Yaliyojiri Mkutano wa Edward Lowassa, Musoma mjini - Oktoba 11, 2015

Mhhhh yaniii ni shidaaaa... Kupoteza Muda tuuuu uku.. Uchaguzi wa urais umeshaisha NEC wajikite kwenye ubunge na udiwan...... White hair white house.... Viva Lowassa...... Kwel nimeamini watu ufuata majira na siyo majira ufuata watu... Edo hachafukiki na wala hazuirik.... When God says yes no one can say otherwise.....
 
Nimecheka sana kumbe tuko wengi...... Niko CCM lakini kwa hali hii itakua usaliti wa sauti ya umma....... LOWASSA anatisha guys tumpeni kura, tumpelekeni ikulu..... Kazi aanze rasmi...
 
Acheni zenu.. Mnataka mtu ambaye Ni fisadi apewe Nchi? Kamanda Wa Anga mbowe, Na wenzio mmetuaminisha miaka nenda rudi kuwa ENL Ni Fisadi, hafai kupewa nafasi ya kutuongoza iweje Leo mumkubali aingie madarakani? Tena kupitia Chama chetu tuku

Labda wewe unachotaka ni nini Ungana na Slaa Sisi Tunaenda Chukua Nchi na Lowasa Wetu Gari ikospid ukishuka tunakuacha hatunamda wa kusubiri
Bilashaka we ni IT Masaki
 
Picha za kuunga unga za nini hizi?? Musoma watu mmewabeba toka Sirari na Nyamuswa mnasema ati wa Musoma? CCM ni mbele kwa mbele. Ngoja Kinana aje hapo muone atakavyo wasambaratisha.
Aaaaah mbavu zangu. Lizaboni, njoo wanakinanga chama chetu huku, Mr. Chin upo wapi kyama kyinauzwa huku kwa picha za kuokoteza jalalani zile za Mrema na Dr Muhogo

Kwa miaka hamsini ya uhuru kama wewe ni mtanzania halisi na ukaendelea kuitumainia FISIEMU itabidi ukapimwe akili,

Hapa kazi tu mpeni mulley,lowasa ndo mpango mzima.
 
Hujawahi kushabikia japo "Ready"?

Sio rahisi kuelewa hata kishangiliwacho
 
"This is the comming president of United Republic Of Tanzania." Nabii Tb. Joshua
 
Mods bwana kuna maisha baada ya uchaguzi, acheni ushabiki na mahaba kwa ccm. Kila kitu na majira yake, haya ni majira ya mabadiliko, kubalini.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tunapenda kuwataarifu wanachama wetu na umma wa Watanzania kuhusu masuala yafuatayo:

Mwenendo wa Kampeni za CCM

Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, na Mgombea Mwenza, Ndugu Samia Hassan Suluhu, wameendelea kufanya kampeni katika maeneo mbalimbali nchini..

Hadi jana, tarehe 10.10.2015, Dkt. Magufuli alikuwa amekwishatembelea Mikoa 22 na Majimbo 203. Amekwishafanya mikutano mikubwa rasmi 240 na mikutano 865 ya kusimamishwa na wananchi njiani, hasa wananchi wa vijijini. Dkt. Magufuli amekuwa akitumia usafiri wa barabarani, ambapo hadi sasa ametembea kilomita 31,467 kwa barabara kuu, barabara za mikoa, barabara za wilaya, barabara za mlisho (feeder roads), na barabara za mijini na vijijini.

Watu wengi wamekuwa wanajitokeza kwenye mikutano yetu. Lakini la muhimu zaidi ni hamasa na matumaini wanayopata baada ya kumuona jukwaani na kumsikiliza Dkt. Magufuli. Wananchi wanapoondoka kwenye mikutano yetu ya kampeni wanakuwa wamepata fursa ya kumsikia mgombea wetu kwa kitambo kinachotosheleza, wamemuelewa, wameelewa sera za CCM na wameshawishika kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi.

Tunaingia katika ngwe ya mwisho ya kampeni zetu. Tangu kampeni zianze hadi sasa, ushindi wa CCM unajidhihirisha. Hata hivyo, katika kujihakikishia ushindi na kuongeza kiwango cha ushindi, katika ngwe hii ya mwisho, tumeanza kampeni nzito.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameanza ziara ya kampeni katika majimbo 64. Vilevile, viongozi wengine wa CCM, akiwemo Rais na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa, nao wataanza safari za kuzunguka nchi nzima kumuongezea kura Dkt. Magufuli na wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Tutatumia helikopta nne kwa ajili ya shughuli hii. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wataendelea kutumia usafiri wa gari hadi mwisho wa kampeni, isipokuwa pale tu itakapokuwa hakuna budi.

Maandalizi ya Kuleta Mabadiliko ya Haraka na ya Kweli

Pia, tunapenda kutoa taarifa kwamba, mgombea wetu, Dkt. John Pombe Magufuli, ameunda jopo la wanataaluma na wataalamu huru magwiji wazalendo wa uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, kwa ajili ya maandalizi ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini kuanzia siku ya kwanza atakayokuwa madarakani.

Dkt. Magufuli amelipa jopo hili majukumu yafuatayo:

1. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

2. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

3. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali;

4. Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa.

5. Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania;

6. Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.

7. Kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa.

8. Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.

9. Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika;

10. Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini.

Dkt. Magufuli ameazimia kuanza kazi mara moja kwa bidii kubwa na maarifa mapya.

Imetolewa na:-

January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
11 Oktoba 2015
 
Acheni zenu.. Mnataka mtu ambaye Ni fisadi apewe Nchi? Kamanda Wa Anga mbowe, Na wenzio mmetuaminisha miaka nenda rudi kuwa ENL Ni Fisadi, hafai kupewa nafasi ya kutuongoza iweje Leo mumkubali aingie madarakani? Tena kupitia Chama chetu tukufu?
Nilitaka kukujibu,jina lako limenichosha kbsa.....
 
Aiseh magufuli ana akili sana..kura yangu kaipata achaneni na hao wapiga deal wasio na tija...wamekuwa waziri wakuu wakitufanyia nn hapa pombe tuuu genge la walanguzi 2a ukawa tupa kule
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tunapenda kuwataarifu wanachama wetu na umma wa Watanzania kuhusu masuala yafuatayo:

Mwenendo wa Kampeni za CCM

Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, na Mgombea Mwenza, Ndugu Samia Hassan Suluhu, wameendelea kufanya kampeni katika maeneo mbalimbali nchini..

Hadi jana, tarehe 10.10.2015, Dkt. Magufuli alikuwa amekwishatembelea Mikoa 22 na Majimbo 203. Amekwishafanya mikutano mikubwa rasmi 240 na mikutano 865 ya kusimamishwa na wananchi njiani, hasa wananchi wa vijijini. Dkt. Magufuli amekuwa akitumia usafiri wa barabarani, ambapo hadi sasa ametembea kilomita 31,467 kwa barabara kuu, barabara za mikoa, barabara za wilaya, barabara za mlisho (feeder roads), na barabara za mijini na vijijini.

Watu wengi wamekuwa wanajitokeza kwenye mikutano yetu. Lakini la muhimu zaidi ni hamasa na matumaini wanayopata baada ya kumuona jukwaani na kumsikiliza Dkt. Magufuli. Wananchi wanapoondoka kwenye mikutano yetu ya kampeni wanakuwa wamepata fursa ya kumsikia mgombea wetu kwa kitambo kinachotosheleza, wamemuelewa, wameelewa sera za CCM na wameshawishika kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi.

Tunaingia katika ngwe ya mwisho ya kampeni zetu. Tangu kampeni zianze hadi sasa, ushindi wa CCM unajidhihirisha. Hata hivyo, katika kujihakikishia ushindi na kuongeza kiwango cha ushindi, katika ngwe hii ya mwisho, tumeanza kampeni nzito.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameanza ziara ya kampeni katika majimbo 64. Vilevile, viongozi wengine wa CCM, akiwemo Rais na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa, nao wataanza safari za kuzunguka nchi nzima kumuongezea kura Dkt. Magufuli na wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Tutatumia helikopta nne kwa ajili ya shughuli hii. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wataendelea kutumia usafiri wa gari hadi mwisho wa kampeni, isipokuwa pale tu itakapokuwa hakuna budi.

Maandalizi ya Kuleta Mabadiliko ya Haraka na ya Kweli

Pia, tunapenda kutoa taarifa kwamba, mgombea wetu, Dkt. John Pombe Magufuli, ameunda jopo la wanataaluma na wataalamu huru magwiji wazalendo wa uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, kwa ajili ya maandalizi ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini kuanzia siku ya kwanza atakayokuwa madarakani.

Dkt. Magufuli amelipa jopo hili majukumu yafuatayo:

1. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

2. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

3. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali;

4. Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa.

5. Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania;

6. Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.

7. Kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa.

8. Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.

9. Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika;

10. Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini.

Dkt. Magufuli ameazimia kuanza kazi mara moja kwa bidii kubwa na maarifa mapya.

Imetolewa na:-

January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
11 Oktoba 2015

Peleka kule kwenye special thread yenu ya magufuri au mmekosa watu mmeona muwe mnadania nyuzi za watu
 
Back
Top Bottom