Yanga imetikiswa na inasimama mwishoni

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
7,617
16,712
Habari wakuu.

Nimeona nizungumzie kidogo usajili wa Yanga unaoendelea.

Nimekuwa nikifuatilia mpira kwa kiasi chake.

Nimekuwa nikimsikia Jose Mourinho anaposisitiza usajili Bora ndani ya Klub ni kuhakikisha kubaki na wachezaji wako Bora zaidi kikosini.

Mfano miaka ya Karibuni Simba ilitikisika mno Baada ya kuwauza na kuachana wachezaji wake tegemeo Clatous Chama, Luis Miquesson, Larry Bwalya, Thadeo Lwanga n.k

Naona yanga wameshidwa kuwabakisha wachezaji wake Muhimu mno ndani ya misimu miwili.

1. SAID NTIBAZONKINZA
2. FEISAL SALUM.
3. FISTON MAYELE.
4. JUMA SHABAN.
5. JOYCE LOMALISA.
6. YANIC BANGALA.
7. BENARD MORISON.

Naona ghafla wameamua kufanya usajili mzuri kutoka Asec Mimosa.

Je, ikitokea wachezaji wakashindwa kufanya vizuri kama Azizi ki itakuwaje?

Je, wataweza ku copy haraka na kufanya vizuri Katika ligi ya mabingwa maana hakuna mteremko wa kwenda shirikisho.?

Hapo hapo imepoteza Benchi lote la ufundi.

Niwashauri yanga kukaa na wachezaji kwa Muda mrefu iwe angalau kwa miaka isiyopungua 5.

ILa vilabu vyetu bado vina ubabaishaji mwingi sana.
 
Lomalisa kaenda wapi labda..
Huo mchango wa Benard Morrison kwa Yanga ni upi labda katika msimu huo ulioisha?

Saido hakuwepo msimu mzima huo uliopita na Yanga ikafanya vizuri tu nyumbani na kimataifa kwa pengo lake kuzibwa vyema.Mpira Ni biashara Mayele thamani yake imepanda anatakiwa na timu nyingine asiuzwe?

Acha kujitoa fahamu wewe.
 
Screenshot_20230720-100830.png

yanga hawajafanya usajili na wamepoteza wachezaji
 
Lomalisa kaenda wapi labda..
Huo mchango wa Benard Morrison kwa Yanga ni upi labda katika msimu huo ulioisha?

Saido hakuwepo msimu mzima huo uliopita na Yanga ikafanya vizuri tu nyumbani na kimataifa kwa pengo lake kuzibwa vyema.Mpira Ni biashara Mayele thamani yake imepanda anatakiwa na timu nyingine asiuzwe?

Acha kujitoa fahamu wewe.
Saido alianza kuleta ufadha mwingi uwanjani, yani anatoka hata kabla ya kocha hajaamua. Huyu kilichomtoa Yanga ni ukosefu wa nidhamu.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Kwani dirisha linafungwa lini watu mbona kelele mingi,,,,,, kuingiza mchezaji kwenye database ni kitendo cha muda mfupi tu labda kama dirisha ndo lingekua linafungwa
 
Timu zetu kumshikilia mchezaji aliefanya vizuri ni ngumu sana.

SImba au yanga hawawezi tunishiana misuli na timu kubwa za kaskazini.
Tutajifariji tu eti oooh sisi tulitaka pesa, mpira biashara, mwache aende kwani wameondoka wangapi. Nk ila mwisho wa siku uwezo wa kibunda kumbakisha mchezaji aliefanya vizuri na anatakiwa na timu kubwa ni mdogo sana.
 
Back
Top Bottom