Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 3,013
- 2,044
Kuna siasa za majibizano zinaendelea ndani ya uongozi wa juu kabisa wa CCM na serikali kuu. Mheshimiwa Nchimbi haonekani kufurahishwa na hulka za kikazi za RC wa Arusha na hakai na kitu moyoni mwake, anaweka wazi kabisa kutofurahishwa na kauli pamoja na tabia za Paul Makonda.
Wakati Makonda akifanya kazi nzuri mkoa wa Dar Mheshimiwa Nchimbi alikuwa nje ya nchi akifanya shughuli za ubalozi, Samia alikuwa msaidizi wa moja kwa moja hayati JPM hivyo anamfahamu vyema Makonda.
Naamini Samia anawavuta vijana wa hayati JPM karibu yake wakiwa na uwezo wa kujilipua na hawana aibu kabisa wakiwa kazini. Ni utamaduni mpya wa hayati ambao kwa serikali ya Samia ni wa kawaida kabisa.
Hata kutolewa kwake nafasi ya uenezi ni kwa shinikisho la wakubwa ndani ya CCM wakongwe hawaonekani kufurahishwa na hulka za vijana wa kisasa kina Makonda na wenzake wote wa rika lake na Nchimbi anawakilisha siasa za umri fulani wenye kuheshimu busara na hekima kabla ya kutoa hotuba na baada ya hapo.
Kitendo cha Rais Samia kufurahia namna Makonda alivyokipeleka mchakamchaka chama katika kipindi cha muda mfupi ni ushahidi wa uwepo wa sintofahamu ya chini kwa chini katika uongozi wa juu wa serikali na CCM.
Nchimbi akiwa katibu mkuu wa CCM anapopingana katika hotuba na bosi wake Samia juu ya hulka za kikazi za Makonda sio suala lenye afya nzuri ya kisiasa kwa maana ya muelekeo mzima wa serikali. Nchimbi hana la kufanya vinginevyo Makonda angeondolewa kabisa kutoka kwenye serikali na kurudi mtaani.
Na mpaka muda huu Mzee Kikwete bado ana nguvu ndani ya serikali na anaonekana ni mtu mwenye kupenda sana kuwa karibu na kila kinachoendelea, kule kuombwa kushauri na kutumwa kwenye mikutano mikubwa huko ughaibuni ni ushahidi wa kuhitajika kama mshauri wa masuala nyeti na yenye kuhitaji uzoefu.
Anatumia huko kuhitajika kwake kama tiketi ya kuingiza ushauri wake katika shughuli za kila siku, ni hapa tunapoona namna ambavyo Rais aliyepo madarakani anavyokwazwa na mstaafu anayekuwa nje ya ofisi. Sioni namna yoyote ambayo Nchimbi anakuwa na uhuru wa kufanya kazi pasipo maamuzi yake kutokuwa na chembechembe za hisia za Jakaya Kikwete.
Maamuzi ni yake kumhusu Makonda, Sabaya na Biteko ambao ni masalia halisi ya Bosi wake wa zamani hayati JPM, aendelee kuwa karibu nao kikazi akiwa anaujua uwezo wao au aachane nao kwani Mstaafu Kikwete na kund lake kubwa hawapendi hulka zao za kikazi.
Kinachofikirisha ni ukweli kwamba Kikwete akiwa Rais hakuingiliwa kwa namna yoyote ile na Hayati Mkapa, haonekani kuondoka kabisa kwenye duru za kisiasa akihitajika kwa uzoefu wa ushauri wake na wakati huo huo akiwa na hulka ya kupenda kuhusika kwenye mengi zaidi ya ustaafu wake.