SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,151
- 7,918
Huu unaweza kuwa uzi wangu wa mwisho kwa mwaka 2023 na nataka nimalize mwaka kwa ujumbe chanya. Wenye akili zao watausoma na yale watakayoona ni mazuri wataenda kuyafanyia kazi.
Yanga na Simba bado wako kwenye mbio za kufuzu kwenda katika robo fainali ya klabu bingwa ya Afrika. Yanga hajacheza robo fainali ya Klabu Bingwa toka mwaka 1970. Matokeo ya mechi ya kiporo ya CR Belouizdad vs Al Ahly yatatoa mwanga wa ugumu iliyonayo ili kusonga mbele. Vyovyote itakavyokuwa, CRB itakuja kucheza na Yanga ikiwa inahitaji matokeo kwa njia yoyote ile.
Wakati huo huo, kama mnakumbuka mwaka 2018, Mo Dewji aliwahi kutamka kwamba nia na ndoto yake ni kuiona Simba ikiwa moja ya timu 10 bora barani Afrika, malengo ambayo yameshafikiwa katika rank zote za CAF na FIFA.
Ukiangalia rank za CAF na FIFA (rank ya CAF ya miaka 5 na rank ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa vilabu), CRB akitolewa na Yanga hatua hii ya makundi halafu Simba akashinda mechi zake 2 za makundi na akasogea walau nusu fainali, kwa kuzingatia point itakazokuwa imekusanya Simba itapanda katika rank zote za CAF na FIFA hadi nafasi ya 5 kwa ubora Afrika. Kuna uwezekano mkubwa wa Simba kukutana na TP Mazembe hatua ya robo fainali, timu ambayo Simba inaimudu.
Kwa manufaa mapana ya mpira wetu, unaona wazee wa Kariakoo wakikaa chini na kusuka mbinu za pamoja kwa faida ya pande zote mbili? Kufungwa kwa CRB dhidi ya Al Ahly na Yanga inaweza isiwe sababu ya huzuni sana kwa wanasimba na badala yake inaweza kuwa ni chanzo cha furaha kwetu kama Simba itacheza mechi zake zinazofuata vizuri na kuwa timu ya 5 kwa ubora Africa. Na hauwezi jua, tunaweza kukutana nusu fainali tukamkanda uto vizuri tu kiutu uzima.
Niliwahi kuuliza nini kinazuia timu hizi mbili kushirikiana?