Yaliyojiri Mahakama Kuu: Usikilizwaji wa UAMUZI wa pingamizi la Zitto dhidi ya CC ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,274
Wakuu tupo ndani ya viunga vya Mahaka kuu tayari kwakusikiliza uamuzi wa Pingamizi la Zitto (aliyekuwa mwanachama wa Chadema) dhidi ya cc ya Chadema.

Ulinzi leo unaimarishwa sana, magari ya polisi manne yakiwa na askari waliovalia kikazi wamejipanga kivitendo,

Makamanda wachadema wameshaanza kuwasili

Tutakuwa live kwa kila neno la Jaji Utamwa

UPDATES:

- Wakuu kuna kikundi cha vijana (kile cha juzi) kimeingia na gari suzuki cary no T 2652 ADG Kiongozi wa kikundi hiki nimemfahamu ni maarufu kwa jina la Gash. Wanaimba nyimbo za kumuunga mkono Zitto "Tunataka mtoto wetu Zitto x 2"

- Naaam wamechaguliwa watu maalumu wa kuingia mahakamani, hii ni kwasababu ya uwingi wa na kudhiti kundi la wahuni waliokusanywa na UVCCM na CUF kutoka vijiwe vya Kariakoo, Buguruni na Temeke,

- Polisi wameamua kuamuru kila anaeingia ndani lazima aandikishe jina, na na viongozi wa chadema wa matawi wanasimamia kuwatambua watu wao. Vijana wa Zitto wameambiwa wakae ng'ambo ya barabara kule kabisaaa. Kwa asubuhi hii nalipongeza jeshi la polisi kwa utaratibu linaouchukua,

- Kwa sasa tupo ndani ya ukumbi wa wazi wa mahakama,

- Nimearifiwa na kuwa uamuzi utaanza kusomwa saa nne

- Zitto amewasili, hehee kapitishwa mlango wa nyuma unaotumiwa na majaji hivyo kanusurika zomea,

- Bado tunaendelea kusubiri jaji afike na suala la uamuzi wa shauri hili uendelee,

- Naaam sasa tumeambiwa tuingie kwenye chumba cha hukumu

Hukumu imeahirishwa mpaka kesho saa nane mchana


===========

Nje ya mahakama nyimbo za ukombozi za makamanda,

Hahaa Zitto akifaa mimi siwezi kulia nitamtupa kagera kiwe chakula chakula cha mambaaa x2

Zitto bado yupo ndani ya Mahakama. Wafuasi wake ndio wanaondoka eneo ka mahakama.

Waandishi wa habari bado wametanda geti la mahakama.

Mbele ya mahakama karibu na Hyatty Hotel vijana wa Zitto wanaanza kurusha mawe, polisi wanasogea tayari kwakuwadhibiti,

Polisi wenye gari la maji washawasha sambamba na wenye mabomu wanajipanga kidhibiti hali hii,

UPDATES hizi zimewajia kwa hisani ya

Yericko Nyerere
---------------------
 
Watanzania tusitegemee kuna chama kitatukomboa kimaendeleo,ni sisi watu wa taifa hili bila kuwa na chama tutoke majumbani twende kudai haki zetu kwa watawala bila kusubiria kusemewe kila kitu na watu ambao wana maslahi yao.
Tuache uwoga!!
 
Hivi kwa tamko la Chadema la jana bado huyo kenge anang'ang'ana mahakamani!
 
Watanzania tusitegemee kuna chama kitatukomboa kimaendeleo,ni sisi watu wa taifa hili bila kuwa na chama tutoke majumbani twende kudai haki zetu kwa watawala bila kusubiria kusemewe kila kitu na watu ambao wana maslahi yao.
Tuache uwoga!!


Yani uoga ndiyo itatugharimu sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom