Yaliyojiri: Lowassa kuchukua fomu ya Urais Makao Makuu ya CHADEMA

mkuu pole sana najua inauma lakn hao ndio Chadema wazee wa dili za mjini..

Hawaangalii maslahi ya chama wao wanaangalia maslahi yao.
Hicho ni chama cha mtu na sio chama cha watu. Mtei ndio last say...
Namwona magufuli anaingia magogon kiulaiiini. Chadema ni chama cha ukomboz lakn badoo hakijakomaa kupewa nchi kwasababu hawajitambui

Mbona CHADEMA wenyewe hawalalamiki?

Naona nyie mnalia kuliko wafiwa.
 
karibu sana na sisi sasa tutamtembeza nchi nzima kumtambulisha kama walivyo fanya kwa magufuli tuone nani na nani kwikwikwikwikwikwi.............................
teh,teh,teh,hivyo hivyo mkuu sharti na sisi tuzunguke nae daa!!mwiba wa kujitakia unawachoma,leo ati wanasema ana uroho wa madaraka haahaaaaa.
 
Tukundane dr slaa yupo imara ndani ya chadema..propaganda za wapinzani wetu ndo zinafanya watu wenye moyo mwepesi kama kware wahangaike ....wao huko dodoma walipata mgombea wao kwa nguvu ya jeshi..kwa mara ya kwanza jeshi lilitanda na kupiga watu mabomu na kumwagia maji ya kuwasha...ndani ya vikao kuliparaganyika...wanapoona chadema wanatumia utaratibu madhubuti wanaanza kuweweseka na kupandikza chuki...
kwa kuwa dr slaa hagombei yeye kama katibu mkuu anakuw ana kazi kubwa ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa....hakuna haja ya kutia hofu....la mwisho kama uko nje ya ukawa basi tafuta chama ndani ya ukawa ujiunge nacho..

safari hii kabla ya sadaka ukawa watakuwa ikulu...namaanisha hivi siku ya uchaguzi wale watakaoanzia kanisani asubuhi kabla hawajatoa sadaka ukawa watakuwa wameshafika ikulu....

Tatizo wanachadema wengi ni kama misukule. Hawahoji wala hawafikiri, wao wanajua poweeeeeeeeer..........!!
 
Last edited by a moderator:
Hana lolote kanunua ugombe kwa 10bl chezea Mbowe wewe yuko kibiashara zaidi na manywele washauri wake wanataka hizo pesa zake za kifisadi tu

Nimemtafuta Mnyika na Slaa sijawanona!The real intellectualls whom I still believe they cant mix with these thieves
 
Vijana wengi mnatoka povu, Lowassa hajakwenda CDM kuvaa gwanda au kwamba ameona mvuto ndani ya CDM. Lowassa amekwenda CDM kuwakimbiza CCM mchakamchaka. Mnaotaka sijui avae gwanda, sijui aseme wazimu wazimu, mtasubiri sana. Lowassa is a political genius, he knows how to win. That is only matter, is how you win. Mboe anajua what matters is trophy, not kelekele.
 
unnamed-52.jpg
WAZIRI Mkuu wa zamani Edward Lowassa, amechukua fomu kupeperusha bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimpitishe kugombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Katika Makao Makuu ya chama chake hicho kipya leo Edward Lowassa alipokewa na maelfu ya watu waliovalia sare za chama huku wakiimba wana imani naye.
Edward Lowassa aliwasili makao makuu mchana moja kwa moja akaenda ofisi za Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa.
Huku akisindikizwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Mwanasheria wa chama Tundu Lissu na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Edward Lowassa aliingia katika ofisi hizo katika jukwaa maalumu la kupokea fomu.
Lissu ndiye alikuwa mzungumzaji wa kwanza kwa kuwahakikishia wanachama hawakubahatisha kumpokea Lowassa kwa sababu walifanya utafiti wa kina.
"Kamati Kuu imejiridhisha kwa kushirikiana na viongozi wote wa juu akiwemo Katibu Mkuu na manaibu wake wote wawili, Mwenyekiti na makamu wote wawili, wajumbe wa Kamati Kuu na Mkutano Mkuu, kuwa Edward Lowassa ndiye kiongozi tunayemtaka hivyo Jumapili iliyopita tuliitisha Kamati Kuu ya dharura kumpitisha," alisema Lissu.
Baada ya kukabidhiwa fomu aliyolipiwa na wanachama waliochangishana fedha hadi kufikia Sh milioni moja, Edward Lowassa alisimama kuwasalimia waliohudhuria kwa kuwaahidi kufanya kazi kwa juhudi ili kuiondoa Tanzania katika hali mbaya ya kiuchumi.
"Nashukuru kwa kunipa heshima kubwa namna hii, sina maneno ya kuwashukuru zaidi ya kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili iwe malipo ya mlichonifanyia.
"Shukurani yangu itakuja baada ya kushinda uchaguzi, lakini ushindi hauji bila umoja. Chadema inaweza kuleta mabadiliko kupitia ukawa.
Baada ya kumaliza kuzungumza alisimama Mbowe kutoa neno la shukurani kwa Edward Lowassa kwa kusema Chadema kitaendelea kuwa chama makini kinachosimamia maamuzi yake.
Vilevile alizungumzia ratiba ya vikao vya kujadili fomu ya mgombea ambaye mpaka sasa ni Edward Lowassa pekee, "Vikao vitaanza Agosti mbili kujadili namna tutakavyoingia katika uchaguzi mkuu.
"Baraza Kuu litaketi Agosti tatu kujadili fomu ya mgombea na kujadili ilani ya uchaguzi, Mkutano Mkuu utafanyika Agosti nne kupitisha jina la mgombea na mgombea mwenza.
"Vikao vya kamati Kuu vitaendelea tarehe tano, sita hadi saba kuidhinisha wagombea wa ubunge kwa kushirikiana na Ukawa. Kazi ya kujadili wagombea si ndogo nawaomba waandishi wa habari muwe wavumilivu msipige ramli," alisema Mbowe.
Baada ya kumalizika hafla hiyo Edward Lowassa alitoka nje kwa ajili ya picha ya pamoja kuwaonyesha wanachama fomu yake.
 
Ha ha ha..........demokrasia imebakwa live. We umewahi kuona mtu unaenda kuchukua form unasindikizwa na viongozi wa chama!! Hapo ni ndio afande,ukamanda na demokrasia wapi na wapi.
we kilaza sana! Kwani kuwa kiongozi ndo usimuunge MTU mkono! K
 
lowasa ameonesha ubinafsi sana,wana akili ndogo wale waliokua wanamkashifu kuwa ni fisadi wakati akiwa waziri mkuu lakini leo hii wanampokea kwa mikono miwili......... ni mtazamo tu


Acha umbea umeshaachika mara ngapi?
Kuing'oa CCM is first priority.
Mtaugua kiharusi mwaka huu.
 
Ushuri tu kwa wana ndoa usiache mke kwa maneno ya kusikia tu unamwacha mke halafu kesho unasikia kachukuliwa na wale wale waliomwita mkeo mhuni,halafu unawafuata unawauliza kwa nini wamemchukua inahusu???wee si ulimwachaa tena kwa fitna kubwa leo unamlilia hahaaaaaaa............
 
Tundu lisu nimemuona viongozi wakuu karibia wote wa UKAWA walihojiwa wakaeleza ni kwanini wamekubali kumpitisha Lowassa kuwa mgombea wao isipokuwa Dr slaa peke yake ndiye hajahojiwa na kutoa ya moyoni mwake,jamani tuambizane ukweli Dr slaa yuko wapi?.

Juzi maccm waliitisha mkutano na waandishi wa habari lakini wakaairisha mkutano wao katika mazingira ya utata baada ya kupiga blabla ambazo hata wandishi wenyewe walishitukia.

Nimeanza kupata wasiwasi kwa nini CCM walitaka kuongea na wandishi wa habari siku moja tu baada ya CHADEMA kuitisha mkutano na wandishi wa habari na kumtambulisha Lowassa ambaye alikuwa ni mwanachama wa CCM kuwa amehama CCM na kujiunga CHADEMA?isije ikawa CCM walikuwa wanataka kuijibu CHADEMA kuwa si mnajifanya wajanja mumemchukua mwanachama wetu na sisi tayari tumemnasa mwanachama wenu kwa hiyo ngoma imekuwa droo.

Halafu baada ya muda mfupi mkutano ukaahirishwa pasipo kutoa hata sababu za maana zilizowafanya waahirishe mkutano katika mazingira yale,kwa mazingira haya inaonekana CCM walikuwa na jambo maalumu la kulisema na wakalazimika kuahirisha mkutano wao kutokana na mambo kwenda kinyume na jinsi walivyokuwa wamepanga.lakini mwisho wake tutakijua kilichofichwa nyuma ya pazia.

Angalau umeweza unganisha dot.Wadau hawajui mambo yanayoendelea kwenye kiza.Mpaka jumamos kila kitu kitakua wazi tusubiri upepo ufanye kazi ili nyeti za kuku zionekane
 

Edwald Lowasa Waziri mkuu wa Zamani aliyejiunga na Chama cha CHADEMA hivi karibuni akiwasili katika makao makuu ya ofisi za CHADEMA tayari kwa kuchukua fomu za kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia chama hichi leo jijini Dar es salaam.
Edwald Lowasa Waziri mkuu wa Zamani aliyejiunga na Chama cha CHADEMA hivi karibuni akiwapungia mkikono wananchi kwenye makao makuu ya CHADEMA.
Edwald Lowasa Waziri mkuu wa Zamani aliyejiunga na Chama cha CHADEMA hivi karibuni akiingia katika ofisi za makao makuu ya chama hicho kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho.
 
we kilaza sana! Kwani kuwa kiongozi ndo usimuunge MTU mkono! K

We ndio kilaza ila nasikitika hujajitambua bado. Kumbuka hapo ndio kwanza anachukua form,then ijadiliwe kama anafaa au hafai. Tatizo nyie mmempitisha kwanza kabla ya hata hajachukua form kwa sababu ya bn 10.
 
_MG_1457.jpg


_MG_1497.jpg
IMG-20150730-WA0076.jpg

IMG-20150730-WA0078.jpg
IMG-20150730-WA0084.jpg
Lowassa akiwasili makao makuu ya Chadema hii leo ikiwa ni siku chache baada ya kujiunga na chama hicho.
IMG-20150730-WA0085.jpg
Lowassa akisalimiana na wanachama wa Chadema.
IMG-20150730-WA0088.jpg
Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chadema.
IMG-20150730-WA0083.jpg
Lowassa na ujumbe wake wakiwa katika ofisi ya Mwenyekiti kuchukua fomu.
IMG-20150730-WA0080.jpg
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa leo amechukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Lowassa amechukua fomu hio Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mamia ya wanachama wa Chadema na viongozi wa juu wa Chama hicho.
DSC_6838.jpg
WAZIRI Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, (kulia), akionyesha mkoba wenye fomu za kuomba kuwania urais kupitia CHADEMA, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mh. Freeman Mbowe, kwenye makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2015. Mh Lowassa, alijiunga hivi karibuni na chama hicho, baada ya kujitoa CCM.
IMG-20150730-WA0082.jpg
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza jambo baada ya kumkabidhi fomu Edward Lowassa kugombea Urais.
IMG-20150730-WA0081.jpg
Edward Lowassa akizungumza jambo.
IMG-20150730-WA0077.jpg
Lowassa na Tundu Lissu wakifurahia jambo
IMG-20150730-WA0089.jpg
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza jambo na Edward Lowassa.
IMG-20150730-WA0087.jpg
Naibu Katibu Mkuu, Salum Mwalimu akiteta jambo na Edward Lowassa
 
Back
Top Bottom