Yaliyojiri Mkutano wa Waziri Nape Nnauye na Waandishi wa Habari: Kamati haijamaliza kazi

Unaona umeshindaaaaa.For your information Serikali ya JPM ilianguka ijumaa.Kwa kawaida Redio au TV ikiyekwa maana yake aliyeiteka ndiyo Rais wa siku au muda ule.Hivyo Makonda alikuwa Rais ni Mpumbavu kama wewe watashangilia alichofanya huyo punguani wako Bashite.

Mmmh yaani siku hizi humu kuna lugha za hatari kweli.Mawazo,yako,yangu na yule hayawezi kufanana hata siku moja.Kwa hiyo tupunguze hasira tujitahidi kutumia lugha ya kistaarabu tunapowajibu wenzetu ambao tutaona tunatofautiana mawazo.Sisi sote ni Watanzania
 
Kwanini chadema ndio mnashadidia sana mambo ya udaku
Kama yapi? Ivi kukemea Vyeti feki na umafia unaofanywa na wateule ni udaku?
Unamaanisha Nape naye ni CHADEMA na pia ni mdaku? Jiongeze chukua hatua leo kwahuyu kesho kwako.
Uhakika wa Vyeti mmeuanzisha wenyewe mmetimua watu kwenye kada mbalimbali. Mkafikia hadi wengine kuwaita vilaza kwasababu hawakufiksha wastani wa division 2 ama 1.
Je na asiyefikisha hata wastani wa division 4 tumuiteje?
Tanzania haihitaji vilaza piga kelele waachiea nafasi vipanga waongoze
 
Hivi Jakaya yuko wapi?Anafuatilia kweli hii amsha amsha inayoendelea?
kwasasa nchi inaongozwa na jeshi la mtu mbili tu.
hakuna cha makamo,waziri,wala pm,wote kimya dadadeki.wanafanya wanavyotaka wao.hala anaejiona kidume ajitokeze.

YAANI BORA ULEWE POMBE KULIKO KULEWA MADALAKA YA KUONGOZA WATU. UTATAMANI UITWE MUNGU.
 
Hizi episode zilikuwepo toka enzi ya Farao na wana Wa Israeli. Wakati yule mwanafunzi anapigwa ngumi na mateke kule Mbeya mawaziri wote walicharuka kuwa watawachukulia wale walimu hatua Kali. Wakati yule mama akichapwa viboko hadi akazimia na mimba ikatoka waziri Wa afya alisema atasimama kidete kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua Kali. Hiyo ilikuwa ni huko mkoa Wa Mara, Mpaka Leo kwa matukio hayo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. Leo hii hakuna hata MTU mmoja aliefungwa kwa ishu ya madawa ya kulevya.

Leo hii hakuna hata kiwanda kimoja kilichojengwa pamoja na kelele za serikali ya viwanda.
Episode,, Episode...mpaka mwisho.
 
Hapa kazi tu
Furaha Mh. Makonda anasingiziwa

Naona waliosoma na uwaziri wote wanachagua tume ya upande wa upande huo huo, ha ha haaaaa viroja... hata kujaribu kuvuta wawili wa kwingine halafu ungejaribu kutegemea watatu uliowapanga wapi fikra hazikuwepo. Huwa nasema hamjui uongo. Nendeni shule za uongo mkafundishwe

Tume ina wa

1. Idara ya habari
2. Jukwaa la wahariri
3. Mhariri gazeti la Nipashe
4. Wapo redio
5. TCRA

Hapa ha ha haaaaaaa, gemu mbovu aliicheza na afikirie next time kupanga mambo na kusubiria.

Halafu kujiuliza by Mon morning aliwapataje wakawa wameshakubali kazi hiyo, na alifika mida hiyo hiyo ofisi za kwenye tukio.

Nape nape, hukujipanga danganya hao wafata mikumbo sio akina sisi.

Uongozi tunauona kwa Makonda

Jembe la Taifa

Makonda oyeeee
 
Sijui unakuwaga maeneo gani unapo andika hoja zako yaan ni kituko juu ya kituko sijui nimiongoni mwa wale walio soma shule inje ya mfumo rasmi mana unaandika utumbo haswaaa ndio nn sasa umeandika
 
huyu nape vuvuzela ndio anapaswa kujihuzulu otherwise anabaki kuwa mpiga domo kama mnywa kahawa. makonda go on in magufulis voice...
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, leo Jumanne, Machi 21, 2017, atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari, Saa 7 mchana katika Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA). Atatoa msimamo wa Wizara ya Habari kuhusu kadhia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, baada ya kuvamia ofisi za Clouds Media.

Jana asubuhi Waziri Nape aliunda Kamati ya watu watano ikiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, ili kuchunguza tukio alilolifanya Makonda kabla ya kutoa tamko rasmi la Wizara anayoiongoza.

==========
UPDATES:

Tunasubiri wahusika kufika ukumbini baada ya kufika tutawataarifu muendelee kuwa na subira.

Mpaka muda huu 13.28 wahusika hajawafika ukumbini.
Taarifa kutoka kwa Waziri wa Habari na Michezo Nape Nnauye.

"Kuna simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!" - Nape Nnauye

Labda simu kutoka juu ikaonya kukusanyika maana sharia inakataza ya mwaka 2016 kifungu cha ikuru na kidogo cha waziri mkuu.
 
Kamati ilishakufa hata kabla ya kuundwa! Ukiangalia ule ugeni wa pale Clouds Media kwa wale wenye kujua taratibu za nchi!!

'Unaunda Kamati ya kwenda kumtafuta mhojiwa then ukipata upande namna ya kumhoji ndani ya saa 24 halafu utoe taarifa kwa Waziri naye aitangazie Dunia'

Kitu ambacho hakitatokea unless otherwise
 
Jamani, jioni ndio hii, masaa 24 yamekwishapita kitambo ila hakuna tulichotarajia kukisikia!

Sio kesi, sasa naomba kujua taaluma gani ilizuia kutoa habari ambayo haikuwa inabalance story kitaaluma ambayo ilishinikizwa kurushwa ktk luninga wakati huohuo kukarushwa kipindi cha taarifa ambayo nayo haikuwa imebalance stori na watu wakashangilia!?

Taarifa ya Ruge kumbe nayo kitaaluma ilipaswa itolewe kukiwa tayari na stori zinazobalance pande mbili!

Pamoja na Nape kuliona hilo, aliruhusu taarifa na kuipongeza wakati haikuwa inabalance stori na yeye kwa kujisahau ama kutumika vibaya akaunda kamati ambayo itatoa tathmini halisi ya kinachotajwa kwa kuzingatia pande zote mbili, cha kushangaza akatoa laana kadha wa kadha kwa kusikia stori ya upande mmoja!

Sasa watu na taasisi mbalimbali wanaendelea kutoa matamko na laana lanja wa kadha kwa kupitia kauli ya Nape kuhukumu mora kwa moja bila kusubiri ripoti ya Tume aliyoiunda!

Vipi endapo kamati wamebaini story ilikuwa ya kupikwa, itahitokezaje mbele ya kamera kutoa ripoti ukizingatia matamko na laana zilizotajwa na watu juu na RC wenu?

Hii si ilikuwa ni sawa na kumkamata mtuhumiwa na hatia ama uthibitisho mkononi kwa kuwa cctv camera zilirekodi matukio?

Vipi mpaka sasa ripoti haitoki? Aidha, kwa akili zangu yaweza kuwa Makonda kakataa kutoa ushirikiano kwa kuwa tayari upande mmoja na waziri wamekwishatoa hukumu na matamko kadha wa kadha!

Ndio maana nasema, tumeingizwa kanyabazongo!
 
utangoja sana. nape ameunda kamati ya uchunguzi chini ya sheria ip??????
 
C7c6xTxX0AIW7_W.jpg
 
Back
Top Bottom