Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Kamanda wa Kikosi cha usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga
Madereva zaidi ya 357,552 wamebadilisha leseni zao za zamani na kupata mpya tangu zoezi hilo lilipoanza Oktoba mwaka 2010.
Akizungumza na NIPASHE ofisini kwake Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Kikosi cha usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga, alisema zoezi hilo linaenda vizuri kwa kuwa waliobadilisha leseni ni nusu ya lengo.
"Hadi sasa madereva wapatao 357,552 wamebadilisha leseni zao na hili zoezi linaenda vizuri tangu lilipoanza oktoba 2010," alisema Mpinga.
Alisema zoezi hilo limeenda vizuri baada ya operesheni waliyoifanya januari mwaka huu kwa madereva wa mabasi yanayobeba abiria wengi wao wameitikia wito na kwenda kusoma ili waweze kupata leseni daraja C.
Alisema kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita kulikuwepo na msongamano katika vituo vya kukatia kwa kuwa mtandao ulikuwa chini ikawalazimu kuagiza wataalamu kutoka Israel kutatua tatizo hilo na kwa sasa zoezi linaendelea kwa kasi.
Mpinga alitoa wito kwa madereva ambao hawajabadilisha leseni zao wafanye haraka kufanya hivyo hasa kwa wale wa daraja C kwa kuwa wasipofanya hivyo watakakosa sifa za udereva kuendesha magari ya abiria.
CHANZO: NIPASHE