Yaliyojiri Mkutano wa Waziri Nape Nnauye na Waandishi wa Habari: Kamati haijamaliza kazi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, leo Jumanne, Machi 21, 2017, atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari, Saa 7 mchana katika Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA). Atatoa msimamo wa Wizara ya Habari kuhusu kadhia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, baada ya kuvamia ofisi za Clouds Media.

Jana asubuhi Waziri Nape aliunda Kamati ya watu watano ikiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, ili kuchunguza tukio alilolifanya Makonda kabla ya kutoa tamko rasmi la Wizara anayoiongoza.

==========
UPDATES:

Tunasubiri wahusika kufika ukumbini baada ya kufika tutawataarifu muendelee kuwa na subira.

Mpaka muda huu 13.28 wahusika hajawafika ukumbini.
Taarifa kutoka kwa Waziri wa Habari na Michezo Nape Nnauye.

"Kuna simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!" - Nape Nnauye
 
No longer at ease..... Badala mtu kuwaza kazi ilivyo ngumu, kutatua matatizo ya jamii kunatokea mzigo mwingine unakumbatiwa na kufanya kazi iwe ngumu zaidi. Inabidi ufanye kazi maradufu, ufikirie maradufu bila sababu za msingi.
 
Hamna chochote atakachofanya. Bashite mwenyewe keshaomba radhi uongozi wa clouds media. Kilichobaki ni bla bla bla. Kwa kauli ya jana ya mkulu ya kumkingia kifua bwana bashite unategemea kusikia kitu gani?

Businesse as usual. Hamna kitu. Ccm ni ile ile
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, leo Jumanne, Machi 21, 2017, atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari, Saa 7 mchana katika Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA). Atatoa msimamo wa Wizara ya Habari kuhusu kadhia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, baada ya kuvamia ofisi za Clouds Media.

Jana asubuhi Waziri Nape aliunda Kamati ya watu watano ikiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, ili kuchunguza tukio alilolifanya Makonda kabla ya kutoa tamko rasmi la Wizara anayoiongoza.

[HASHTAG]#LiveUpdates[/HASHTAG] leo tutakuletea LiveUpdates za Kile Kitakachojiri kwenye mkutano wa Mh. Nape Nnauye pamoja na waandishi wa Habari.
But why all this mess.Why doesn't sense prevail?Usanii mtupu.Ipo shida kubwa katika serikali ya awamu ya tano_Only God knows where we are heading to.
 
Back
Top Bottom