Inaelezwa kuwa Mkandarasi alitoa tangazo la kupunguza muda wa kufanya kazi, kutoka saa kumi na kuwa saa nane uamuzi ambao uliendana na kupunguza malipo ya Wafanyakazi hao.
Maamuzi hayo hayakukubaliwa na Wafanyakazi wengi ambao baadhi yao wanataka malipo yarejeshwe kama awali na wengine wanataka walipwe stahiki zao waondoke kazini kwa kuwa pia wanadai hawajaingiziwa malipo yao ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa miezi kadhaa.
Uongozi wa Yapi haujajitokeza kujibu madai hayo ya Wafanyakazi ambao kuanzia asubuhi ya leo Novemba 8, 2023 walifika katika ofisi za Yapi na kutaka kikao.
Pia soma
- (Video) Raia wa Uturuki wanaojenga Reli ya SGR waendeleza mgomo, wakidai mishahara, waomba msaada kwa Rais Samia
- Mkandarasi Yapı Merkezi anayejenga Reli ya SGR atoa ufafanuzi taarifa za kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake raia wa Uturuki