BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,413
- 8,199
Abiria zaidi ya 300 wanaosafiri kwa gari moshi (Treni) kupitia reli ya TAZARA kutoka Nchi jirani ya Zambia,na Mikoa ya Songwe na Mbeya kuelekea Mkoa wa Dar es Salaam, wamekwama kwa zaidi ya saa nane katika stesheni ya TAZARA Mkoa wa Mbeya baada ya kichwa cha gari moshi hilo kupata hitilafu na kushindwa kuendelea na safari.
Wakizungumza baadhi ya abiria katika stesheni ya Tazara Mkoani Mbeya wamesema walitakiwa kusafiri siku ya jumamiosi lakini usafiri huo haukufika kutoka Zambia, hivyo ikawalazimu kusubiri kwa siku tatu hadi jana ambapo usafiri huo ulifika majira ya saa nane usiku, ukiwa na hitilafu ya kichwa na kupelekea kuendelea kusubiri kwa masaa nane zaidi ili waendelee na safari.
Allen Masuba ni meneja stesheni ya TAZARA Mkoa wa Mbeya amesema gari moshi hilo limepata shida likiwa nchi jirani ya Zambia hivyo kulazimika kusafiri kwa kuchelewa na kufanyika marekebesho katika karakana kubwa ya TAZARA iliyopo Iyunga Jijini Mbeya, ambapo lilibadirishwa kichwa na kuendelea na safari kuelekea jijini Dar es Salaam.
WASAFI MEDIA