Yanayompata Lowassa liwe ni funzo kwa wanaompongeza Rais Magufuli

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,980
Baadhi ya wananchi wamekuwa wakijiuliza bila kupata majibu sahihi kuhusu dhana ya baadhi ya madiwani na wabunge kuhama CHADEMA/upinzani na kujiunga CCM ili kuunga mkono juhudi za serikali ya Rais Magufuli au kumpongeza kwa juhudi zake.

Kinachompata Edward Lowassa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa juu wa CHADEMA wakisaidiwa na manazi wake baada ya kupongeza juhudi za Rais Magufuli ni jibu linalojitoshereza kuhusu sababu za madiwani na wabunge kuhama kutoka CHADEMA/upinzani kabla ya kuunga juhudi za serikali ya Rais Magufuli.

Edward Lowassa ambaye baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA/upinzani walikuwa wanatuambia amewasaidia kuwapatia wabunge zaidi ya 110 na maelfu ya madiwani ameshambuliwa kwa maneno ya kejeli na dharau huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai aitwe kwenye Kikao cha juu cha CHADEMA ili ahojiwe. Kosa lake ni kuainisha mafanikio ya serikali ya awamu ya tano!

Ujumbe unaotumwa na viongozi wa CHADEMA unasema, kama unataka kutoa pongezi kwa serikali na Rais Magufuli, hama kwanza CHADEMA na sio kutoa pongezi ukiwa bado ni mwanachama wa CHADEMA.

Jaribu kufikiria kama diwani au mbunge wa kawaida angefanya aliyoyafanya Edward Lowassa ya kukutana na Rais Magufuli na kupongeza kazi zake. Nina uhakika angefukuzwa uanachama mara moja na kupoteza udiwani au ubunge au angetengwa na kuitwa msaliti.

Kwa Lowassa hawataweza kutoa onyo au kumfukuza Lowassa mara moja kwa sababu ya pesa aliyowekeza kwa wenye CHADEMA na badala yake wanabaki kulalamika kwenye vyombo vya habari na mitandao kwa kutumia mawakala wao.

Wanachama wanaoifahamu vizuri CHADEMA wanajua kuwa ndani ya CHADEMA kuna wenye CHADEMA na watumishi wa CHADEMA wasio na mkataba.

Yaliyomtokea Diwani wa viti maalum CHADEMA jimbo la Tarime vijijini, Mh Philomena Tontora baada ya kuhudhuria maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli ilikuwa ni ishara tosherezi kuwa kama unataka kufukuzwa uanachama wa CHADEMA toa pongezi kwa Rais Magufuli na serikali yake.

Kwa wale wasiofahamu yaliyompata Diwani wa Viti Maalum wa CHADEMA wanaweza kusoma hii thread;
LINK>>Kufilisika kisiasa kwa CHADEMA: Wanataka kumfukuza diwani aliyehudhuria maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli

Yanayompata Edward Lowassa liwe ni funzo zuri kwa wale wanadhani wanaweza kupongeza juhudi za serikali au Rais Magufuli na kubaki salama ndani ya CHADEMA/upinzani.

Wanaomshambulia Lowassa ndio hawa hawa kila siku wanatuamisha kuwa wanapigania uhuru wa kutoa mawazo (Freedom of speech) hata kama hukubaliani nayo. Kwa haya wanayomfanyia Lowassa siwezi kuwatofautisha na simba ndani ya ngozi ya kondoo kwenye kelele zao za kutaka uhuru wa kutoa mawazo!
 
Baadhi ya wananchi wamekuwa wakijiuliza bila kupata majibu sahihi kuhusu dhana ya baadhi ya madiwani na wabunge kuhama CHADEMA/upinzani na kujiunga CCM ili kuunga mkono juhudi za serikali ya Rais Magufuli au kumpongeza kwa juhudi zake.

Kinachompata Edward Lowassa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa juu wa CHADEMA wakisaidiwa na manazi wake baada ya kupongeza juhudi za Rais Magufuli ni jibu linalojitoshereza kuhusu sababu za madiwani na wabunge kuhama kutoka CHADEMA/upinzani kabla ya kuunga juhudi za serikali ya Rais Magufuli.

Edward Lowassa ambaye baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA/upinzani walikuwa wanatuambia amewasaidia kuwapatia wabunge zaidi ya 110 na maelfu ya madiwani ameshambuliwa kwa maneno ya kejeli na dharau huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai aitwe kwenye Kikao cha juu cha CHADEMA ili ahojiwe. Kosa lake ni kuainisha mafanikio ya serikali ya awamu ya tano!

Jaribu kufikiria kama diwani au mbunge wa kawaida angefanya aliyoyafanya Edward Lowassa ya kukutana na Rais Magufuli na kupongeza kazi zake. Nina uhakika angefukuzwa uanachama mara moja na kupoteza udiwani au ubunge au angetengwa na kuitwa msaliti.

Kwa Lowassa hawataweza kutoa onyo au kumfukuza Lowassa mara moja kwa sababu ya pesa aliyowekeza kwa wenye CHADEMA na badala yake wanabaki kulalamika kwenye vyombo vya habari na mitandao kwa kutumia mawakala wao.

Wanachama wanaoifahamu vizuri CHADEMA wanajua kuwa ndani ya CHADEMA kuna wenye CHADEMA na watumishi wa CHADEMA wasio na mkataba.

Yaliyomtokea Diwani wa viti maalum CHADEMA jimbo la Tarime vijijini, Mh Philomena Tontora baada ya kuhudhuria maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli ilikuwa ni ishara tosherezi kuwa kama unataka kufukuzwa uanachama wa CHADEMA toa pongezi kwa Rais Magufuli na serikali yake.

Kwa wale wasiofahamu yaliyompata Diwani wa Viti Maalum wa CHADEMA wanaweza kusoma hii thread;
LINK>>Kufilisika kisiasa kwa CHADEMA: Wanataka kumfukuza diwani aliyehudhuria maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli

Yanayompata Edward Lowassa liwe ni funzo zuri kwa wale wanadhani wanaweza kupongeza juhudi za serikali au Rais Magufuli na kubaki salama ndani ya CHADEMA/upinzani.

Wanaomshambulia Lowassa ndio hawa hawa kila siku wanatuamisha kuwa wanapigania uhuru wa kutoa mawazo (Freedom of speech) hata kama hukubaliani nayo. Hawa ni kama simba ndani ya ngozi ya kondoo!
Ni nani alikuambia ni lazima rais apongezwe?
Rais anatekeleza wajibu wake kikatiba suala la kumpongeza ni jambo la hisani,inafahamika wazi kiu ya CCM kutaka pongezi nyuma ya pazia kuna janga dhidi ya wapinzani.
 
Huyu mleta mada ni wa ajabu sana. Kwa nini usingejipa subira kwanza ndio uje na pumba kama hizi? Yaani jambo limetokea jana, tayari umesharukia eti mbona hajafanywaje sijui. Au lengo ni kutimiza threads mlizopangiwa kwa siku sio?
Mkuu;
Hoja yako ni nini? Kwamba Lowassa afukuzwe au apewe onyo kwa sababu ametoa mawazo yake kuhusiana na utendaji wa serikali ya Rais Magufuli.

Nadhani hujaelewa msingi wa thread yangu.

Soma vizuri ili uelewe vizuri.
 
Back
Top Bottom