Yaliyojiri: Uhesabuji Kura na Utangazaji Matokeo katika Chaguzi Ndogo kwenye Kata 43 - Novemba 26, 2017

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Heshima kwenu wakuu,

Leo Novemba 26 2017 ni Siku ya Uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 Tanzania. Uchaguzi huu unafanyika kujaza nafasi zilizo wazi katika kata hizo Baada ya Madiwani waliokuwepo Kufariki, Kujiuzulu na wengine Kutenguliwa na Mahakama.

Tutakuwa tunapeana ya kinachojiri kwenye huu Uchaguzi kwenye hii thread. Vilevile Matokeo ya kila Kata yatawekwa kwenye hii thread. Uchaguzi mdogo wa madiwani unafanyika katika Kata 43 ambazo ziko katika Halmashauri 36 kwenye Mikoa 19.

Zifuatazo ni Kata ambazo Zitafanya uchaguzi:

1.ARUSHA
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha = Musa

*Halmashauri ya Jiji la Arusha = Muriet => Idadi ya waliojiandikisha 17,374, waliopiga kura 11,815 sawa na asilimia 68, kura halali 11,757 zilizoharibika 58. Simoni Mollel (CDM) 2,887 sawa asilimia 24.5 na Francis Mbisse CCM 8,586 asilimia 73


*Halmashauri ya Wilaya ya Meru = Ambureni
=>Jasephat Jackson(CCM) 2,057 na Dominick Mollel(Chadema) 1,20

*Halmashauri ya Wilaya ya Meru = Ngabobo=>Solomon Laizer (CCM) kura 820 na Emmanuel Salewa (CHADEMA) kura 353.

*Halmashauri ya Wilaya ya Meru = Maroroni => Yoha Kaaya(CCM) 3,568 na Asanterabi Mbise(Chadema) 1,201.

*Halmashauri ya Wilaya ya Meru = Leguruki => Andason Sikawa(CCM) 3,023 na Daniel Mbise(Chadema) 287.


*Halmashauri ya Wilaya ya Meru = Makiba =>
Samson Laizer(CCM) 2,029, Joyce Martin(Chadema) 608. 1.

*Halmashauri ya Wilaya ya Monduli = Moita => Jumla ya wapiga kura waliojiandikisha 4,417 waliopiga kura 3,059, kura halali 3,006. Aliyeshinda ni
Prosper Damian (CCM) kura 1,563, sawa na asilimia 51.24. Samson Loburu (CDM) 1419 sawa na asilimia 46.52

2.DAR ES SALAAM
*Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni = Mbweni =>
CCM imeshinda kwa asilimia 62.6%,
Chadema 33%,
CUF 3.4% ,
SAU O.3%.

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke = Kijichi=> CCM -2684, CUF- 934, CHADEMA- 813, ACT- 408, ADC- 34, NCCR- 14

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo = Saranga=> CCM. - 6956, CHADEMA - 3202, CUF. - 118, ACT. - 38
MDOE HAROUN YUSUF wa CCM ndio DIWANI wa kata ya SARANGA
saranga.jpg


3.DODOMA
*Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa = Chipogolo => Hosea Fweda (CCM) kura 1,994 na Jafari Simba (Chadema) kura 731.

4.GEITA
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale = Bukwimba

*Halmashauri ya Wilaya ya Geita = Senga => Mgombea Thomas Tumbo (CCM) ametangazwa mshindi kwa kura 2,407 dhidi ya kura 815 za Manyama Charles (CUF)

5.IRINGA
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa = Kitwiru

*Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo => Kimala => CCM 1,104 Chadema 718

6.KILIMANJARO
*Halmashauri ya Manispaa ya Moshi = Bomambuzi =>
Msimamizi wa Uchaguzi, Daima Kapongo ametangaza CCM imeshinda Udiwani kwa kura 2854 dhidi ya kura 1992 za Chadema

*Halmashauri ya Wilaya ya Hai = Mnadani => Nasibu Mndeme(CCM) 1,708, Ezra Nyari( Chadema) 958, Msafiri Hamisi (ACT-Wazalendo) 14 na Maynard Shoo(NCCR-Mageuzi) 3.

*Halmashauri ya Wilaya ya Hai = Machame Magharibi => Martin Munisi(CCM) kura 1,048 na Bariki Lema(Chadema) 595,

*Halmashauri ya Wilaya ya Hai = Weruweru=>
Swalehe Msengesi (CCM)1,410, Moses Kalaghe (Chadema) 706, Haji Ndarai (CUF) 26, Mabranda Msabaha(ACT-Wazalendo) 3 na Friman Massawe (NCCR-Mageuzi) 00.


7.LINDI
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi = Chikonji

*Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa = Mnacho =>, Damian Chilemba (CCM) 1,924 na Onesmo Kambona (Chadema) 637.

8.MANYARA
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ = Nangwa

9.MBEYA
*Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
= Ibighi=> Emmanuel Lusubilo (Chadema) kura 1,436 na Suma Fyandomo (CCM) kura 1,205 hakuna kura iliyoharibika.

10.MOROGORO
*Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro = Kiloka =>
CCM kura 2225, Chadema kura 250 na CUF 390.

*Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi = Sofi => CCM ndiye ameshinda kwa kupata kura 2,099. CHADEMA amepata kura 1,684

11.MTWARA
*Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba =
Milongodi => Manzi Livedo (CCM) ameshinda kwa kura 827, akifatiwa na Juma Mngawa (CUF) kura 819

*Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara = Mikindani Reli
=> Genfrid Mbunda (CCM) 422 Antony Kwezi (Chadema) 356, Mwajuma Hassan (ACT) 27 na Phillipo Mwomba (CUF) 21.

*Halmashauri ya Mji wa Masasi = Chanikanguo =>Nichalaus Syprian (CCM) 928, James Kaombe(Chadema) 773, Musa Nangoha (CUF) 36 na Humphrey Kasembe(ACT) 10.

12.MWANZA
*Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi = Kijima =>
Mgombea Ezekiel Kanzaga (CCM) ametangazwa mshindi wa Udiwani, kwa kura 1, 428 dhidi ya kura 674 za Gabriel Shiloti (Chadema)

*Halmashauri ya Jiji la Mwanza = Mhandu => Mgombea Constantine Sima (CCM) ametangazwa mshindi kwa kura 2,749 dhidi ya kura 1,842 za Godfrey Misana (Chadema)

13.RUKWA
*Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga = Sumbawanga =>
Mgombea wa CCM ashinda kwa kura 1,904 akifuatiwa na Chadema kura 1,446 NCCR 2, DP 2 na CUF kura 1.

14.RUVUMA
*Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru = Lukumbule => Milepa Makande (CCM) kura 1,572, Omary Gaibu (CUF) 1,351, Chadema kura 234 na ACT kura 112.

* Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru = Kalulu=> Rabihi Makumba CCM kura 703, CUF 53, Chadema 58.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga = Muongozi

15.SINGIDA
*Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi = Siuyu =>
CCM kura 1404 Chadema kura 1053

16.SIMIYU
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa = Nyabubinza

17.SONGWE
Halmashauri ya Wilaya ya Momba = Ndalambo

18.TABORA
*Halmashauri ya Wilaya ya Nzega = Nata =>
CCM 2000, CHADEMA 595 CUF 33
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo = Muungano

19.TANGA
*Halmashauri ya Mji wa Korogwe = Majengo
=> Mustapha Shengwatu (CCM) alishinda kwa kura 527 na kuwashinda Abdallah Maonga(Chadema) aliyepata kura 385, Abbas Chomboko (ADC ) kura 17 na Kassim Msenga (CUF) kura 26.

Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto = Lukuza

*Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli => Mamba. =>
Richard Msumari(CCM) ameshinda kwa kura 1,399 akiwashinda Jafari Ndege(Chadema) kura 774 na Nurdini Kipingu(CUF) kura 30. Kwenye kata hiyo jumla ya kura zilizopigwa ni 958 zilizoharibika ni 3 halali ni 955

Karibuni.

UPDATES:

=> Wagombea wawili walijitoa kwenye Huu Uchaguzi. Wagombea waliojitoa ni Ndugu Lunda Rashid Ulaya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka katika kata ya Milongodi Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba na Juma Mohamed Siyame wa Chama cha ACT Wazalendo kutoka kata ya Ndalambo katika Halmashauri ya Momba.

=> Idadi ya wagombea waliobaki katika kinyanganyiro hiki ni 151.

=> Mgombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA Kata ya Sofi wilayani Malinyi mkoani Morogoro,Riko Venance amewekwa chini ya ulinzi na polisi wakati akitembelea kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Mission asubuhi hii.

=> Mawakala wa Vyama Vyote Wametolewa Nje ya Vituo vya Kupigia Kura Kata Zote 5 za Arumeru Mashariki.

Sababu ni Kwamba Fomu za Mawakala Zilipaswa Kusainiwa na Msimamizi wa Jimbo Na Siyo Msimamizi Msaidizi.

=> Zoezi la kupiga kura kuchagua diwani Kata ya Ibighi wilayani Rungwe limeanza saa 1:00 asubuhi hii katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata utulivu. Hali ni ya utulivu

=> KIJICHI, DAR: Mbunge Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) adai CCM wameandaa wapiga kura hewa takribani 2,000 kwa lengo la kuvuruga uchaguzi.

=> Katibu wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Arusha Elisa Stephano Mungure amesema mawakala wa chama hicho kwenye kata za Musa,Ngabobo, Maroroni,Leguruki, wamezuiwa kwenda kusimamia upigaji wa kura mpaka mda huu.Katibu huyo amedai mkurugenzi wa uchaguzi huo ndugu Wilison Mahela ameshindwa kuwapa barua za utambulisho mawakala wa Chama hicho na hivyo kushindwa kuruhusiwa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuingia vituoni..

=> Upigaji kura katika Kata ya Milongodi wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara unaendelea kwa utulivu.

=> Katibu wa Mambo ya Nje Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Jojen Patrick amekamatwa na polisi katika kata ya Kijima, Misungwi.

Yeye ni Mratibu wa Kampeni wa Kata hiyo na alikuwa anahudumia mawakala wa ACT Wazalendo katika uchaguzi mdogo wa Madiwani unaofanyika leo.

=> Huko Kata ya LEGURUKI Halmashauri ya Meru, Mh Paulina Gekul na Wanachadema Wengine Wanne, Wamekamatwa na Polisi Wameplekwa Kusikojulikana. Mawakala Wametolewa vituoni.

=> Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ndugu John Kayombo amekanusha madai ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo kuhusu kuwanyima fomu za mawakala wa chama hicho. Kayombo amesema mawakala wote wa Chadema waliotakiwa kupewa fomu za utambulisho wamepewa fomu hizo toka saa kumi alfajiri.

=>
Uchaguzi.jpg
Katibu wa CCM wilaya ya Itilima mkoani Simiyu amelazwa hospitali wilayani Itilima baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakati akiwasindikiza mawaka wa Chama chake kwenda vituoni kwa ajili ya kusimamia kura

UPDATES: 1200HRS
=>Morogoro. Mgombea udiwani kwa tiketi ya Chadema katika Kata ya Sofi wilayani Malinyi mkoani Morogoro, Riko Venance ambaye aliwekwa chini ya ulinzi kwa takribani saa moja amesema polisi walifanya hivyo baada ya kuhoji sababu za mwananchi mmoja kuzuiliwa kupiga kura.

Alizungumza na Mwananchi leo Jumapili baada ya kuachiwa amesema alipofika katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Mission alipata malalamiko toka kwa mmoja wa wapiga kura aliyejulikana kwa jina moja la Akwilina kwamba amezuiliwa kupiga kura.

“Nilikuwa nahoji kwa nini Akwilina azuiliwe kupiga kura na ndipo nilipoambiwa nasababisha vurugu na kuwekwa chini ya ulinzi," amesema Venance.

Amesema mpiga kura huyo alipoulizwa jina alisema anaitwa Akwilino wakati kwenye kadi imeandikwa Akwilina na hapo ndipo utata ulipoanzia, hata hivyo baadaye aliruhusiwa kupiga kura.

Mgombea huyo ambaye anaendelea kutembelea vituo tayari ameshatembelea vituo 10 kati ya vituo 21 vya kupigia kura vilivyopo katika kata hiyo.
Chanzo: Mwananchi

=> Upigaji kura katika kata 43 unaendelea vema. Vituo vyote 884 vimefunguliwa saa 1:00 asubuhi. Hakuna mapungufu ya vifaa.

UPDATES:1340HRS

=> Freeman Mbowe‏: Pamoja na ukakasi unaoendelea katika vituo mbalimbali nawasihi wananchi wote kwenda kupiga kura. Na nitoe Rai kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA kuhamasisha wananchi kwenda kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi watakaowawakilisha.
dom.jpg

=> Uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Chipogoro mkoani Dodoma unaendelea huku watu wachache wakijitokeza kupiga kura

UPDATES: 1400 HRS

=> CHADEMA: Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amekamatwa na Jeshi la Polisi mchana huu. Pia yeye ni wakala mkuu wa uchaguzi mdogo wa Udiwani wa Kata ya Saranga unaofanyika leo.

=> HALIMA MDEE: Leo ni siku ya pili toka ngome yetu ivamiwe na polisi kuwakamata Campaign Team ya mgombea Udiwani, Polisi wamegoma kabisa kutuambia vijana wetu wameshikiliwa wapi. Hata haki ya kuwapelekea chakula haipo. Kuna maisha zaidi ya uchaguzi jamani.

=> Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, ameagiza wagombea wote wa udiwani katika kata tano Arumeru Mashariki wajitoe katika uchaguzi huo kwani umegubikwa na vurugu. Ameagiza pia mawakala na viongozi wote waondoke vituoni.

=> Iringa. Gari la Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Dadi Igogo limeshambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM. Igogo amesema watu waliohusika na tukio hilo anawafahamu na tayari ametoa taarifa polisi ili waweze kuchukukiwa hatua.

=> Arusha. Wagombea udiwani wawili wa Chadema mkoani Arusha wametangaza kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo unaofanyika leo Jumapili katika Kata ya Maroroni na Embuleni. Wagombea hao ni Asanterabi Lazaro(Maroroni) na Dominick Mollel (Embuleni).

Wakizungumza na Mwananchi wagombea wamesema hawana sababu ya kuendelea na uchaguzi uliotawaliwa na vurugu na hujuma. Mbise amesema mawakala wake wamezuia kuingia vituoni na wengine kukamatwa. Kwa upande wake mgombea wa Embuleni, Mollel alisema anajitoa kwani uchaguzi sio huru na haki.

"Tutaenda mahakamani kudai haki huu sio uchaguzi ni vita," amesema.
Chanzo: Mwananchi
mbo.jpg

=> Freeman Mbowe: Kwa kuwa vyombo vya ulinzi vimeshindwa kulinda watu wetu, naagiza vijana wetu wa Chadema popote walipo waanze kujitetea kwa namna yoyote, Sasa tumeamua kujibu mapigo" amesema Freeman Mbowe mda huu Arusha

=>Saa sita mchana, Mawakala wote wa chadema kwenye vituo vya kupigia kura kata ya mamba Wilaya ya Korogwe wametolewa kwa nguvu nje ya vituo

UPDATES: 1530HRS

=> DODOMA: Mtu mmoja anayedaiwa kuwa mwanachama wa CHADEMA anashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilayani Mpwapwa kwa tuhuma za kugawa fedha katika Kata ya Chipogoro.

=> Mtu mmoja amekamatwa akiwa na orodha ya majina ya wapiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Bwawani, Kata ya Kijichi. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke N.Mbaga amesema.

=> M/kiti wa Chadema Nickson Mbise aliyeshambuliwa kwa mapanga Kata ya Makiba Arusha ashonwa nyuzi 64, kupelekwa hospitali ya KCMC, polisi yathibitisha.

=======

=> Polisi wilayani Malinyi, Morogoro wametumia mabomu ya machozi kutawanya watu waliokuwa wanasogelea kituo cha kuhesabia kura cha Shule ya Msingi

MATOKEO YA AWALI

UPDATE: 1900HRS
Matokeo ya awali ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 yameanza kutolewa kukiwa na mchuano kati ya CCM na Chadema.

Jijini Mwanza matokeo ya awali kituo cha Sokoni A Kata ya Mhandu ni kama ifuatavyo, Amiri Barahila (ACT) kura 0, Sima Costantine (CCM) kura 103, Godfrey Faustine (Chadema) kura 55, Vaileth John (Chaumma) kura 0, Masalu Sebastian (CUF) kura 0, na Beatus Bujiku (DP) kura 1.

Matokeo kituo cha Sokoni B Kata ya Mhandu, Sima Costantine (CCM) kura 106, Barahila Kassim (ACT) kura 0, Godfrey Faustine (Chadema) kura 38, Vaileth John (Chaumma) kura 0, Masalu Sebastian (CUF) kura 4 na Beatus Bujiku (DP) kura 0.

Matokeo Sokoni B -2 Kata ya Mhandu, Amir Barahila (ACT) kura 0, Sima Costantine (CCM) kura 74, Godfrey Faustine (Chadema) kura 42, Vaileth John (Chaumma) kura 0, Masalu Sebastian (CUF) kura 2 na Beatus Bujiku (DP) kura 0.

Kata ya Makiba wilayani Arumeru mkoani Arusha matokeo ya awali kituo cha Patanumbe namba moja, CCM kura 140, Chadema 89 na ACT Wazalendo 2

Kituo cha afya Meta namba mbili CCM kura 158, Chadema 52 na ACT Wazalendo 0


Ofisi ya kata namba mbili CCM kura 163, Chadema 80 na ACT Wazalendo 1.

Katika kata tano amesema chadema amechoka na kunyanyaswa kwani tangu kampeni hadi sasa vituo vya polisi vimejaa wanachama wa chadema

Katika Kituo cha Kanisa la Lutheran namba mbili CCM kura 85, Chadema 76 na ACT Wazalendo 2

Kituo cha Kanisa la Lutheran namba mbili CCM kura 83, Chadema 66 na ACT Wazalendo 0.

Katika Kata ya Senga wilayani Geita Kituo cha Msilale namba mbili, CCM kura 72, Chadema 1 na CUF 8.

Kituo cha Msilale namba moja, CCM 76. Chadema 3 na CUF 6.

Kwenye Kituo cha Shule ya Msingi Buligi CCM kura 138, CUF 13 na Chadema 1.
 
leteni au kashtak ukiwa na ushaidi au subiria muda ufike ili muwakamate pindi watakapo taka kupiga kura... na ili zoezi lifanikiwe, nashauri Mr. Zito uwe mmoja wa wakala ktk moja ya kituo kwa ajiri ya kuchunga kura zenu...
 
Visingizio kabla ya kura susieni uchaguzi!

Hiyo propaganda kwamba mnakubalika mneitunga wenyewe kisha mkaiamini. Sasa naona hamko tayari kusononeka kwa kujua ukweli kwamba hamkubaliki. Kwa aina ya unyama ccm mnaowafanyia wapinzani ni dhahiri mnachodhani mnakubalika hivyo mnajidanganya. Huu mchezo wa kutumia dola kuonyesha umma kwamba mnakubalika hata Idd Amini na Mugabe walitumia sana mbinu hiyo.

Hebu hata ww mwenyewe jiulize, mmejaribu kutangaza kila mnachodhani ni kizuri. Wapinzani hawapewi nafasi yoyote kujitangaza na wanapotangazwa ni kwa mabaya tu, lakini bado watu wengi wanawaunga mkono wapinzani. Kwenye kampeni za ccm mnahubiri maendeleo mnayoamini yatawabeba, lakini mnaona hayatoshi mnaishia kutoa vitisho na kuonyesha vyombo vya dola vinawatii. Hata leo mtatatangazwa washindi sio kwa kukubalika bali kwa kulazimisha.
 
kauli za mfamaji,kwani kazi ya mawakala wenu ni ipi??tatizo hata hao mawakala wenu wananunulika kirahisi sana,kama mngeweza kuwa na mawakala ngangari sidhani kama mngekuwa mnalialia kama hivi...

Kama mawakala na wagombea wa Upinzani wamekamatwa na Polisi usiku wakuamkia Leo kuna Uchaguzi tena hapo?

Ni bora CCM mnegesema Rais atateua wagombea kwenye nafasi zote zilizowazi Tume ya Uchaguzi usitangaze nafasi hizo tungewaelewa.Lakini mpaka sasa CCM mmeprive upumbavu
 
Back
Top Bottom