Zaidi ya bilioni 200 kutumika kutandaza mkongo wa Taifa wa mawasiliano wenye urefu wa 4244km kwa kutumia miundombinu ya TANESCO

Nchi kukua kwenye soko la Tech itakuwa kazi kubwa sana kulingana na soko lenyewe linahitaji huduma za data ndio Mambo yaende, Kama sisi tu wenye vikampuni uchwara tunalia sijui wanaoendesha TV station Hali zao zikoje🤔🤔🤔🤔
 
Nakuuliza na wewe,umewahi fanya Kazi ofisi yoyote ya serikali?

Kule kuna wife za TTCL zilizounganishwa na hiyo cables, gharama za data ni chini Sana,kasi kubwa kuliko mitandao mingine hii inayotegemea satellite.

Kwa mfano 4G iko expensive kuliko kutumia cables nk.
"Gharama za data ni chini sana" si utueleze kinagaubaga, maana tunatafuta unafuu wa data
 
Anasema "mradi huo utapunguza kwa kiasi kubwa gharama za huduma za maendeleo na kufikisha huduma za internet kwa maeneo mengi Tanzania " huku mnafungia YouTube na twitter sasa internet mnaimairisha kwa matumizi gani ,mna akili za kujifunika shuka na kujamba sijui unamkomoa nani hapo.
Serikali iwaulize Halotel wanapata faida gani na mkonga wao ulioenea nchi nzima kabla ya kutupa hizo billioni 200 chooni.
 
Ninavyofahamu tofauti ya waya na mkongo ipo hivi: waya ni mmoja lakini mkongo ni 'universal', umebeba nyaya(fiber) nyingi ndani yake.
Aiseeee kazi ipo....
Yaani hiyo ndiyo tofauti kati ya 'waya(wire)' na 'mkongo(optical fiber)' ??
 
Wamechelewa sana hawa, Starlink soon watatumwagia kitu kina speed zaidi ya broadband kwa bei karibu na bure, kitu kitakuwa kama kuangalia high definition TV
 
Hili nalisapoti kwa asilimia zote sababu itarahisisha huduma za internet kupatikana kwa uhakika haijarishi bei.
Baadhi ya viongozi wanaonekana kuwa na asilimia kadhaa za muamko kitu ambacho ni kizuri kwa maendeleo ya taifa.
Now nasubiri watoe tamko kuhusu paypal.
 
Huyu waziri anakula shavu mbaya. Kapewa hela za startups anapeleka kwenye miradi ya watu
 
'Miundombinu ya TANESCO', kwamba mkonga utaning'inizwa kwenye nguzo za umeme ama...!?

Ukisikia neno mkongo wa taifa maana yake ni fiber cable network...

Fiber cable ni kama waya lakini wenye kujumuisha nyuzi nyuzi zenye material ya glasi yenye kupitisha taarifa za kimawasiliano kwa mtindo wa miale ya mwanga katika frequency yenye kubeba taarifa za ki intaneti, sauti, video n.k

Ni kama ambavyo unaona umeme katika miundombinu yake unapitishwa kwa waya zile za aluminium, au mawasiliano ya simu za mezani/intaneti yanavyopitishwa kwa nyaya za copper
 
Ndugulile huwa namkubali sana! Kama mambo yataenda smooth kama yanavyoenda basi anaweza kuwa Ajaye 2030! Ni kiongozi pekee aliweza kusimama against na maagizo ya Jiwe, na Jiwe kwa kuliheshimu hilo akamtengenezea wizara mpya akampatia.
 
Ukisikia neno mkongo wa taifa maana yake ni fiber cable network...

Fiber cable ni kama waya lakini wenye kujumuisha nyuzi nyzui zenye material ya glasi yenye kupitisha taarifa za kimawasiliano kwa mtindo wa miale ya mwanga katika frequency yenye kubeba taarifa za ki intaneti, sauti, video n.k
May be yeye anadhani ni mkonga kama wa Tembo
 
Ni hatua nzuri...

Maana FTTH ilipaswa ije mwanzo kabisa lakini ujenzi wetu holela ndio umekwamisha kwa kiasi kikubwa watu kuwa na intaneti za fiber katika majumba yetu...

Katika nchi zilizoendelea wao hulaza hizo cable chini kama yalivyo mabomba ya maji, lakini kwetu ukifanya hivyo maintenance cost huenda ikawa kubwa kwa sababu ya kukatwa katwa kwa cables hizo mara kwa mara kutokana na shughuli zetu na ujenzi nyumba hovyo...
 
Nahitaji kufahamishwa.
Kuna mwaka Kati ya 2006/7 enzi za rais kikwete,ulichimbwa mtaro kandokando ya barabara kuu za nchi yetu, tuliambiwa ni mkongo wa taifa utaenda Kila mkoa na wilaya kwa ajili ya mawasiliano ya intaneti!

Je huu mradi unatofauti gani na ule wa mh kikwete?
Mwisho, tumeshuhudia maendeleo gani kwenye ule mradi wa awali?
 
Back
Top Bottom