Yeyote anayemiliki gari/pikipiki kisheria, kadi iwe na jina lake, vinginevyo nalo ni jipu!

Pelle mza

JF-Expert Member
May 15, 2008
3,050
1,692
Wamiliki wengi wa magari ya binafsi au biashara wanatembelea mikataba ya mauziano bila kwenda TRA na kubadili umiliki ili jina lisomeke kwenye kadi(motorvehicle registration card)ya gari kwamba mmiliki wa sasa ni fulani.

Mfano mzuri ni magari yalioingizwa hapa nchini na walimu kwa njia ya mgongo wa 'exemption' kisha kuyauza, aliyenunua gari la namna hii anaogopa kubadili jina maana atatakiwa na TRA kulipa ushuru wa tangu lilipoingia hapa nchini!

Binafsi niliwahi kununua gari la 'exemption' nilipoenda kukopa benki nikaambiwa badili jina kwanza liwe lako, nilivyoulizia TRA na kupigiwa hesabu nilichanganyikiwa ikabidi niliuze kimya kimya!

Lakini vilevile kuna magari mengi ya kubeba abiria aina ya 'Hiace' yamenunuliwa na yanamilikiwa na maaskari, kwenye kadi ya gari/pikipiki ni jina la mtu mwingine iki ni kichaka. Wenye daladala wengi wanostahili kulipa kodi wanasumbuliwa na askari wa usalama barabarani ila ya wenzao yanapeta ili hali hayana hata insurance au motor vehicle road licence, hili nalo ni jipu!

Mara nyingi ajali zinapotokea, waanga wanakosa mmiliki wa kumshitaki mahakamani ili walipwe fidia!

WITO: Serikali itunge sheria au kama ipo!, mtu yeyote ukinunua gari mtu, ndani ya mwezi mmoja badili umiliki kwenye kadi ya gari ionekane ni la kwako.

HAPA KODI IMELALA!
 
Sheria iko wazi. Ukanunua gari unatakiwa ubadilishe jina ndani ya miezi mitatu kama sijakosea
 
Kwa hili la kutobadili jina la mmiliki nchi yetu ni tatizo sugu na hata hao TRA na askari wa usalama barabarani (traffic) wenye magari binafsi wengi wao hawabadili jina la mmiliki na huko ndiko kodi kubwa pesa imeshikiliwa, nimuombe waziri mkuu alitolee tamko tunaweza tukafikia makusanyo ya trillioni tatu na siyo ubishi nchi hii kuna pesa uwajibikaji unaokosekana
 
Kuna ukweli hapa......japo mnam'beza ila kaongea point.......
Tutaheshimiana tu........pole pole......😜
 
Kwenda kubadilisha umiliki kwa kadi ya pikipiki ni lazima uwepo mmiliki au hata kumuagiza mtu inafaaa??
 
Sheria ipo na ukibainika na hilo kosa unakabiliwa na faini au kifungo kisichopungua miaka miwili
 
Back
Top Bottom