Yanga vs Toto; Simba vs Majimaji - ni mwisho mtamu!

kichwat

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
1,819
587
Ligi ya Tanzania bara itafikia kilele tarehe 10/04/2011.
Timu zote zinatakiwa kushinda kwa idadi kubwa ya magoli ili kutwaa ubingwa.
Yanga inatakiwa kuifunga Toto, wakati Simba inatakiwa kuifunga Majimaji.

Hivyo tutarajie maajabu siku hiyo. Yanga ikishinda kwa tofauti ya 'x goals', Simba inatakiwa ipige 'x+3' goals

MSIMAMO WA LIGI

Timu /Michezo /Pts /Goal Diff
Yanga 21 46 22
Simba 21 46 20
Azam 21 40 23
Kagera 21 36 5
Mtibwa 21 33 1
JKT Ruvu 21 26 -1
African Lyon 21 25 -9
Toto African 21 21 -7
RuvuShooting 21 20 -7
Polisi Dom 21 20 -10
Majimaji 21 16 -9
Arusha FC 21 12 -28

RATIBA YA MECHI ZA MWISHO (TAREHE 10/04/2011)
Toto v Yanga
Ruvu Shooting v Azam FC
JKT Ruvu v Polisi Dom
Simba SC v Majimaji
Kagera v Arusha FC
Mtibwa Sugar v African Lyon

my take ...usishangae timu kufungwa 8-0 siku hiyo, ndo mwendo!
 
Yanga watoe draw na toto kuinusuru!!!ubingwa mzuri sana ila si kama tawi lako kulizamisha mwaka juzi walipata ubingwa kwa kuifunga toto pia!!
 
Ukiangalia league table uliyoibandika hapa Toto haiwezi kushuka daraja, na majimaji na afc arusha zimekwisha shuka daraja.
So kupanga matokeo ndio mpango mzima
 
Ligi ya Tanzania bara itafikia kilele tarehe 10/04/2011.
Timu zote zinatakiwa kushinda kwa idadi kubwa ya magoli ili kutwa ubingwa.
Yanga inatakiwa kuifunga Toto, wakati Simba inatakiwa kuifunga Majimaji.

Paradox ipo kwa Yanga, kwani Toto (yenye uhusiano wa kimtindo na Yanga) ipo kwenye hatari ya kushuka daraja. Hivyo tutarajie maajabu siku hiyo,

MSIMAMO WA LIGI

Timu /Michezo /Pts /Goal Diff
Yanga 21 46 22
Simba 21 46 20
Azam 21 40 23
Kagera 21 36 5
Mtibwa 21 33 1
JKT Ruvu 21 26 -1
African Lyon 21 25 -9
Toto African 21 21 -7
RuvuShooting 21 20 -7
Polisi Dom 21 20 -10
Majimaji 21 16 -9
Arusha FC 21 12 -28

RATIBA YA MECHI ZA MWISHO (TAREHE 10/04/2011)
Toto v Yanga
Ruvu Shooting v Azam FC
JKT Ruvu v Polisi Dom
Simba SC v Majimaji
Kagera v Arusha FC
Mtibwa Sugar v African Lyon

my take ...usishangae timu kufungwa 8-0 siku hiyo, ndo mwendo!

Mkuu, mwaka huu TFF wanaongeza timu 1 kupanda kwenda ligi kuu. Kwa hiyo zitashuka timu 2 na kupanda timu 3. Zilizoshuka tayari ni Majimaji na AFC. Kwahiyo toto hawezi kushuka daraja.

My take: Ili ubingwa uende Simba ni lazima wajue matokeo ya mechi ya Yanga na Toto. Maadam mechi zote zinachezwa siku moja na muda mmoja kusubili matokeo ya mwenzako hakuna tena. Yanga wameshawahi ifunga Toto hadi goli 6 - 0, na Toto hana cha kupoteza hata wafungwe 10 - 0. Hiyo Simba itamlazimu azidishe magoli ma3 kwenye mechi ambayo Yanga atashinda ili wawe mabingwa. Mfano, Yanga akishinda 7 - 0 Simba inabidi ashinde 10 - 0
 
duh, NOMA! kwa maneno mafupi HAKUNA MPIRA siku hiyo. ni umafia na mizengwe tu!

Yanga wana kazi moja, lakini Simba wana kazi MBILI!
 
Soka letu ni mdebwedo to haliendi mbele wala nini?

natamani siku moja Taifa Stars ingeundwa na wachezaji wasiochezea simba, yanga and azam hasa bila kujumuisha timu zote za Dar, ikanolewa kwa umakini na makocha wa ndani ili tuone matokeo yake. usimba, u-yanga na sasa u-azam, ndiyo kaburi la soka la tz
 
  • Thanks
Reactions: Iza
natamani siku moja Taifa Stars ingeundwa na wachezaji wasiochezea simba, yanga and azam hasa bila kujumuisha timu zote za Dar, ikanolewa kwa umakini na makocha wa ndani ili tuone matokeo yake. usimba, u-yanga na sasa u-azam, ndiyo kaburi la soka la tz
Ahaaa ahaaaa naona AZAM wameongezeka na wao
 
Toto haishuki daraja, tayari timu mbili (AFC Arusha na Majimaji) zilishashuka tangu wiki ileee!
 
...hapo sasa utasikia Yanga kashinda 5-0, ...mara Simba bingwa 9-0!
 
Mkuu hapo umechemsha! Toto hata afungwe 10-0 hana cha kupoteza. Hivyo, Simba wana kazi pevu! Pole yao na hivi Yanga anamalizia na mdogo wake si ndo kwaheri hiyo!!
 
Kombe ni la Yanga haina ubishi maana before the game Yanga tayari ana advantage ya 2 goals so akishinda hata 1-0 Simba has to win at least 3-0 poleni Simba msiokuwa na makucha Kombe laja Jangwani
 
Toto haishuki daraja timu zinazoshuka ni 2,tayari afc na majimaji,toto haina chakupoteza hapo,naona yanga wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa,huo ni mtazamo wangu.
 
Hivi teknolojia hairuhusu hapa kwetu simu zote zikakata mawasiliano kwenye viwanja vyote ili watu wasiwasiliane kupeana taarifa za matokeo? Maana hapa sasa tutegemee mchezo mchafu, Simba akisikia mwenzake anaongoza kwa magoli mawili naye anaongeza mara utasikia Yanga 3-0 na Simba 9-0. Yaani safari hii mchezo huu hautanoga kabisa!!
 
TFF isimwone huruma yeyote kati ya hao wanne
namaanisha yanga/toto simba/majimaji fungia na teremsha daraja mara moja ikibainika wamepanga matoke wasijali ni timu kubwa wala nini. Na uhakika simba watakuwa wakisubiri matokeo ya ccm kirumba ili wafanye wakitakacho ili wakae juu TFF Waige mfano uliochukuliwa na shirikisho la soka la Italia hakuangalia timu kubwa wala ndogo ikazishusha daraja Juventus na Lazio pia kuzipiga faini na kuzipoka point AC Millan na Reggiana, Naamini kwa msimamo ulivyo Simba imekaa vibaya na inauwezekano wa kupanga matokeo ila pia Yanga pia itupiwe jicho la karibu ipewe angalizo la mechi zake na Toto zilikuwa za huko nyuma zina matokeo gani! Pia izingatiwe kuwa Toto na Yanga zina uhusiano wa kindugu kama tawi la Yanga hata siku za nyuma yanga waliwapatia misaada mingi Toto ikiwemo Jezi hivyo najuwa kuwa Simba tawi lao mwanza ni Nyamaume sc. Siku nyingi imetoweka na Yanga tawi lao ni Toto africa Sasa tuangalie kigezo cha mechi za mzunguko wa kwanza, Yanga/Toto Matokeo yalikuwaje? Majimaji/Simba kama Simba walishinda kwa idadi ya magoli zaidi ya mawili ugenini Songea si ajabu hata wakipata zaidi ya magoli matano kwa mtaji wa Majimaji kuwa imeshashuka daraja hawana watakacho kipata hata wakiwagomea Simba kwani kwa vigezo vya heshima utamaduni huo haupo katika soka letu. Pia kuna uwezekano majimaji wasije Dar kumalizia mchezo huo ikiwa hawata ingiza timu Simba watapewa pointi 3 na magoli mawili hivyo hata Yanga wakishinda 1-0 watakuwa mabingwa na haita onekana kama WAMECHAKACHUA matokeo ila wasije kuoneka wameicheza pia mechi hiyo ya mpinzani wake ila Simba kwa upande wao kuicheza mechi ya Mwanza ni ngumu maana Uongozi wote wa klabu ya Toto unajulikana ni wanazi na Wafurukutwa wa Yanga kiasi hata wachezaji Emmanuel swita na Hussein sweid waliwapelekea Toto bure(kwa mkopo) hivyo kwa msaada waliokuwa wakiutoa wana Kishamapanda pia mshikamano waliokuwa wakiwapatia wana Jangwani enzi hizo wakienda mwanza kucheza na Pamba unatoa picha halisi bila hata ya kuchukuwa muda kuumiza Kichwa. Otherwise watumie kigezo cha HEAD 2 HEAD Kumpata Bingwa ikionekana alimfunga mwenzie ktk msimu huu Basi anastahili iwapo uwiano utakuwa sawa Linaweza kuwa jibu gumu kwangu na Kwako pia ila ni Rahisi kupata jibu kutoka kwa aidha (mosha)Davies wa Yanga kajiuzulu ila ina semekana ndie anacheza mechi zote za kwao na za wapinzani wao wajadi au (Kaburu)Geofrey wa Simba anaweza kukupa jibu
 
Mwenye kumbukumbu za mechi za awali Majimaji vs Simba ...iliochezwa Songea
Yanga vs Toto iliochezewa Dar es salaam,
 
Hivi teknolojia hairuhusu hapa kwetu simu zote zikakata mawasiliano kwenye viwanja vyote ili watu wasiwasiliane kupeana taarifa za matokeo? Maana hapa sasa tutegemee mchezo mchafu, Simba akisikia mwenzake anaongoza kwa magoli mawili naye anaongeza mara utasikia Yanga 3-0 na Simba 9-0. Yaani safari hii mchezo huu hautanoga kabisa!!

Kama Vigezo ni mechi za mzunguko wa kwanza ulioyozikutanisha timu hizo unaweza kutoa Angalizo.
Tarehe 07 11 2011
Yanga-2 Toto-0 Uwanja wa uhuru, DSM.
Majimaji-1 Simba-2 Uwanja wa majimaji,Songea RVM.
Hapo Simba wakishinda hata 5-0 Ni sawa kwani kama walishinda ugenini idadi hiyo ya mabao tena kipindi hicho ushindani wa ligi ungali ulikuwa mbichi na majimaji hawakuwa katika nafasi mbaya iweje hiyo keshokutwa wameshakuwa na uhakika mwakani hawapo katika VPL Wasipigwe?. Upande wa Mechi ya Toto Walifungwa 0-2 Ugenini na Marudiano wapo CCM Kirumba, Nyumbani kimtazamo wakifungwa zaidi bao. 0-1 inawezekana ila matokeo halisi washinde wao bao 1-0 hata 2-1 au sare yeyote ile itakuwa fair. Kumbukumbu zangu 1987 timu 8 zilipanga matokeo TFF Wakati huo FAT Waliyafuta matokeo ya mechi zote Nne na hivyo basi Biashara fc ya mwanza ilishushwa Baada ya kubebana na RTC Kigoma Kurugenzi Dodoma wakashushwa baada ya kupanga matokeo na Coast union halafu matokeo ya Nyota nyekundu dhidi Tukuyu stars na Reli morogoro dhidi ya Ushirika moshi yakafutwa. Sasa tuangalie TFF wana meno ya kuweza kuyafuta matokeo ya Timu kubwa hizi Yanga na Simba iwapo itabainika zimecheza mchezo mchafu ikiwa Yanga watashinda goli 5-0.Simba wawo italazimika kushinda 8-0 ili watete ubingwa wao huku ikitambua kuwa Mwisho wa siku TFF wakiyafuta matokeo yao yote na ya Yanga basi bila shaka Mpinzani wake anabakia kileleni hivyo kombe litatua Jangwani. Simba walichokosea ni ku concentrate zaidi katika mechi ya TP Mazembe huku wakivurunda kwenye ligi Sare mechi mbili dhidi ya Kagera na JKT walikuwa tayari wameshapoteza pointi Nne leo wangekwisha tangazwa mabingwa mara ya pili mfululizo walishatjuwa kuwa TP Mazembe si SIZE yao ila walitaka tu kuwadanganya wasiodanganyika.
 
Kombe ni la Yanga haina ubishi maana before the game Yanga tayari ana advantage ya 2 goals so akishinda hata 1-0 Simba has to win at least 3-0 poleni Simba msiokuwa na makucha Kombe laja Jangwani

Maji maji wameapa watakufa na mtu hapo Simba asipo tembeza mshiko amekwenda na maji.
 
Simba 2: Majimaji 1

Yanga 2: Toto 0

Source:Vodacom Premier League 2010/2011

Simba 2 - 0 Majimaji - Source : Nilikuwepo uwanjani. Hiyo source ya kayuni ni feki maana tuliokuwepo uwanjani tulishuhudia Simba ikifunga magoli yake mwishoni mwa mchezo na hatukuona Majimaji wakifunga goli lolote.

Azam ndiyo watakuwa Bingwa kwa vile hata kabla mechi za Simba na yanga hazijachezwa kila mtu anajua matokeo kuwa yanga itashinda 6 na Simba itashinda 9, so in that situation, only a fool ndo hawezi kujua what is behind those results. Sasa je TFF itashusha daraja Simba na yanga! It won't happen! Hii inadhihirisha kuwa soka bongo ni porojo tupu.

Lakini kwa upande wa pili, nadhani Simba kwa uungwana wao watadraw ili kujiepusha na kashfa maana hakutakuwa na ushahidi kuwa draw inaweza kupangwa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom