Yaliyojiri Mkutano wa Edward Lowassa, Musoma mjini - Oktoba 11, 2015

Ocampo four

JF Senior Expert Member
Feb 28, 2014
5,790
2,159
Mgombea urais kupitia tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa ametikisa mji wa Musoma Mjini Leo kwa kufanya mkutano mkubwa wa historia katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo!

Tazama picha mbalimbali ya mkutano huo.

Hatareeeeee, sina maneno mengi, sema mwenyeweeeeee!!!

Lowassa: Wananchi anzeni kushangilia ushindi

Huku zikiwa zimebaki siku 13, Mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendelea na anayeungwa mkono na umoja wa Ukawa Ndg. Edward Lowassa kawataka wananchi waanze sasa kushangilia ushindi na ukombozi wa pili wa Taifa hili.

Lowassa kasema hayo jana alipokuwa mjini Musoma, ambapo alipata mapokezi ambayo hayajawahi kutokea, tokea nchi ipate uhuru. Lowassa kasema kutokana na mapokezi na hamasa kubwa ya vijana, wakina mama, na wazee anayopata, kawataka wananchi waanze kushangilia ukombozi wa pili unaotarajiwa kutokea oktoba 25.

Lowassa kasema baada ya oktoba 25, kila mwananchi ataanza kufaidika na matunda ya mgao wa keki ya Taifa, na sio hali ilivyo ya sasa, ambapo keki inamegwa na wachache na kuacha vijana wengi, bodaboda, machinga, wakina mama vijijini, walimu, madaktari, wafanyabiashara, wauguzi, wakulima na wafugaji wakiwa hawana hata uwakika wa kupata milo mitatu. Hilo linakoma mara moja baada ya oktoba 25..

"najua uhuzi, masikitiko na mfadhaiko mliyonayo wananchi. Mwisho wa hayo yote ni tarehe 25, ndio maana nataka muanze kusherekea kuanzia sasa kwani naenda kuwatoa kwenye kifungo cha kunyimwa fursa na serikali ya CCM kwa zaidi ya miaka 54"...

Vile vile kawataka wananchi kwa uwingi wao siku ya tarehe 25.10.2015 wajitokeze kwa wingi sana sana kupiga kura...

4.jpg 9.JPG
11224158_407108222815115_1303473295106911564_n.jpg
5.jpg 2.jpg 3.jpg 6.jpg 7.JPG 8.JPG 10.JPG
6.jpg

Siongei tena
 
Last edited by a moderator:
Wataalam wa IT Masaki chini ya January Magamba hebu toleeni ufafanuzi.

Hizi picha siyo za kutengeneza kweli?
 
Acheni zenu.. Mnataka mtu ambaye Ni fisadi apewe Nchi? Kamanda Wa Anga mbowe, Na wenzio mmetuaminisha miaka nenda rudi kuwa ENL Ni Fisadi, hafai kupewa nafasi ya kutuongoza iweje Leo mumkubali aingie madarakani? Tena kupitia Chama chetu tukufu?
 
Back
Top Bottom