Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 14 Aprili 2014 - Uwasilishaji wa Taarifa za Kamati

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
- Lissu: Nyerere alitoa amri yaani Decree na watumishi wote na idara zote za Tanganyika ziligeuzwa kuwa za muungano

- Lissu anamalizia kwa kusema nchi hii ni haramu!!

- Lissu: Tanganyika haikuwawa na Hati ya Muungano bali na amri ya aliyekuwa rais Nyerere

- Mwongozo wa Serukamba kuwa tuko hapa kama nani kama Hati ya Muungano haipo.

- Mtikila ameomba kuongea .. haya .. anamjibu Serukamba kuwa tuko hapa kuandika katiba mpya kwa msingi wa ukweli

- Mchungaji Mtikila: 'tulijengwa kwenye misingi ya uongo ndio maana Mungu alishindwa kubariki hii nchi yetu kwa miaka 50'

- Sasa ni kamati 6 inawasilisha mkiti ni wasira

- Mtikila: Muungano wa Tanzania ni suala la Kitapeli!

- Amon Mpanju: hakubaliani na Mtikila kuwa hatujabarikiwa na pia amehoji utaalam wa Lissu

- Kamati 6 ufafanuzi wa walio wachache utawasilishwa na Ismail Jussa .. msikose..

- Naona wasirra anaongea bila kusumbuliwa

- Sasa sijuwi walio wengi kama wataheshimu pale jussa atakapo kuja kwa ufafanuzi wa walio wachache

- Sasa wassira anawasilisha maoni ya wachache

- Wassira Tukiweka serikali 3 hapa zikaweka masharti kuna watu watapata matatizo, unapunguzia Wazanzibari fursa'

- Wassira anasoma maoni ya wachache cha kushangaza anasitasita na kuyatolea ufafanuzi

- Pia anasoma kama kalazimishwa

- Mwandosia sasa anatowa taarifa ya ajali aliyopata makamu wa rais jana na viongozi waandamizi

- Sitta amsisitiza atoe kwa kifupi tu

- Bunge maalum linatoa pole kwa makamu wa rais na waathirika wote wa mafuriko

- Anawaasa wabunge wote watoe posho zao za siku kuchangia maafa ya mafuriko

-Jussa anaanza na kusema ana waraka ambao haukuwekwa ktk ripoti.

- Jussa: kujadili muundo ni kinyume na sheria ya mabadiliko. Tukitaka kujadili s2 tuunde Tume nyingine

- Jussa: tuhuma nzito kurudisha sultani .. Mkapa alipotoa msamaha kwa sultan alikuwa kama mkiti.wa chama gani?

- Jussa taarifa ya mpanju naipuuza kama navyompuza yeye mwenyewe

- Jussa: anaeleza kuwa chama kitakachorudisha sultani ni CCm

- Jussa: kuleta hoja ya sultani haina mishiko mbona hatusemi kwa Tanganyika tunataka kumrudisha Malkia

Jussa: tukifanya vitu kwa kuzoea tu.. tulipaswa kuendelea na ukoloni? Tanganyika ilitawaliwa na Zanzibar

Jussa: Katiba ya 1965 ilitaja Tanganyika .. sasa ilikufa vipi aprili 1964?

- Jussa: Tanganyika ipo lkn imejificha ivuliwe koti

- Jussa: mwaka 2011 mkiti Sitta ukikutana na sisi Baraza la Wawakilishi wote pande zote tulikuwa wamoja sasa wameufyata!

Jussa: kamtaja Asha Bakari walitoka wote baada ya kukataliwa kuzungumzia masuala.ya utalii sasa anaufyata

- Jussa: mambo yote ya sarafu na benki, elinu ya juu, mafuta, utafiti.. nk yamechukuliwa na kuwekwa Muungano.. tumechoka

- Jussa: Shivji alitaja zaidi sheria 40 zilizotumika kunyanganya mamlaka ya.Zanzibar. Hatukubali

- Jussa: Tanganyika ikiwa imevaa koti la Muungano inatunyanganya mamlaka yetu.Znz .. hatukabali hatukubali

- Jussa amemaliza kuwasilisha kwa makofi makubwa

- Jussa: hansard ya 1965 inaonyesha katiba iliandaliwa kwa siri

attachment.php


Jussa.. ramani ya Zangebar inayoonyesha utawala wa Znz mpk huku Bara

Ufafanuzi wa walio wachache kwa kamati.hii ya mwisho ni Freeman Mbowe

- Mbowe anamshukuru Wassira kwa niaba ya dola atawasilisha Hati ya Muungano

- Mbowe: Fursa hii ya kutibu majeraha. Tuone makosa waliyofanya waasisi wetu kwa nia njema na turekebishe

- Mbowe: lazima tuwe na misingi ya kuandika katiba .. hatuwezi kuandika katiba mpya kwa rushwa.. unafiki

- Mbowe: Ni lazima tuwe na Ujasiri wa kusema ukweli ktk kila hatua ya mchakato wa kuipata Katiba Mpya

- Mbowe: Miongoni mwa watu waliotaka tuwasaidie kufikisha kilio chao sisi tulio wachache ni Makonda!

- Mbowe: tunapata wapi ujasiri kuwatukana wajumbe wa Tume

- Kuna Mjumbe: Kama hayati Mwl Nyerere alikosolewa na kudaiwa ni mwongo; basi hata Wariona na wenzake wanaweza kukosolewa

- Mbowe:Hatupo hapa kutetea 'personality' tunatetea 'issues'

- Mbowe: serikali ya CCM walikuwa na watumishi zaidi 100 walishirikiana na Tume kufanya hii rasimu. Kawataja baadhi

- Mbowe: Tume ya Warioba inapobezwa basi ni kuwa wanaobezwa ni watumishi wa serikali na hata chama tawala!

- Mbowe: taifa limetumia pesa za wananchi bil 68 kufanya utafiti huu

- Mbowe: mnataka kuleta rasimu ya serikali 2 ambayo haipo

- Mbowe: Kuna seminar imefanywa kwa baadhi ya wabunge ikiandaa vifungu vya kuchomeka kwenye rasimu!

- Mbowe: taasisi zenye uwakilishi wa mamilioni ya watu mf CDM, CUF, NCCR, LHRC, Tanganyika Law Society walipendekeza s3

- Mjumbe: Mbowe anapotosha, TUCTA tulipendekeza "Serikali Moja" na si tatu kama alivyodai CWT wadai walipendekeza TATU!

- Hawa Mchafu: TUCTA tulipendekeza s1 .. Oluoch kajibu walimu ni 90% wamependekeza s3

- Mbowe:Tunawaunga mkono wazanzibari wanaoipigania Zanzibar, nasi tunaupigania utaifa wetu wa Tanganyika!

- Orodha imeshatoka ya kuchangia leo.

- Machali:nimestuka leo hii kusikia mjumbe mwenzetu pinda leo anakiri hati ya muungano imepatikana

- Serekali ya ccm mlificha wapi hati hiyo ziku zote

- Machali:menyekiti naomba uwatulize watomvu wa nidhamu

- Machali:tunaitaji maelezo ni kwa nini walishindwa kutupatia hati ya mungano kwenye kamati wanasema leo ipo hicho ni kiini macho

- Machali:taarifa yake nimeisiki lakini ndio walele wenye fikira zilezile za chama ccm aende akawaeleze haohao ccm wenzake

- Sitta anasema kishabiki kuwa machali roho inamuma kwa kitendo cha hati kuonekana

- Kuna mjumbe anasema bi asha atafutiwe mchumba...hahahha...!

- Asha Bakari: Jussa yeye hata kuzaa hajazaa wala kuoa. Yeye ndo kaufyata.

- Kigwangala:tume mpaka kupende keza waliopendekeza kwenye rasimu walifuata mfumo gani?

- Kigwangala:mwendelezo huu wa hizi tume kuvuruga serekali yetu siukubali kabisa

- Na utafiti uliofanywa na tume hautoshelezi

- Zakia:waasisi hawakuwa na maudhui ya s3 walikuwa na maudhui ya s2

- Zakia:mwanasheri wa uganda ndio aliyeitwa kuja kutengeneza hati ya muungano

- Alikuwa mwanasheri maarufu Africa

- Zakia:mimi nimezaliwa znz nimesomea na kuolewa bara watoto wangu wote nimewazalia bara

- Msigala:mfumo ambao mimi nitaupenda ni ule utakaolinda amani na kulinda haki za walemavu

- Ni mfumo ambao hautambebesha garama kubwa mwananchi

- Mpaka sasa bado nashwinda kushawidhika kwa asilimia mia kama s3 sitaleta ufumbuzi wa matatizo nilyoyasema

- Kigwangala anamtuhumu Sitta kwa upendeleo anao utoa kwa walio wachache

- Kigwangala anamkatuza Tundu Lisu hapa.anadai anapotosha kuhusu Shivji

- Lisu anahoji kuhusu amri iliyotolewa na Nyerere kuhusu kugeuza mambo ya Tanganyika kuwa ya Muunngano

- Lisu anaendelea kudai nchi hii haijawahi kua moja na nchi hii ni haramu

- Serukamba anahoji kama hati za muungano hazipo wabunge wapo pale kama kina nani

- Shekifu anamtaka Tundu Lisu athibitishe wale aliodai wameuwa

- Rev. Mtikila anadai tumeishi kwenye uongo kwa miaka hamsini ndio mana Mungu ameshindwa kuibariki

Inaonekana hii hotuba ya Lisu imewagusa wajumbe wengi.

- kamati no.sita inawasilisha taarifa.na muwasilishaji ni Steven Wasira

- Wasira anawahakikishia watanzania kua hati ya makubaliano ipo na ipo ktika hali nzuri na itawasilishwa bungeni ndani ya siku mbili.

anaendelee......

Video: Mh. Jussa akiwasilisha maoni ya wachache.
 
Last edited by a moderator:

Tangu juzi na jana, kumekuwa na vikao vya njama, kutaka kuzuia Tundu Lissu asiendelee na kumalizia kutoa ufafanuzi wake, kama ilivyoagizwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta.

Njama hizo zimekuwa zikipangwa na CCM. Lakini inavyoonekana wameshindwa na sasa Lissu atawasilisha ufafanuzi wa wajumbe wachache katika Kamati Namba 4.

Hila hizo zinaonekana kupitia taarifa hiyo ya Kingwangala...

Mbali ya Lissu, Watanzania watakuwa attention kusikiliza watu wengine wawili, ambao ni pamoja na msemaji wa wajumbe wachache kwenye Kamati Namba 6 ambaye ni Ismael Jussa Ladhu atakayezungumza baada ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Steven Wassira.

Lissu anajulikana kwa uwezo wake na namna ya uwasilishaji wa hoja, hususan zinazohusu masuala ya Zanzibar na Muungano kwa ujumla. Anajulikana kuwa ni mzungumzaji na mwasilishaji mzuri wa hoja zake.

Leo taifa linatarajia kupata mwelekeo wa namna mchakato wa Katiba Mpya utakavyoendelea huko mbele, kutokana na mwenendo unavyokwenda hadi sasa, hasa kwenye hatua ya Bunge Maalum la Katiba kuelekea Kura ya Maoni, itakayopigwa na wananchi, iwapo rasimu hii yenye msingi wa serikali tatu itapaita.

Hapo ndipo penye umuhimu wa kusogea kwenye redio na televisheni yako, kumsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.


 
- Kigwangala anamtuhumu Sitta kwa upendeleo anao utoa kwa walio wachache

- Kigwangala anamkatuza Tundu Lisu hapa.anadai anapotosha kuhusu Shivji

- Lisu anahoji kuhusu amri iliyotolewa na Nyerere kuhusu kugeuza mambo ya Tanganyika kuwa ya Muunngano

- Lisu anaendelea kudai nchi hii haijawahi kua moja na nchi hii ni haramu

- Serukamba anahoji kama hati za muungano hazipo wabunge wapo pale kama kina nani

- Shekifu anamtaka Tundu Lisu athibitishe wale aliodai wameuwa

- Rev. Mtikila anadai tumeishi kwenye uongo kwa miaka hamsini ndio mana Mungu ameshindwa kuibariki

Inaonekana hii hotuba ya Lisu imewagusa wajumbe wengi.

- kamati no.sita inawasilisha taarifa.na muwasilishaji ni Steven Wasira

- Wasira anawahakikishia watanzania kua hati ya makubaliano ipo na ipo ktika hali nzuri na itawasilishwa bungeni ndani ya siku mbili. anaendelee......
 
Jembe linaanza kutupa mambo ya ukweli kwa ushahidi wote hati ya muungano haipo znz wala tanzania bar haipo wala uno
 
Tundu lissu anatoa taarifa ya uongo bungeni, taarifa yake inapingwa na wabunge
 
Kesha sema ushahidi upo kuwa Khasim Hanga aliuwawa


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Tundu kashaanza kumwaga sumu.

kasema Kasim HANGA NA SOMEBODY TWAHA WALIUWAWA NA USHAHIDI UPO.
 
Suala la kuunganisha tanganyika na zenji halikuwahi kujadiliwa kwenye baraza la mapinduzi.
 
Back
Top Bottom