Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,894
- 155,913
Yondo Kusala Denise (amezaliwa tar. 1 Januari 1958) ambaye anajulikana zaidi kwa jina la kisanii kama Yondo Sister, ni msanii wa Kikongo. Wengi humwita "Malkia wa Soukous", "Tina Turner" wa muziki wa dansi barani Afrika. Yondo Sister amepata kuwa mwimbaji mkuu katika bendi ya Soukous Stars kwa miaka kadhaa kabla ya kwenda kufanyakazi kama msanii wa kujitegemea. Uwezo wake wa kuimba iliibuliwa na Lutu Mabangu wakati huo Yondo akiwa kama mnenguaji wa Tabu Ley katika bendi yake ya Rocherettes. Yondo muziki uko katika damu, mzee wake alikuwa akipiga muziki kwa kujifurahisha tu, humo kukajengeka ujasiri wa kutoogopa hadhira. Na mara kadhaa alishiriki katika dansi, polepole na kuja kuwa mwanamuziki kamili na kutoa albamu ya kwanza mwaka 1991.
Yondo Sister amepata kutoa album 6 kwenye studio za Air B. Mas Production na Melodie, T.J.R. Music na zote zilikuwa moto mkali. Album hizo ni:-
FBI (2001)
Agenda (2002)
Dernière Minute(1995)
Deviation (1994)
Bazo (1991)
Planete (1990)
Yondo Sister bado yuko hai nchini kwao Congo DRC akiendelea na shughuli za muziki.
Mungu amjalie umri mrefu wenye afya njema, furaha, amani ya moyo, ma mafanikio ya kila aina na ya kila rangi.
Mshana Jr , Pascal Mayalla, Elli