Wakubwa si kama nabeza ila nakumbusha tu kuwa Jf ya leo ni habari taarifa au habari za kipambe na inaweza kutekwa na mtu mmoja ama grupu dogo la waitu.

Kinachokosekana ni habari za kiuchunguzi. Sifa ya Jf ni habari za kiuchunguzi na critical discussions.

Katika siku hii ya uchaguzi tunaomba habari za kiuchunguzi zipewe nafasi. Tuambie Jimbo Fulani nini mtizamo wa wapiga kura. Kundi gani linaonekana kujitokeza zaidi rika jinsia. Mawakala wa upinzani wapo vituoni? Nini tabia ya wasimamizi na wanausalama Katika kituo husika.

Matokeo yamebandikwa mda gani au hayakubandikwa, nani anaelekea kushinda Kama mambo yataenda kihalali.

Rushwa ipo au haipo, vitisho na uwezekano wa kuvurugika amani
 
Mtaani kwetu tunamalizia kujikusanya bado mtu mbili ifike idadi yetu tulioahidi kumrudisha Magufuli halafu ndio tuelekee machinjoni.

Leo ndio leo lazima tuchinje kuwadi wa mabeberu. Kura millioni 22 alizotabiri Polepole lazima zifike.
 
Pambaf hawa, vyama vilitakiwa kuwa ktk alphabetical order. Mtu anajifanya kuweka Mungu mbele lkn anashinda na kuzunguka na Sangoma!

Mimi wala sikutaka kuangalia juu, directly nimeenda kwa mkombozi, tiki na kuondoka. Shime twendeni tupige kura ili kuwatoa hawa na flyover zao.

"mwanamwana, post: 37145583, member: 50047"]

Eti sababu ni kwamba Magufuli alirudisha fomu wa kwanza na Lissu wa mwisho. Utetezi usio na mashiko kabisa.
 
Muda utatupa majibu, Hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino upo,itachukua muda kutangazwa ila ushindi ni wetu CHADEMA.

Mpaka sasa asilimia 80% ya kura zimeenda kwa yule msiyempenda, bado zile za ziada inabidi zipunguzwe chache apewe mzee wa dakika 89
 
Muda utatupa majibu, Hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino upo,itachukua muda kutangazwa ila ushindi ni wetu CHADEMA.
Kamanda kura tumeshahesabu bado chini ya masaa mawili wenye nchi waichukue kwa mara ya nyingine, fuatilia zaidi mawakala wenu wanafanya nini halafu ndio utaelewa, huku kwenye mitandao tunajazana upepo tu ili ukiingia mtaani ndio utaelewa hali halisi.
 
Nauliza ni lini ITV, REDIO ONE na taasisi zenu mmekuwa taasisi za Chama cha Mapinduzi?
Mnako elekea mtasuswa kama TBC na UHURU.

Tangu alfajiri mna tuletea taarifa za watu wa CCM tuu. Mmetoka Zanzibar kutuletea taarifa za Mwinyi na mkewe na kina Kificho mkaenda Mbeya taarifa ni za Tulia na mumewe. Hivi wapinzani hapo juko vituo vya kupigia kura..

Nashauri jitathimini mnako elekea sio kuzuri. CCM haita wasaidia chochote baada ya huu uchaguzi. Mnakwenda kufa kama taasisi nyingine za CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Narudia tena, kama kigezo ni hicho, mbona mtiririko sio huo kwa nafasi za ubunge na udiwani? Maana huko kurudisha kulitofautiana pia. Lisu hahitaji upendeleo wowote bali Magufuli ndio anahitaji upendeleo. Utaratibu wa mpangilio ni alphabetical order,. Sio huo uhuni wa kitoto.
Tindo nenda kapige kura!

Lissu hata angekuwa wa kwanza haingesaidia kitu.
 
Kwa hali ilivyo na aina ya watu mpaka washabiki wa CCM wanavyosema magufuli hashindi hata kwa dawa, watu wengi makada wanadai magufuli kawaletea njaa na wamempa Lissu kwa hasira.
 
Mimi tayari Niko kituoni. SAA 9:45.

SAA ya Ukombozi ni sasa, majuto ni Mjukuu, usifanye makosa
Kweli hapo umenipiku, yaani saa 9:45 upo kituoni! Mimi nilikuwa kituoni toka saa 11.00 Alfajiri nimetoka saa 2:47 asubuhi. Tumeanza kupiga kura kuanzia saa 1:35 asubuhi. Wasimamizi wametupanga upande mmoja akina mama (wanawake) upande mwingine akina baba (wanaume). Msaidizi anaita kutoka kila upande. Mambo yanaenda vizuri.

Jambo moja tu la kurekebisha kwa usimamizi wa uchaguzi kwa siku zijazo ni hili. Tunapenda sana wenzetu ambao wana matatizo ya Afya, wazee, akina mama wanaonyonyesha, wajawazito na walemavu wapewe kipaumbele cha kuwahi kupiga kura ili wakapumuzike na wasikae kwenye foleni muda mrefu. Lakini kwa kuwa kuna wengine wamewahi sana pale kituoni ili wakapige kura hasa kwa upande wa akina mama lakini mpaka naondoka walikuwa bado hawajuruhusiwa kuingia kupiga kura.

Hii ni kwa sababu kuna mama wanaonyonyesha walikuja baadaye na walikuwa wengi na wao ndiyo sasa wakawa wanaruhusiwa kupiga kura. Hii imekera wale wa mama waliowahi pale kituoni. Na nimeacha kuna dalili baadhi watalazimika kuondoka bila kupiga kura leo.

Nimejaribu kuwashauri wasimamizi waangalie namna bora ya kutokuwakera wapiga kura hawa; wasimamizi hawakutaka kabisa kunisikiliza wakasema wao wanafuata masharti tu yaliyobandikwa pale nje kwa ajili ya mpigakura . Na mimi sikutaka kulazimisha maana sina mamlaka hayo.

Nilitaka kuwashauri kuwa wale wenzetu waliopewa kipaumbele kupiga kura kwanza iwe ivyo waendelee kupewa kipaumbe hicho. Lakini iwe hivi, wakipiga kura wawili wale ambao hawana kipaumbele basi ndiyo aingie mmoja mwenye kipaumbele cha kupiga kura kabla ya wengine. Binafsi nadhini hili lingepunguza manung'uniko na kukereka kwa wapigakura hawa.

Kwa hiyo, ushauri niliyotaka kuwapa wasimamizi wa kituo hicho nilipokwenda kupiga kura leo, ni maoni yangu kuwa uchaguzi ujao, basi ushauri huu ufuatwe. Nadhani hili litarekebeshwa kwa kufuata sheria na taratibu za nchi yetu ili sheria za Uchaguzi za nchi ziakisi utatuzi wa kero hii.

Nawatakia uchaguzi mwema.
 
Wakuu nina shida

1. Sikumbuki kituo cha kupigia kura
2. Kitambulisho kimepotea
3. Namba ya kitambulisho siikumbuki

Na ninataka kupiga kura
 
Back
Top Bottom