Yerusalemu Iwe makao Makuu wa Palestina - Serikali ya Tanzania

MCHANGO WANGU KWENYE
KIPINDI CHA MALUMBANO
YA HOJA ITV LIVE JANA
ALHAMISI
Awali ya yote niwapeni pole kwa majukumu ya Ijumaa ya leo, kwa shughuli nzito na mapambano ya kila Siku ya kulijenga Taifa letu.

Ndugu zangu,
kwa wale mliofuatilia kipindi cha "Malumbano ya Hoja" kilichokuwa hewani jana alhamisi kuanzia muda wa Saa 3:00 Usiku,
Mimi Francis Boniface, Sister angu Upendo Peneza na Iron lady Nusrat Hanje tulikuwa LIVE ndani ya Studio za ITV na Radio One Stereo kwa ajili ya kuwawakilisha vijana wenzetu katika kipindi kile cha jana kilichokuwa na mada ya
"Nini Mchango wa Vijana katika kukuza Demokrasia Nchini".

Kwa upande wangu,
nilikuwa na hoja tatu za msingi, ambazo kutokana na ufinyu wa muda, sikupata fursa nzuri ya kuzitolea ufafanuzi mzuri na wa kina, kama nilivyokusudia, licha ya kwamba nilizielezea kwa ujumla kiasi chake.
Hoja hizo ni pamoja na,
tatizo la ajira kwa vijana Nchini, Vijana kunyimwa haki ya kuandamana na kunyimwa haki ya kupiga na kupigiwa kura.

TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA

Kwa kipindi cha miaka takribani mitatu mfululizo ya hivi karibuni, vijana wengi hususani ambao ni wanachama, wafuasi na mashabiki wa vyama vya upinzani, wameonekana kuwa mstari wa mbele katika kulipigia kelele tatizo hili sugu la ajira kwa vijana.

Kwa mfano, wakati na baada ya usaili wa ajira za watu 70 kwenye Idara/Kitengo cha Uhamiaji, vijana wameshiriki kikamilifu katika kuhakikisha kwamba, ukweli wa usaili ule unajulikana bayana.
Vijana hawa kwa kupitia Social Medias, walichukua maamuzi ya kuyataja majina yote yaliyohodhiwa kwa misingi ya kiurafiki, kijamaa na kindugu zaidi.

Hatimaye, baada ya uovu
huu kuzagaa kwenye Social Medias, Serikali kupitia uongozi wa Idara husika ya Uhamiaji Nchini,
walikiri wazi kuwepo kwa tatizo hilo la kuwaengua watu waliokuwa na Qualification za kuweza kupewa ajira hizo 70 zilizofanyiwa Interview na watu zaidi ya elfu kumi, na kuwapachika Ndugu, Jamaa na marafiki wa maofisa wa Idara hiyo, ama waliostaafu au waliopo madarakani hivi sasa.

Unawezaje kuwaajiri Watu ambao hawsna Uzoefu au Taaluma ya Uhamiaji, tena katika kitengo nyeti kama hiki cha Uhamiaji, ambacho huwezi kukitenganisha na kile cha Usalama wa Taifa.
Hii ndio inayopelekea, mpaka kushamiri kwa matukio ya
Mauaji, Umwagaji wa Tindikali, Milipuko ya Mabomu kwenye mikusanyiko ya watu, Kung'olewa Kucha na Meno, ili hali Serikali imeshindwa totally kuwabaini wahusika, hatimaye viongozi wanabaki kutoa majibu dhaifu tena ya kejeli kwamba, hao wamejilipua wenyewe n.k.

Hivyo basi, matatizo kama haya, ni miongoni mwa vikwazo wanavyopambana navyo vijana wa Taifa letu katika kuikuza na kuijenga Demokrasia Nchini.

HAKI YAO YA KUANDAMANA

Vijana wa katika makundi mbalimbali, wamekuwa wakinyimwa haki yao ya msingi iliyopo Kikatiba na Kisheria kwamba kuandamana ni haki ya Raia wa Taifa letu, katika kudai haki zake za msingi, pale inaposhindikana kuzipata haki hizo kama anavyostahili.

Mfano vijana wengi
(Wanafunzi) wa Shule za Sekondari, Elimu ya Juu (Vyuo Vikuu) na Vyuo vya kawaida, wameendelea kuwa na wakati mgumu wa kupambana na watawala hususani pale inapofikia suala la malipo yao ya kujikimu kimaisha (Boom) wanakuwa huko Vyuoni hasa nyakati za masomo.

Wanapoomba kibali cha kufanya maandano ili kuufikisha ujumbe wao kwa walengwa, Jeshi la Polisi hao hao wanaotoa vibali vya maandamano, wanaanza kuwapiga kwa mabomu ya maji, pengine hata risasi na mabomu ya moto.

HAKI YA VIJANA KUPIGA NA
KUPIGIWA KURA

Hapa sasa ndipo kuna
tatizo sugu, tunalohitaji kulishughulikia mapema na haraka iwezekanavyo ili Vijana wenzetu, hususani wale waliopo mashuleni na vyuoni, waweze kushiriki kikamilifu katika kuijenga na kuikuza Demokrasia Nchini kwetu katika Siku za usoni.

Nasema hivyo kwa Sababu gani,
Serikali hii kiziwi ya CCM, kutokana na kuitumia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama chaka lao la kuficha maovu na kung'ang'ania madaraka.
Licha ya kwamba, Katiba inatoa fursa kwa kila Raia kuwa na Haki ya Kupiga na Kupigiwa Kura, isipokuwa kwa wenzetu wa Vyuoni hili ni tatizo linalohitaji tiba mbadala.

Pale ITV na Radio One jana,
niliyaweka wazi haya, kwa sababu tayari nimekuwa miongoni mwa wahanga wa tatizo la kunyimwa haki ya kupiga kura nyakati za chaguzi Kitaifa kwa muda mrefu sasa, kutokana na kigezo cha kanuni na Sheria mbovu za uchaguzi zenye maslahi kwa watawala pekee.

Unapofika wakati wa uchaguzi,
wao watawala, jukumu lao kubwa, kwanza ni kutafuta mbinu ya kuwadhibiti wanafunzi wa vyuoni ili wasipate fursa ya kupiga kura.

Jambo kubwa au mbinu wanayoitumia ni kupima upepo wa wanafunzi hawa kwanza, ikibainika kwamba hawaungwi mkono vyuoni kutokana na madudu ya wazi kama haya ya kuyakataa hadharani maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Rasmu ya Tume ya Jaji Waryoba, Wizi wa billioni 200 za wanyonge unaowahusu vigogo wa Serikali hii ya Chama legelege cha CCM, wanaanza kutengeneza zengwe la kuwadhibiti ipasavyo.

Wanachukua maamuzi ya
kufunga Shule au Vyuo haraka sana na kuwafukuza wanafunzi kutoka mashuleni au vyuoni na kuwaamuru kurudi makwao kwa kisingizio cha kutokuwepo kwa vipindi vya masomo, ili wakose fursa ya kupiga kura, hapo ni endapo walijiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura wakiwa mashuleni na vyuoni.

Kama kipindi cha uandikishaji wa wapigakura wanafunzi hawa walikuwa likizo majumbani kwao, basi mbinu inayotumiwa hapa, ni kuhakikisha kwamba, Siku au Tarehe husika ya kupigakura, iwakute Shuleni au Chuoni, ili wabanwe na ile kanuni mbovu inayotamka kwamba, kila mtu atapiga kura katika kituo alichojiandikishia awali.

Ndugu zangu,
hayo pamoja na mengi zaidi ni miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo vijana wenzetu, katika zoezi zima la ushiriki wao katika kuikuza na kuijenga Demokrasia ndani ya Taifa letu.

Na;
Francis Boniface Marwa,
Mgombea
Uratibu wa Hamasa
BAVICHA Taifa
0785881009/0767881009.
05/09/2014.
*****************

Ahsanteni sana!!!
 
Nitafurahi sana kumsikia membe siku anasikia Israeli nao wakisema wanaitambua Zenj Huru.Wachina ,na israel wna amhusiano makubwa sana na Israel
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom