Yanasemwa mengi juu ya ajira za Sensa, nami niseme machache

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Kuna wanaosema ajira hizi za sensa wapewe ambao ni watumishi ili kudhibiti uzembe utakaojitokeza na wengine wanadai wapewe ambao hawana ajira ili walau wapate mitaji.

Makundi yote ukiwasoma katikati ya mstari wana hoja zenye mashiko lakini kuna sehemu nakubaliana kutokukubaliana.

Kundi la kwanza ambao wanadai watumishi waangaliwe zaidi wamesahau Jambo moja. Ajira hizi za sensa hazina uhusiano kabisa na ajira nyingine mtu aliyonayo, kwamba muajiriwa wa TRA aliyeomba nafasi za sensa za NBS aadhibiwe na TRA kwa uzembe atakaofanyia NBS? Hapa inakosekana logic kabisa

Ninachojua kila ajira kuna utaratibu wake wa kinidhamu na hivyo ajira za sensa zina utaratibu wake uliowekwa na NBS na mtu anapoonyesha utovu wa nidhabu ni NBS wanatakiwa kumuwajibisha pekee kwa kosa la ajira ya sensa na si nyingineyo aliyonayo kutoka mamlaka nyingine.

Tukija kwa kundi la pili, hawa wanadai wasio na ajira wafikiriwe kwanza. Kwa kundi hili Nina haya machache, ajira zinapotolewa zinaangalia uwezo wa mtu, katika walioomba sensa na wasio na ajira kuna watu Wana Elimu ya kidato Cha nne tu lakini kuna mwenye ajira na kaomba sensa ana Elimu ya chuo kikuu. Hawa ni watu wawili tofauti, wa kidato Cha nne reasoning yake ipo chini kuliko wa chuo kikuu. Elimu inasaidia kufikirisha ubongo na kutoa maamuzi yenye busara. Madhara ya kutumia vijana wa form 4 ni mengi na ushahidi ninao wa kilichotokea kwenye zoezi la ANUANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI kwenye Halmashauri fulani.

Maoni yangu

i) Kusiwepo na upendeleo wa aina yoyote ile kwenye kazi hii ya sensa, ama mtu ana vigezo vyote achukuliwe yeye bila kujali ni mtumishi au hana ajira. Upendeleo ndio hupelekea kupatikana wasio na sifa wakafanya vituko.

ii) Wote watakaofanikiwa kupata ajira wale viapo vya uaminifu na uadilifu kwa zoezi zima na viapo hivyo viwe vinaweza kumshtaki mtu na kumtia hatiani.

iii) Yawepo makubaliano maalumu kwamba muombaji alipwe baada ya kazi kukamilika na baada ya uhakiki wa kazi ya mtu. Kwa Sababu ni zoezi la kidigitali naamini uhakiki utakuwa wa haraka na yakibainika makosa yoyote akatwe sehemu fulani ya malipo yake. Hii itadhibiti kufanya kazi hovyo. Na pia naamini kunaweza kufanywa hujuma ili kulipa pungufu na hela kupigwa.

iv) Kwa sababu zoezi hili litakuwa na wasimamizi kigezo Cha kusema watumishi wa eneo husika wanayajua maeneo yao ndio wapewe sio sawa. Usimamizi na ufuatiliaji ukiwepo mzuri hata mtu akiletwa kutoka Burundi ahesabu watu wa manzese hatoshindwa. Kigezo Cha kujua eneo kwa kuishi eneo sio sawa kwa Sababu kuna wengi Sana wapo eneo hilohilo kwa miaka 15 lakini hajui mipaka ya mtaa wake.

Mwisho,

Kuna kikundi Cha watu kinataka kuhalalisha umuhimu wako kwa zoezi hili ili wengine wasipewe, kikundi hicho ni hatari Sana. Sifa na vigezo Kama mtu anavyo apewe.
 
Swala hili linafikirisha. Ukimpa asiye na ajira ni huwezi kumwajibisha baadae hata akiboronga tofauti na kada zenye kuheshimu utawala kama kada ya ualimu
 
Kuna wanaosema ajira hizi za sensa wapewe ambao ni watumishi ili kudhibiti uzembe utakaojitokeza na wengine wanadai wapewe ambao hawana ajira ili walau wapate mitaji.

Makundi yote ukiwasoma katikati ya mstari wana hoja zenye mashiko lakini kuna sehemu nakubaliana kutokukubaliana.

Kundi la kwanza ambao wanadai watumishi waangaliwe zaidi wamesahau Jambo moja. Ajira hizi za sensa hazina uhusiano kabisa na ajira nyingine mtu aliyonayo, kwamba muajiriwa wa TRA aliyeomba nafasi za sensa za NBS aadhibiwe na TRA kwa uzembe atakaofanyia NBS? Hapa inakosekana logic kabisa

Ninachojua kila ajira kuna utaratibu wake wa kinidhamu na hivyo ajira za sensa zina utaratibu wake uliowekwa na NBS na mtu anapoonyesha utovu wa nidhabu ni NBS wanatakiwa kumuwajibisha pekee kwa kosa la ajira ya sensa na si nyingineyo aliyonayo kutoka mamlaka nyingine.

Tukija kwa kundi la pili, hawa wanadai wasio na ajira wafikiriwe kwanza. Kwa kundi hili Nina haya machache, ajira zinapotolewa zinaangalia uwezo wa mtu, katika walioomba sensa na wasio na ajira kuna watu Wana Elimu ya kidato Cha nne tu lakini kuna mwenye ajira na kaomba sensa ana Elimu ya chuo kikuu. Hawa ni watu wawili tofauti, wa kidato Cha nne reasoning yake ipo chini kuliko wa chuo kikuu. Elimu inasaidia kufikirisha ubongo na kutoa maamuzi yenye busara. Madhara ya kutumia vijana wa form 4 ni mengi na ushahidi ninao wa kilichotokea kwenye zoezi la ANUANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI kwenye Halmashauri fulani.

Maoni yangu

i) Kusiwepo na upendeleo wa aina yoyote ile kwenye kazi hii ya sensa, Kama mtu ana vigezo vyote achukuliwe yeye bila kujali ni mtumishi au hana ajira. Upendeleo ndio hupelekea kupatikana wasio na sifa wakafanya vituko.

ii) Wote watakaofanikiwa kupata ajira wale viapo vya uaminifu na uadilifu kwa zoezi zima na viapo hivyo viwe vinaweza kumshtaki mtu na kumtia hatiani.

iii) yawepo makubaliano maalumu kwamba muombaji alipwe baada ya kazi kukamilika na baada ya uhakiki wa kazi ya mtu. Kwa Sababu ni zoezi la kidigitali naamini uhakiki utakuwa wa haraka na yakibainika makosa yoyote akatwe sehemu fulani ya malipo yake. Hii itadhibiti kufanya kazi hovyo. Na pia naamini kunaweza kufanywa hujuma ili kulipa pungufu na hela kupigwa.

iv)kwa Sababu zoezi hili litakuwa na wasimamizi kigezo Cha kusema watumishi wa eneo husika wanayajua maeneo yao ndio wapewe sio sawa. Usimamizi na ufuatiliaji ukiwepo mzuri hata mtu akiletwa kutoka Burundi ahesabu watu wa manzese hatoshindwa. Kigezo Cha kujua eneo kwa kuishi eneo sio sawa kwa Sababu kuna wengi Sana wapo eneo hilohilo kwa miaka 15 lakini hajui mipaka ya mtaa wake.

Mwisho,

Kuna kikundi Cha watu kinataka kuhalalisha umuhimu wako kwa zoezi hili ili wengine wasipewe, kikundi hicho ni hatari Sana. Sifa na vigezo Kama mtu anavyo apewe.
Kama mtu wa eneo husika anavigezo ndiye anafaa zaidi kwa ufahamu wa eneo wa haraka na unafuu wa kibajeti wa mamlaka husika. Ni zoezi muhimu wapewe kipaumbele walimu wa msingi na sekondari awe kwenye ajira au hapana ila awe mwalimu na kama hawako vizuri kwenye Tehama waongezwe watu wa fani za biashara na science.
 
Swala hili linafikirisha. Ukimpa asiye na ajira ni huwezi kumwajibisha baadae hata akiboronga tofauti na kada zenye kuheshimu utawala kama kada ya ualimu
Kwamba mtu aadhibiwe kwenye ajira yake ya ualimu kwa makosa aliyofanya kwenye sensa?
 
Kama mtu wa eneo husika anavigezo ndiye anafaa zaidi kwa ufahamu wa eneo wa haraka na unafuu wa kibajeti wa mamlaka husika. Ni zoezi muhimu wapewe kipaumbele walimu wa msingi na sekondari awe kwenye ajira au hapana ila awe mwalimu na kama hawako vizuri kwenye Tehama waongezwe watu wa fani za biashara na science.
Nakubaliana nawe kwa maana ya kwamba inawezekana walimu wakaonesha umahiri na uwezo katika zoezi hili na hiki ndicho Serikali iangalie ubora

Kutokukubali nawe, Kuna wengi wenye uwezo na umahiri kuzidi walimu na hawapo kwenye sayansi au biashara hao pia wanatakiwa kutumika kwenye zoezi hili. Kasumba ya kuaminisha watu kwamba kazi fulani ni kwa kada fulani ndio imetufikisha hapa, kazi zinaborongwa bila matokeo kuonekana.

Nimekubaliana kutokukubaliana nawe, walimu wa kuboronga wapo tena wengi.
 
atakaepewa ni yule atakayetoa 50 elfu kwa mtendaji wa kata pia wale watakaovua vyupi kwa wenye mamlaka wanaweza pia patiwa hizo nafasi
 
Nakubaliana nawe kwa maana ya kwamba inawezekana walimu wakaonesha umahiri na uwezo katika zoezi hili na hiki ndicho Serikali iangalie ubora

Kutokukubali nawe, Kuna wengi wenye uwezo na umahiri kuzidi walimu na hawapo kwenye sayansi au biashara hao pia wanatakiwa kutumika kwenye zoezi hili. Kasumba ya kuaminisha watu kwamba kazi fulani ni kwa kada fulani ndio imetufikisha hapa, kazi zinaborongwa bila matokeo kuonekana.

Nimekubaliana kutokukubaliana nawe, walimu wa kuboronga wapo tena wengi.
uko na point wazingatie sifa za kitaluuma, uaminifu umakini na mengineyo kulingana na matakwa ya kazi husika ili ifanyike kwa tija lengwa.
 
Ushauri mzuri sana.

Pia kumpa MTU aliyepata 'F' ya hesabu kuhesabia watu/takwimu nayo ni dharau kubwa.

Unachukua mwalimu wa Kiswahili au History unampa kazi NBS ni dharau kubwa sana kwa taaluma ya hesabu, uchumi na Takwimu kwa ujumla.
 
Swala hili linafikirisha. Ukimpa asiye na ajira ni huwezi kumwajibisha baadae hata akiboronga tofauti na kada zenye kuheshimu utawala kama kada ya ualimu
Kwamba wasio na ajira hawaruhusiwi kushitakiwa au mimi ndio sielewi! Halafu unadhani wazamini waliwekwa kwa sababu gani?
 
Ushauri mzuri sana.

Pia kumpa MTU aliyepata 'F' ya hesabu kuhesabia watu/takwimu nayo ni dharau kubwa.

Unachukua mwalimu wa Kiswahili au History unampa kazi NBS ni dharau kubwa sana kwa taaluma ya hesabu, uchumi na Takwimu kwa ujumla.
Kikitumika kigezo hiki cha hesabu, wataenguliwa wengi sana kwenye hii kitu maana wengi walikimbia na alerg na hesabu/takwimu
 
Back
Top Bottom