Nimepiga kura katika kituo kimoja hapa nchini, nilichokishuhudia kwa macho yangu ni kwamba ndani ya chumba kinachoratibu upigaji kura hapo kituoni, wakala wa CHADEMA amezuiliwa katakata kuingia katika chumba hicho.

Humo ndani nimekuta wakala wa CCM akiwa ametulia peke yake.

Wakala huyo wa CHADEMA kwa uchungu amekaa nje huku kukiwa na askari wa kituo maeneo hayo akiangalia kwa makini ili asifurukute.

Huu ni uporaji wa haki ya mtanzania kupata kiongozi kwa ridhaa yake bila uchakachuaji.

Pia na taarifa za mawakala wa CHADEMA kuzuiwa kuingia katika vyumba vya kkutoka vituo vingine vya jirani ni hizohizo.

CCM wameona hali imekuwa ngumu kwao, wameamua kufanya uhuni na dhulma.

Kitendo hiki cha kidhalimu ni ushahidi kuwa CCM imekosa ridhaa ya wananchi wanalazimisha ushindi.

Ngoja tuendelee, lakini ukweli ni kuwa NEC inaharibu huu uchaguzi.
Wapi huko mkuu
 
-Taarifa rasmi kutoka jimbo la moshi mjini ni kwamba jana waliondolewa mawakala 54 wa chadema, ikabidi mawakala wote waungane kwa wingi wao kwenda halmashauri saa 8 usiku kudai haki yao ya kusimamia kura za Chadema baada ya mvutano mkali kati yao na Mkurugenzi, wote wakarejeshwa
 

Attachments

  • 20201028_093110.jpg
    20201028_093110.jpg
    222.9 KB · Views: 1
Sio wewe peke yako watanzania karibia asilimia hamsini (50%) wamelitekeleza ,kila anaetoka unamsikia tiki kwa wa mwisho ,wa mwisho kuwa wa kwanza kwenye matokeo, ndio codes ya ushindi.
Vituo vingi wapiga kura wengi wanawafokea mawakala wa chadema kwa kuwatuhumu na kuwa fokea wafanyakazi wa tume, hivyo wapiga kura hao kuchukizwa na hivyo vitendo na kuwaambia hao mawakala wa chadema wanataka kulianzisha kitu ambacho hakipo.

Hiyo ni Dalili tosha kuwa wapiga kura hao wanataka kupigia chama gani.
 
Tume ya taifa ya Uchaguzi wameweka jina la Lissu mwisho kama ambavyo alikua wa mwisho kurejesha fomu za kuteuliwa na tume, Hawajafanya hivyo kimakosa ila kiimani wanasema wakwanza atakua wa mwisho na wa mwisho atakua wa kwanza.
Utetezi dhaifu sana huu, kwani waliondaa ratiba ya wagombea urais kurejesha form ni nani kama sio hao hao NEC CCM?
 
Aiseee muitikio wa Vijana ni hafifu mnoo..

Wengi ni kina Mama watu wazima na wazee..

Hii si nzuri.. Akina mama watalichagua jiwe
 
Wakuu nina shida

1.sikumbuki kituo cha kupigia kura
2.Kitambulisho kimepotea
3.Namba ya kitambulisho siikumbuki


Na ninataka kupiga kura
Sharti lazima ujue ulijiandikisha wapi kupiga kura. lingine ukikosa kitambulisho cha kupiga kura unaweza kwenda na kitambulisho cha NIDA lakini majina ya kitambulisho chako cha NIDA lazima yafanane na yale yaliyokwenye 'daftari la mpigakura'!
 
-Jimbo la Muheza, mawakala wa @ChademaTz zaidi ya nusu ya mawakala wamezuiwa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura. Pamoja na hivyo, @yosepherfkomba anasema kwamba wamebaini baadhi ya kura feki zikiratibiwa na wasimamizi wa vituo. Tunaendelea kuweka rekodi sawa. Taarifa ni muhimu.
 
Kwa picha nililoliona kituoni hapa hii ngoma ngumu kuliko 2015.Mimi ni mwana CCM japo mwaka huu nilitamani mabadiliko ya kweli kidogo ili kurejesha nidhamu. Nilitamani tugongwe ili tufike mahali tuanze kuheshimu thamani ya maisha ya Mtanzania. Refa ngekua fea tusingetoboa hii mbungi
 
Back
Top Bottom