Zaidi ya Abiria 300 wa Treni ya TAZARA kutoka Zambia wakwama Mbeya

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Abiria zaidi ya 300 wanaosafiri kwa gari moshi (Treni) kupitia reli ya TAZARA kutoka Nchi jirani ya Zambia,na Mikoa ya Songwe na Mbeya kuelekea Mkoa wa Dar es Salaam, wamekwama kwa zaidi ya saa nane katika stesheni ya TAZARA Mkoa wa Mbeya baada ya kichwa cha gari moshi hilo kupata hitilafu na kushindwa kuendelea na safari.

Wakizungumza baadhi ya abiria katika stesheni ya Tazara Mkoani Mbeya wamesema walitakiwa kusafiri siku ya jumamiosi lakini usafiri huo haukufika kutoka Zambia, hivyo ikawalazimu kusubiri kwa siku tatu hadi jana ambapo usafiri huo ulifika majira ya saa nane usiku, ukiwa na hitilafu ya kichwa na kupelekea kuendelea kusubiri kwa masaa nane zaidi ili waendelee na safari.

Allen Masuba ni meneja stesheni ya TAZARA Mkoa wa Mbeya amesema gari moshi hilo limepata shida likiwa nchi jirani ya Zambia hivyo kulazimika kusafiri kwa kuchelewa na kufanyika marekebesho katika karakana kubwa ya TAZARA iliyopo Iyunga Jijini Mbeya, ambapo lilibadirishwa kichwa na kuendelea na safari kuelekea jijini Dar es Salaam.

WASAFI MEDIA
 
Tazara ni shirika lililojichokea,linatirisha huruma na serikali zote mbili hazina mpango wa kulifufua.

Ngojera za kulifufua hazijaanza leo.Ukiongea na wastaafu wa Tazara watakuambia jinsi ambavyo wamekula posho na fedha za safari na vikao nyingi ssna za kujadili jinsi ya kulifufua shirika.

Zamani mkitoka zambia,mkifika Mbeya.Lazima kichwa kibadilishwe.Kimoja kinaingia karakana.alafu kingine kinatoka karakana kinawavuta mpaka Dar.Karakana ilikuwa bize, vichwa vilikuwa vingi vinasubiri kazi.Leo ukienda karakana ya Mbeya ineota nyasi.

Vichwa hamna.Ma Engineer wanavuta sigara tu.
Tazarabis a dead man.
 
Safari ya treni ni ya kizushi sana,mwaka 2006 nilitaka kujaribu kusafiri na treni nikiwa Makambako kurudi DSM nikakata tiketi saa 9 alasiri nikaambiwa itapita saa 3 Usiku, duuuh aiseee nikakaa pale holaaa,mpaka asubuhi.......mchana nikaahirisha na kupanda basi,tangu siku hiyo ya kwanza na ikawa ya mwisho na sijawahi kupanda kabisa hapa Bongo
 
Sasa hao ni Tazara tu tena inatokea si mara nyingi, embu njoo Trc uone jinsi Waha wanavyolalishwa porini.. Ubaya Waha ni wavumilivu huwezi sikia kelele nyingi sababu ndo mkombozi wao wakija na kutoka Dar😂..

Ila kiukweli haya mashirika yetu yana management mbovu sana, mfano mzuri tu hapo TRC.. Viongozi wanawaza jinsi gani watajinufaisha wao wala si shirika. Tunasafari ndefu sana hata kwenye iyo Sgr sina uhakika wala matumaini yoyote yale
 
Hivi mtu una hela zako unapanda zako flight shida zote za nini
Treni ni utalii tosha, bahati mbaya haujawahi kuupanda, ndani ya treni unaweza ukatembea, unaweza ukaenda hotelini au ukaenda baa na usiku ukifika unatandika kitanda chako kisha unapiga usingizi na kama uko daraja la kwanza utakula tunda kimasihara, hizo ndizo raha za treni tofauti na kufungiwa ndani ya kopo ambapo ukipanda tu unaishia kukaa kwenye kiti chako.
 
Sasa hao ni Tazara tu tena inatokea si mara nyingi, embu njoo Trc uone jinsi Waha wanavyolalishwa porini.. Ubaya Waha ni wavumilivu huwezi sikia kelele nyingi sababu ndo mkombozi wao wakija na kutoka Dar😂..

Ila kiukweli haya mashirika yetu yana management mbovu sana, mfano mzuri tu hapo TRC.. Viongozi wanawaza jinsi gani watajinufaisha wao wala si shirika. Tunasafari ndefu sana hata kwenye iyo Sgr sina uhakika wala matumaini yoyote yale
Waha ni wavumilivu kweli kweli, wamewahi kusafiri na basi fulani lina kunguni likaharibikia tabora, walilala kwenye basi siku tatu ndiyo wakafaulishiwa basi kwenda dar
 
Treni ni utalii tosha, bahati mbaya haujawahi kuupanda, ndani ya treni unaweza ukatembea, unaweza ukaenda hotelini au ukaenda baa na usiku ukifika unatandika kitanda chako kisha unapiga usingizi na kama uko daraja la kwanza utakula tunda kimasihara, hizo ndizo raha za treni tofauti na kufungiwa ndani ya kopo ambapo ukipanda tu unaishia kukaa kwenye kiti chako.
Treni zipi izo bro? Hizi za bongo ambazo kulazwa porini ni kugusa na hakuna anaejali? Jamaa hawafati ratiba, watu wanajazwa kwenye treni kama mizigo.. hakuna kitu hapo kwenye treni bongo
 
Treni zipi izo bro? Hizi za bongo ambazo kulazwa porini ni kugusa na hakuna anaejali? Jamaa hawafati ratiba, watu wanajazwa kwenye treni kama mizigo.. hakuna kitu hapo kwenye treni bongo
Umezipanda au unazisikia? Daraja la kwanza ni peke yako, daraja la pili ni abiria wanne tu kulingana na vitanda vinne ambavyo mchana ni viti na daraja la tatu ni holela. Dinning Car na baa ni kwa daraja la kwanza na la pili.
 
Sasa ilo daraja la tatu ndio linachukua abiria wengi kwenye train na wanavundikwa haswa.. mimi naongea kwa uzoefu
 
Back
Top Bottom