Yaliyojiri: Kongamano la amani ya Tanzania - Julai 28, 2013

Hitimisho la mada ya Prof Bernadeta akichangia mjadala huo, kwa hisani ya mdau mmoja wa facebook

Kukiwa na jitihada za makusudi kuleta amani, amani itakuwepo.. Kukiwa na jitihada za kuweka umoja na usawa katika jamii.. itawezekana!

Mfano.. Nyerere alibuni utaratibu wa kuwachanganya watanzania wa maeneo tofauti kwa kusoma ama kufanya kazi.. matunda yake ni amani na maelewanao wakati wa utawala wa mwalimu..

Bunge limekuwa uwanja wa mapambano kati ya watawala na wapinzani ana kuibua mifarakano inayofanya nchi ionekane haina utulivu

Taasisi za kidini zinapaswa kuungwa mkono katika jitihada za kulea jamii inayolinda amani

Kuwe na taasisi maalumu ya kushughulikia migogoro. Jeshi la Polisi haliwezi kutatua mgogoro yote ikiwemo ya kidini.. Kukiwa na Tume maalumu kama walivyofanya South Afrika kutatua migogoro kutasaidia. Kutumia mjeshi ndio

Leo hii Viongozi wa kisiasa kukamatwa na Polisi sio breaking News tena.. imekuwa kama utamaduni.. kumekuwepo na dhana ya kubambikiwa kesi ambayo inapata mashiko kwa vile tunaona viongozi wa kisiasa wanakamatwa na kuachiwa tu..

Wananchi wanazoea mabomu na risasi..

Ni nani wadau wa amani... Ni nani alirusha bomu mkutano wa Chadema na kanisani.. bado hatujaweza kujua kiini cha tatizo.

mgogoro ukitokea, tunaanza kuuliza wametumwa na nani?? badala ya kutafuta kiini cha tatizo

Rushwa pia ni chanzo kingine cha uvunjifu wa amani...

Viongozi wa kisiasa wameshika kasi kwenye ssiasa za uchaguzi, za vyeo na madaraka ambayo hawatayafaidi kama amani hakuna.

CCM wamekuwa akishindwa kuzuia mifarakano ya kuwania uraia ndani ya chama na mwishowe kuwaachia mzigo wote Jeshi la Polisi kutatua migogoro..

Chadema wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kujihami na jeshi la polisi, na na kushughulikia kesi.. Kama chama kikuu cha upinzani kinapaswa sasa kutoa mapendekezo ya kuleta amani.

Iko haja ya kuwa na kampeni endelevu ya kujadili amani kupitia wadau mbali mabali.. iwe kama kampeni endelevu ya kujenga utamaduni wa amani..

Mahusiano yetu na nchi jirani pia yanaweza kuwa chanzo cha tatizo.. Mfano Rwanda, Malawi.. ukitupiga tunakupiga!

Mchakato wa Katiba unatupa nafasi ya kuweka utaratibu na taasisi za kuweka amani

HAKUNA NJIA YA KULETA AMANI ISIPOKUWA AMANI YENYEWE!

Amamaliza Prof Bernadetha Kilian
 
you are very poor in understanding the prayer as a concept theoretically and practically
Acha ukauzu, nchi za kikomonst kama Zamani USSR, CUBA na kazalika hakukuwa na dini lakini kuliikuwa na amani, Nyie ndo mnao haribu mazingila kwa kukata mit na mvua isipo nyesha mnaanza maombi
 
Kwanza, Chadema hawakuspecify.

Walisema "amani haijadiliwi", "amani inawekwa"

Period

Mwezi haujatimia Katibu Mkuu wa Chadema anaenda kujadili amani

Hivi pale mkisema huwa hamjui mnachokisema, au ndio kujisemea lolote tu alimradi litakaloungwa mkono na watu kwa wakati ule?

Natumaini hutumii ubongo wa punda kufikiri kufikri!!
 
kosa lako ni kuwaza kwa mafungu, nani aliyekwambia maombi yanafanyika msikitini au kanisani tu? Nani kakwambia maombi yanafanywa na mchungaji au shekhe tu? kama hufahamu jambo wewe soma tu husichangie mapovu
Acha uwongo.Amani tangu lini ikaombewa kanisani au msikitini?
 
mantiki ya huu mjadala ni nini? nini hasa tutakipata kama nchi kutoka katika huu mjadala au ni business as usual

Amani na Mustakabali wa Taifa letu...kama huoni mantiki hapa Ni vigumu sana kuijenga Mimi kama Mimi...
 
Dah! watanzania naona ni shughuli kujenga hoja, yaani mtu haeleweki anataka kuchangia lipi. matunda ya mfumo wetu wa elimu!
 
hivi wewe unategemea jawabu gani kutoka kwenye hili kongamano???
Ni haki yangu kutoa mawazo yangu popote pale kama mtoa mada anaonyesha wazi kuona upande mmoja huko siko kujenga na kwa mtindo huu kongamano hili halitatoa jawabu.
 
Hivyo unapingana na Dr Slaa?, maana alisema amani haiombewi na alikejeli mpaka wachungaji na maaskofu kuwa waache unafiki kwa kujifanya wanaombea amani.

Wanaompinga Mungu wapo wengi tu, Kama na yeye alisema Basi amekosea. Ni upumbavu kutotambua nafasi ya Mungu katika AMANI. Kwa kawaida mambo ya kiroho husimamia ya kimwili "The Spiritual controls the physical"
 
Huyu Nassoro kachangia kwa akili bila kuegemea ila amepoteza baadhi ya pointi
 
Back
Top Bottom