Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na rushwa. Shauri kuendelea kesho Nov, 2, 2021

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,829
Kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake itaendelea leo katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, ambapo upande wa mashitaka utaleta shahidi mwingine.

Fuatilia hapa kujua kitakachojiri katika mchakato mzima wa kesi hiyo kwa siku ya leo 11/01/2021

==========

Watuhumiwa wote wamekwishawasili katika ukumbi wa mahakama tayari kuanza kwa kesi.

Jaji: Ameingia sasa

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 inatajwa

Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe na wenzake

Wakili wa Serikali, Robert Kidando anatambulisha Jopo lake
1. Pius Hilla
2. Abdallah Chavula,
3. Jenitreza Kitali,
4. Nasorro Katuga,
5. Esther Martin,
6. Ignasi Mwinuka
7. Tulimanywa Majige

Wakili Peter Kibatala anawatambulisha Mawakili Wa Utetezi
1.Jeremiah Mtobesya
2.Michael Mwangasa
3.Seleman Matauka
4.Nashon Nkungu
5.Alex Massaba
6.Michael Lugina
7.Maria Mushi
8.Hadija Aron
9.Dickson Matata
10.Jonathan Mndeme
11.Fredrick Kihwelo
12.John Malya

Jaji: anawait Washitakiwa 1,2,3 na 4 Wanasimama Kuitikia

Wakili wa Serikali: Kwa Upande wetu tuna shahidi Mmoja kwa Leo na tupo tayari Kuendelea Kwa Upande wetu tupo tayari kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Tupo tayari na sisi Kuendelea

Wakili wa Serikali: Mmoja anatoka Kwenda Kumuita Shahidi Nje ya Chumba Cha Mahakama Mahakama Ipo Kimya Kidogo

Shahidi anapita ni Mdada Kajitanda Buibui na Kavaa Barakoa Kubwa sana Kumziba Sura,

Jaji: Majina Yako

Shahidi: Anita Varelian Mtali

Jaji: umri Shahidi: 45yrs

Jaji: Kabila

Shahidi: Mchaga

Jaji: Shughuli Zako

Shahidi: Nafanya Biashara

Jaji: Dini yako

Shahidi: R. C

Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii Kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa ni kweli, kweli tupu Eeeh Mungu nisaidie

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Shahidi Ataongozwa na Wakili Esther Martin

Wakili wa Serikali: Esther Ikumbushe Mahakama Majina yako

Shahidi: Anita Varelian Mtali

Wakili wa Serikali: Unaishi Wapi

Shahidi: Moshi, RAU madukani.

Jaji: Jina lako la Tatu sijalipata Vizuri ni Mtali.?

Shahidi: Mtaro

Wakili wa Serikali: Umeishi kwa Muda gani Rau

Shahidi: Miaka 08

Wakili wa Serikali: Unafanya Shughuli gani

Shahidi: Nafanya Biashara ya Kuuza Mbege

Wakili wa Serikali: Ulianza lini Biashara yako ya Mbege

Shahidi: Miaka 08 ninayo

Wakili wa Serikali: Mbali na Biashara yako ya Mbege una bishara gani Nyingine

Shahidi: Kuna Glocery, Stationary, Banda la Tigo Pesa na Kuna Sehemu ya Kutolea Movie

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama 05 Mwezi 08 2020 ulikuwa wapi

Shahidi: Sehemu yangu ya Biashara, Nikifanya Usafi

Wakili wa Serikali: Saa ngapi

Shahidi: Saa Saba Kasoro

Wakili wa Serikali: Ya Muda gani

Shahidi: Ya Mchana

Wakili wa Serikali : Kabla ya Kufika eneo lako la Biashara ulikuwa umetoka wapi?

Shahidi: Nilikuwa Nimetoka Nyumbani Nikaenda Saloon Kuosha Nywele

Wakili wa Serikali: Na Ulipotoka Saloon kuelekea sehemu yako Kufanya Usafi

Shahidi: Nilikuta Wakaka Watatu walikuwa wamekaa Mbele Yangu walikuwa wanakunywa na Kusajili Laini

Wakili wa Serikali: Walikuwa wanakunywa nini

Shahidi: Walikuwa wanakunywa Bia

Wakili wa Serikali: Hizo laini walikuwa wanasajili wapi

Shahidi: Kuna Vijana wanapitaga Mitaani Kusajili Laini

Wakili wa Serikali: Ukiwa unafanya Usafi kitu gani Kingine ulishuhudia

Shahidi: Kuna wakaka wawili walikuwa wanapitapita wakiongea na simu, Wanaenda wanarudi wakiongea na Simu

Wakili wa Serikali: Hao wanaopita ni tofauti na wale uliposema walikuwa wanakunywa Bia

Shahidi: Hapana ni walewale

Wakili wa Serikali: Kutoka Kwako Unapofanyia Kazi Mpaka Glocery ni Umbali gani

Shahidi: Kama Hatua 10

Wakili wa Serikali: Hapo Katikati sasa, Kati ya Glocery na ulipo, pana kitu gani

Shahidi: Pana uwazi

Wakili wa Serikali: Baada ya Muda kitu gani kilitokea

Shahidi: Wakati wanaongea na Simu Walitokea watu wawili wakaongea kwa sauti kali "Mpo chini ya Ulinzi Mnahusika na Mambo ya Kigaidi, chuchumaa Chini Mikono Juu"

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine ulisikia

Shahidi: Chuchumaa Chini Mnahusika na Mambo ya Kigaidi Wakili wa Serikali: Ni watu gani sasa hao

Shahidi: Ni Askari

Wakili wa Serikali: Ulikuwa unafanya nini wakati huo

Shahidi: Nafanya Usafi

Wakili wa Serikali: Pana umbali gani kutoka Walipo na Mpaka Ulipokuwa unafanya Usafi

Shahidi: Hatua 05

Wakili wa Serikali: Ulisikia nini Kingine

Shahidi: Sikusikia Kingine zaidi ya Chuchumaa Chini Nyoosha Mikono Juu

Wakili wa Serikali: Walikuwa Askari wangapi

Shahidi: Wawili

Wakili wa Serikali: Hali ya Pale ilikuwaje

Shahidi: Ilikuwa ni Utulivu

Wakili wa Serikali: Nini Kilifuata

Shahidi: Walitokea Askari Wengine watatu wakawa wamefika eneo la Tukio

Wakili wa Serikali: Ongeza Sauti

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kiliendelea

Shahidi: Baada ya Kuwa Askari watano alitokea Mmoja akaniambia anaomba nisogee anahitaji Kuwafanyia Upekuzi

Wakili wa Serikali: Ni Askari gani huyo

Shahidi: Alinitambulisha anaitwa Askari Polisi Jumanne

Wakili wa Serikali: Ulifanya nini kujiridhisha?

Shahidi: Alitoa Kitambulisho Akanionyesha

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo nini kilifanyika

Shahidi: Alimsimamisha Mmoja

Wakili wa Serikali: Kabla ya Kumsimamisha..?

Shahidi: Afande Jumanne alijipekua kuanzia Kifuani akatoa Mifuko Nje

Wakili wa Serikali: We ulikuwa na nani wakati huo

Shahidi: Dada Mmoja anaitwa Esther

Wakili wa Serikali: Kutoka Eneo la walioambiwa Wachuchumae Chini, palikuwa na Umbali gani?

Shahidi: Kama Hatua Mbili

Wakili wa Serikali: Kuna Kitu gani Kingine

Shahidi: Raia walikuwa wamekuja

Wakili wa Serikali: Kabla ya Raia Kusogea eneo hilo palikuwa na hali gani?

Shahidi: Palikuwa na Jua

Wakili wa Serikali: ahaa ahaaa yani hali ya pale ilikuwaje?

Shahidi: Palikuwa pametulia

Wakili wa Serikali: Ikaendelea nini?

Shahidi: Alimsimamisha Mmoja akamuuliza Unaitwa nani?

Wakili wa Serikali: Akajibu anaitwa nani?

Shahidi: Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: Akamwambia nini?

Shahidi: Akiwa amenyoosha Mikono Juu akamwambia Geuka, akageuka

Wakili wa Serikali: Baada ya Kugeuka

Shahidi: Askari Jumanne alianza Kumpekua Kuanzia Kichwani, Mabegani, Alipofika Kiunoni alikuta Kitu kigumu

Wakili wa Serikali: Alikikuta Upande gani

Shahidi: Kushoto

Wakili wa Serikali: Maeneo Gani?

Shahidi: Niliona ni Bastola

Wakili wa Serikali: Ulijuaje kama ni Bastola?

Shahidi: Afande Jummane alituambia ni Bastola

Wakili wa Serikali: Halafu

Shahidi: akatuonyesha namba

Wakili wa Serikali: Zilikuwa ni namba gani.?

Shahidi: A5340

Wakili wa Serikali: Zilikuwa kwenye nini

Shahidi: Kwenye Bastola

Wakili wa Serikali: Wakati anakuonyesha Bastola Adam alikuwa wapi?

Shahidi: Alikuwa amesimama

Wakili wa Serikali: Ukiona na nini Kingine

Shahidi: Risasi 03

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea

Shahidi: Akaendelea na Upekuzi

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea

Shahidi: Akaendelea na Upekuzi, alipofika Upande wa Kulia akakuta Vitu vidogo vidogo Kwenye Karatasi ya Nailon akasema inasadikiwa ni Madawa ya Kulevya ila itajulikana Mbele.

Wakili wa Serikali: Zilikuwa ngapi Shahidi: 58

Wakili wa Serikali: ikawaje

Shahidi: Aliendelea Kumpekua akamkuta na Simu Ndogo aina ya Itel

Wakili wa Serikali: Hiyo simu akaifanyaje

Shahidi: Akatoa laini akakuta namba akaziandika

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo aliendelea na nini

Shahidi: Akamwambia Naomba fomu, .......akaleta fomu

Wakili wa Serikali: fomu ngapi

Shahidi: Zilikuwa Mbili

Wakili wa Serikali: Akafanya nini sasa Kwenye ile Fomu

Shahidi: Kaandika Vitu alivyokuwa amempekua

Wakili wa Serikali: Umesema palikuwa na fomu Mbili, fomu ya kwanza akijaza nini

Shahidi: fomu ya kwanza alijaza Bastola, Risasi na Laini

Wakili wa Serikali: Zilikuwa ni laini gani

Shahidi: Laini ya Voda na Airtel

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumalizia fomu ya kwanza

Shahidi: alichukua fomu Nyingine

Wakili wa Serikali: Kabla ya Kujaza Fomu Nyingine

Shahidi: Alipomaliza Kujaza akampa akasaini na Baadae akasaini yeye alipo maliza Kusaini.

Wakili wa Serikali: alimpa nani

Shahidi: Alimpa Adam

Wakili wa Serikali: baada ya fomu ya kwanza nini kiliendelea

Shahidi: alichukua Fomu Nyingine

Wakili wa Serikali: alijaza nini

Shahidi: alijaza vile Vikete vidogo Vidogo

Wakili wa Serikali: Vingapi Vilikuwa Vingapi

Shahidi: Vilikuwa 58

Wakili wa Serikali: baada ya hapo

Shahidi: akampa Adam asome alafu asaini na sisi akamtupa tusaini

Wakili wa Serikali: Wewe na nani..?

Shahidi: Mimi na Dada Esther

Wakili wa Serikali: baada Kumalizia nini kilifuata

Shahidi: akamuita Mwingine

Wakili wa Serikali: huyo Mwingine anaitwa nani

Shahidi: Mohamed Abdulahi Ling'wenya

Wakili wa Serikali: akamwambia nini

Shahidi: asimame ageuke, Baada ya kugeuka akaanza Kumpekua

Wakili wa Serikali: alianzaje Kumpekua

Shahidi: Kichwani Mikononi

Wakili wa Serikali: ilikuwaje

Shahidi: Upande wa Kulia alikuta na Vikete Vidogo Vidogo

Wakili wa Serikali: Vilikuwa Vingapi

Shahidi: 25

Wakili wa Serikali: akafanyeje

Shahidi: akavishika Akaendelea Kumpekua

Shahidi: akavishika Akaendelea Kumpekua

Shahidi: alikuta Simu aina ya Tecno

Wakili wa Serikali: Rangi gani

Shahidi: Nyeusi

Wakili wa Serikali: akafanya nini

Shahidi: akapekua akakuta kuna laini

Wakili wa Serikali: laini gani

Shahidi: Hallotel

Wakili wa Serikali: baada ya Kupata simu akafanyeje

Shahidi: akazitoa zile Laini, Akampa yule Mwingine akazishika

Wakili wa Serikali: Na Yeye Akaendelea na nini

Shahidi: Akaendelea na Upekuzi

Wakili wa Serikali: hizo laini alikuwa anafanya nazo nini?

Shahidi: Alimpa Askari wa Pembeni akazishika

Wakili wa Serikali: Baada ya Upekuzi

Shahidi: Aliendelea na Upekuzi lakini hakukuta kitu Kingine

Wakili wa Serikali: Baada ya Upekuzi

Shahidi: aliomba fomu Mbili


Wakili wa Serikali: fomu ya Kwanza alijaza nini

Shahidi: alijaza vile Vikete Vidogo Vidogo

Wakili wa Serikali: Vilikuwa Vingapi

Shahidi: 25

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo

Shahidi: Alimpa akasema akasaini

Wakili wa Serikali: Nani Yeye, afande Jumanne?

Shahidi: Ndiyo na Baadae Mohamed

Wakili wa Serikali: na baadae

Shahidi: tukasaini sisi

Wakili wa Serikali: Wewe na nani

Shahidi: Mimi na Dada Esther

Wakili wa Serikali: baada ya hapo

Shahidi: Ile fomu Nyingine akajaza Simu na laini Nyingine

Wakili wa Serikali: Za Mtandao gani

Shahidi: Airtel na Hallotel

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo

Shahidi: Alimpa Mohamed asome kisha akasaini

Wakili wa Serikali: baada ya hapo

Shahidi: afande Jumanne alituomba na sisi tusome Kisha tusaini

Wakili wa Serikali: Wewe na nani

Shahidi: Mimi na Dada Esther

Wakili wa Serikali: baada ya Upekuzi

Shahidi: walivalishwa Pingu

Wakili wa Serikali: baada ya hapo

Shahidi: afande Jumanne akatuomba tuelekee Kituoni

Wakili wa Serikali: Hao walivalishwa Pingu walikuwa ni akina nani

Shahidi: Adam na Mohamed

Wakili wa Serikali: baada ya kuvalishwa Pingu..?

Shahidi: Wakaelekea kwenye Magari, Barabarani

Wakili wa Serikali: Palikuwa na Askari wangapi

Shahidi: Watano

Wakili wa Serikali: Walikuwa wamebeba nini

Shahidi: Wawili walikuwa wamebeba Bunduki

Wakili wa Serikali: Hali ya hewa eneo lile ilikuwaje

Shahidi: ilikuwa imetulia

Wakili wa Serikali: Hali ya hewa ilikuwaje

Shahidi: Kulikuwa na Jua na Mwanga

Wakili wa Serikali: Mlichukua Muda gani kwenye lile eneo Mpaka Mnamaliza Zoezi

Shahidi: Kama Dakika 45

Wakili wa Serikali: Baada ya Kufanya Upekuzi Kuna Vitu Vilipatikana na Kwamba Kuna fomu zilijazwa Sasa fomu ukiziona hapa utaweza Kuzitambua?

Wakili wa Serikali: sasa bada ya Kumalizia Mkaelekea kituoni, kituo gani..?

Shahidi: Central Moshi

Wakili wa Serikali: baada ya Kufika police central

Shahidi: Tuliandika Maelezo

Wakili wa Serikali: Maelezo ya nini

Shahidi: Kitu gani Kilichofanyika ......

Wakili wa Serikali: Tukianza na fomu ya Adam utaitambuaje

Shahidi: Kwa vitu vilivyoaandikwa, Jina langu na sahihi yangu

Wakili wa Serikali: Kulikuwa na nini Kingine Bastola

Wakili wa Serikali: Kingine

shahidi: Palikuwa na Risasi

Wakili wa Serikali namba gani Shahidi: A5340

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba nimpe fomu aweze Kuitambua

Wakili wa Serikali: Shika hii Karatasi iangalie kwa Makini

Shahidi: Ndiyo yenyewe

Wakili wa Serikali: Yenyewe nini

Shahidi: Fomu niliyo saini

Wakili wa Serikali: Umeitambuaje

Shahidi: Kwa Jina langu na Sehemu niliyosaini

Wakili wa Serikali: Jina lipo wapi, Ni Jina gani

Wakili Peter Kibatala: ALICHOKIFANYA DADA YANGU ESTHER HAIRUHUSIWI, ANAKWEMDA KWENYE DETAILS

Wakili wa Serikali: Sawa naondoa hilo swali

Wakili wa Serikali: Ungependa hii fomu ipokelewe Mahakamani

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaomba Fomu ipokelewe

Jaji: Wakili wa Mshtakiwa wa kwanza

MTOBESYA: HATUNA PINGAMIZI

Mallya: Hatuna Pingamizi Fredrik

Kiwhero: kwa Niaba ya Mshitakiwa.....wa tatu hatunapingamizi

Peter Kibatala: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne hatuna Pingamizi

Jaji: anaandika Kidogo

Jaji: Mahakama inaipokea kwa ID 1

Wakili wa Serikali: Shahidi pia ulisema kwenye huo Upekuzi pana Bastola na Risasi unaweza hapa Mahakamani ukavitambua Tuanze na Bastola

Shahidi: Ndiyo nitavitambua

Wakili wa Serikali: Bastola unazitambuaje

Shahidi: Kwa Namba A5340

Wakili wa Serikali: na Kwa Upande wa Risasi

Shahidi: namtambua, zilikuwa na Rangi ya Dhahabu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Naona Exibit nimuonyeshe Shahidi

Afisa Wa Mahakama anafungua Bahasha ya Kaki Anamkabidhi Wakili wa Serikali

Wakili wa Serikali:
Hebu Kiangalie hiki kitu hapa, Iambie Mahakama ni nini

Shahidi: anaingilia bila Kushika, ni Bastola

Wakili wa Serikali: ambayo Imetoka wapi

Shahidi: Imetoka Kwa Adam

Wakili wa Serikali: Uliona wapi?

Shahidi: iliyotoka kwa Adam

Wakili wa Serikali: ni Kitu gani Kilichokufanya ukagundua

Shahidi: kwa namba

Wakili wa Serikali: Namba gani

Shahidi: A5340

Wakili wa Serikali: Umeeleza pia ulishuhudia Upekuzi wa watu wa wili ambao kwa Majina yao ni Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya, Je ukiwaona unaweza Kuwatambua

Shahidi: naweza Kuwatambua

WAKILI WA SERIKALI: WAPO HAPA MAHAKAMANI?

Shahidi: Wapo hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali: Wapo wapi

Shahidi: hapa Mbele, Mohammed amevaa Tshirt ya Amevaa Meupe Kijani na Nyeusi

Wakili wa Serikali: na Adam yupo wapi Shahidi: amevaa Shati lenye Rangi Nyeupe Nyeupe

Wakili wa Serikali: Yupo wapi hapa Mahakamani

Shahidi: Yupo pale

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu

Jaji: Upande wa Utetezi

Mtobesya:
Ndiyo Mheshimiwa Jaji

Mtobesya: naomba Nipatiwe ID 1 Mahakama Inampatia

Mtobesya: Shahidi umeomba Mahakama Ipokee Kielelezo hiki Onyesha Sehemu ipo saini

Shahidi: Nimesaini hapa

Mtobesy: Kwa Ushahidi wako Unasema ulisaini Nyaraka ngapi

Shahidi: Nne

Mtobesya: Ushahidi wako kwamba Sahihi zako Lote zinafanana

Mtobesya: Naomba kwa Kifungu 75(1) Sheria ya Ushahidi, Shahidi asaini tena sehemu Nyingine ili Mahakama iweze Kufananisha Saini zake

Jaji: Unaweza Kutusomea.? Mtobesya: anasoma Kifungu cha 75(1) cha Sheria ya Ushahidi

Jaji: hicho Kifungu kinaitaka Mahakama shahidi asaini ili iweze Kufanya ufafananisho

Mtobesya: Ndiyo ili Mahakama iweze kufananisha, kwa sababu tuna Nyaraka Nyingine inasaini yake tofauti

JAJI: lakini hiyo Nyaraka itakuwa imetengenezwa hapa, Utakuwa umeiiingiza Mhakama .....

Jaji : Bwana Matata una jambo la Ku-she na sisi

Matata: Sheria Anayosoma Wakili Mtobesya Ni Sheria inasema kuwa Shahidi anaweza kuandika sehemu tu 75(2) Mahakama inaweza Kuagiza Mtu yoyote Mahakamani Kulingananisha.

Jaji: Je hiyo inahusiana na Mahakama kumuelekeza Shahidi asaini?

Matata: ni tafasiri yangu kuwa Mahakama Inaweza Kuruhusu Shahidi Kuandika ili Kufananisha Kama alichokiandika ni sawa

Mallya: Pale kwenye 75(2) inasema any Documents haijambana wapi kwa hiyo anaweza Kusaini popote (any documents) ili Mahakama ifanye Uamuzi iwe imepata kwa Usahihi wake....kwa usahihi Kifungu cha 75 lakini siyo kwa Kumtaja Shahidi aandike

Jaji: Upande wa Mashitaka

Wakili wa Serikali: Maombi ya Mtobesya Pamoja na Kuegemea kutoka kifungu 75 cha Sheria ya Ushahidi tunaona amekimbia Sana na siyo wakati wake Lakini pangekuwa na Nyaraka Nyingine ambayo Ndiyo Ingekuwa imekuja Rasmi Mahakamani ndipo angetumia.......Njia yako ya Kutaka Shahidi Asaini Ni sahihi Kama watapinga tutashughulikia Kupinga huko wakati huo.

Jaji: Kwa tafsiri yangu Mamlaka iliyopewa Mahakama 75(2) ni naona Mahakama inayo Mamlaka kumuelekeza Mtu yoyote Kufanya Mlinganisho wa Maneno au Namba kwa Nia ya Kuiwezesha Mahakama Kufanya Ulinganisho, ila huyu Mtu aliye na maarifa Kuliko Mahakama Yenyewe. Najiuliza kama ...Leo nilikuwa na Avoid Upande wa Utetezi Kutuzuia Kutumia Nyaraka hii ambayo sisi tumeipata kwenye Comito.

Mtobesya///; Kifungu cha 47 cha Sheria ya Ushahidi ndiyo kinaruhusu Maoni ya Kitaalamu katika Ushahidi Lakini Kifungu cha 48 au 49 Sikumbuki Vizuri kinaruhusu hata mtu asiye Mbobezi Kufanya Maoni yake Hili Kifungu cha 75 chenyewe Kinataka Mahakama Kufanya Ulinganisho.

Jaji: Na Mimi na kubaliana na wewe Lakini kwenye Document uliyonayo hatujui baada ya Kumkabidhi Karatasi at asaini Sahihi gani kati ya hizo Mbili

Jaji: Ndiyo nasema wewe endelea na Jukumu lako kama Walitokea Wakapinga tutashughulikia Pingamizi hilo wakati huo ...na Sheria ya Ushahidi wa Kifungu cha 75 Vyote Vinafanya washitakiwa Kupewa Nyaraka zinazokusudiwa Kutumika dhidi yao kwenye Makosa Makubwa Kama haya kupitia Comito Kwa hiyo watupatie

Mtobesya: Asante Mheshimiwa Jaji

Mtobesya: Naomba nikabidhi iwe Nyaraka Original ya Hati ya Kuchukua Mali iliyosainiwa tarehe 25 2020 inayomhusu Mohamed Ling'wenya Kwa sababu sisi tunayo Moja

Jaji: chini ya Sheria Gani

Mtobesya: Kifungu cha 246 na 146 ya Makosa ya Jinai ...

..Angetoa basi Maombi Rasmi lakini hata kama no Original haiwezi kuitumia kwa wakati huu Haki yake ya Kuhoji aendelee nayo na anaweza Kuitumia hata sasa Sisi tuna tatizo na Procedure jinsi gani Ushahidi huu unataka Kuletwa Mahakamani

Jaji: Jamani Mmeelewa

Wakili wa Serikali: Sisi Haja yetu ni Swala la Procedure Ni kweli Tulianika Ushahidi Tutaokuja kutumia Mahakamani lakini ieleweka Kuwa Ushahidi hi ni Wa Kwetu. Hakuna mahala popote ambapo Mteja wake anaweza Kuwa na haki ya kutumia Nyaraka hizo ......

.Ubishi ulikuwa kama Mshitakiwa Alikuwa ametahiriwa au haja tahiriwa Mahakama ya Rufani ikasema kuwa Hilo ni Kubwa sana Kwake na Isingeweza Kujiingiza katika Risk. Kwa kesi hii basi Kama anataka Mahakama Ijiridhishe. Swala ni Kama Nyaraka hiyo imepokelewa na Kama .......imekubali imeandikwa na Mtu huyu Na pia kama Nyaraka hiyo Nyingine kama Ingekuwa hapa angekuwa na Haki


KESI YA buying wa John dhidi ya Jamhuri criminal appeal namba 450 ya Mwaka 2017 Mahakama iliyoketi Shinyanga Katika Ukurusa wa 11 paragraph ya Mwisho ya a Ukurasa huo wa 11 Ambapo swala Lililojitokeza tangu wakati wa Trial Court na Kesi Ilikuwa ni ya Ubakaji ........

Mheshimiwa Jaji: tunatakiwa tuzingatie Mfumo wetu wa Utoaji haki, Mahakama kwa Kutimiza Wajibu wake anakuwa ni refa na siyo kwa kukaribishwa Kutaka Kufanya Uchunguzi Zoezi kama hilo ni Kuingiza Mahakama katika riski ambazo zinaweza Kuepukika.

...imekubali imeandikwa na Mtu huyu Na pia kama Nyaraka hiyo Nyingine kama Ingekuwa hapa angekuwa na Haki

Na Hilo Ndiyo Dhumuni la Comito Trial kwamba Mshitakiwa ajue anachokuja akujitetea nacho

Upande wa serikali: Sisi tunaona ni Kukiuka Procedure na Maombi hayo tunaomba uyakatae Mheshimiwa jaji Mtobesya: Tunapoteza sana Muda Mheshimiwa Jaji, Shahidi ni wa Kwao na Ushahidi ni wa Kwao Na sijui ni wakati gani tena sisi tutapata Kuwa na wasaa wa kuwa na Shahidi huyu

Na hapa swala la Copy kwa Washitakiwa halijazungumziwa wakati ni Haki kwa Mshitakiwa Kupatiwa Hiyo Nyaraka

Nashon Nkungu: Naona nisaidie Mahakama kama Afisa wa Mahakama alichosema Wakili Robert Kidando Amejieleza Kwenye Kifungu cha 76 tuh asemi kwa nini kuna Haki ya Kukabidhi wa Nyaraka za Comito Na Kingine Kifungu 30 cha Sheria inasema tupewe Copy siyo Photocopy ....

Ambapo wewe Umegundua Sahihi Katika Nyaraka hizo na Zilizopo hapa Mahakamani Sahihi zinatofautiana Kwa Maana hiyo Ukaomba Mahakama ikupatia Nakala halisi Jaji Jambo la Pili Kwakuwa wanasema Ushahidi huo watautumia basi Wahurumie Mapema ili uweze Kuutumia.

Jaji: Mtobesya

Mtobesya: naam Mheshimiwa Jaji

Jaji: hoja zako ulizijenga katika a Mazingira Matatu Haki za Mahakama Jinai hasa akatika Mahakama Kuu, amtu anasomewa na Kukabidhi wa Nyaraka Kwamba wewe Una taarifa Kwamba zipo Nyaraka wanazolenga kuzitumia Kama Ushahidi Wao

Mtobesya: Mheshimiwa nilikuwa naomba Mashauriano na Mahakama ilitusiiipe Mahakama Mzigo wa a kuandika Rulling

Jaji: mnasemaje Jamuhuri

Wakili wa Serikali: Ni Sawa Mheshimiwa

Jaji: Basi tuta Break kwa Dakika 10, tukutane pande zote pale Ofisini

Jaji: anatoka

Mawakili wamerudi

Jaji ameingia tena Saa 6 NA Dakika 24

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 inatajwa tena Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe Kisha Mahakama Kimyaaaaaa

Jaji:
Muda Mfupi Uliopita Tuli-break kwa Nia ya Kuweka Sawa Mambo ya Kitaaluma Baada ya Kuyaweka Sawa na Kualika Sasa Mtobesya Kuendelea

MTOBESYA: Wakati Unaongozwa na Dada Yangu Esther Ulisema Uliandika Maelezo

Shahidi: Niliandika Tarehe 05 Mwezi 08 2020

Mtobesya: aliyeandika Maelezo yako

Shahidi: Sijui Jina lake

Shahidi: anaitwa Jumanne

Mtobesya: Ulishawahi Kukutana na Askari anaitwa Detective Coplo Francis.?

Shahidi: Sikumbuki kama nimekutana naye

Mtobesya: Lakini walikupa Maelezo Ukasoma na kisha Ukaona sawa

Shahidi Ndiyo

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba Nipewe Statement (Handwritten Statement) Naomba Chini ya Kifungu Cha 164 (1h) cha Sheria ya Ushahidi

Wakili wa Serikali Wapo Kimya Jaji anawasubiri

Wakili wa Serikali: Hatuna Pingamizi la Kumpatia hii Nyaraka

Jaji: Pokea

Mtobesya: Shahidi Unajua Kusoma na Kuandika

Shahidi: Ndiyo

MTOBESYA: Shika Karatasi zipo Mbili Soma kama Ndiyo Uliyosoma Ukasaini na Kama Kuna Majina yako na Askari aliye andika Ihakiki Kwanza

Shahidi Anaipekua, anaikazia Macho anafunua funua mara Nyingiyingi

Mtobesya: Ndiyo hiyo.?

Shahidi: Kimyaaaa anatizama tena ile Karatasi, anaipekua

Shahidi: Ndiyo Yenyewe

Mtobesya: Soma Kuanzia Juu Kwa Sauti

Shahidi: Mimi Ndiyo Mwenye Majina na anuani takwa hapo Juu Mkazi Wa Kilimanjaro Nimezaliwa Mwaka 1979 Familia ya watoto Nilikuwa naelekea Saloon Rau Madukani Na baada ya Kumalizia nilieleza Sehemu yangu ya Biashara Kufanya Usafi. Mbele Kuna Bar Na Kukikuwa na Vijana walikuwa wanakunywa Pale Sikuwa nawafahamu Kwa Maana walikuwa ni wageni

Mtobesya: Soma Kote

Shahidi: Sikuwafahamu kwa Maana walikuwa ni Wageni maeneo haya Kwa Muda Mwingi walikuwa wanaongea na simu. Kwangu Afande Mmoja akajitambulisha Jina Afande Jumanne Akaniomba niwe Shahidi huru Ambapo nilishuduia Kufanya Upekuzi Kwenye Kupekuliwa Kijana Mmoja alikuwa na Bastola Zenye nmabaA A 5340 Pia alikutwa na Kete 58 za Madawa ya Kulevya

Shahidi: Shahidi ananendelea kusoma Baada ya Muda walikuja watu watano na a Kuwafuata wale Vijana Na wakaambiwa wapo Chino ya Ulinzi Askari hao walitaka Kufanya Upekuzi ndipo walipokuka Kuni.... Kamyamaza Kidogo Askari hao walihitaji Kufanya Upekuzi ndipo walikuja.......Adam Kasekwa mbaye nilimfahamu Jina baada ya Kuulizwa Jina lake baada ya Upekuzi Na huyo Mwingine aliyekuwa naye alitaka anaitwa Mohammed Ling'wenya ambaye pia kwenye Upekuzi alikutwa na Simu Moja ya Samrt Yenye Line ya Airtel na Hallotel na Kete 21 za Madawa ya Kulevya

Watu hawa wawili nilikuwa siwafahamu Majina wala Sura niliwafahamu baada ya Kutaja Majina yao Baada ya Kukamatwa na Polisi, Askari wale nilikuwa siwafahamu Na Kiongozi wao aliyekuwa anafanya a upekuzi aliwatambulisha kwangu ASP Jumanne.

Baada ya Majina hayo Nilijaza Hati ya Upekuzi Na Kuzuia Mali Walisaini wote na Watu tulioshuhudia Na Afande Jumanne Na baada ya Upekuzi Nilijaza Hati ambayo inaonyesha Upekuzi umefanyika Ambapo tukasaini wote na tulioshuhudia Haya Ndiyo Maelezo Yangu, Sahihi Kama Nilivyoyatoa.

Mtobesya: Nitakurudisha Kwenye baadhi ya Maeneo kama Ulivyosoma

Mtobesya: Ni sahihi Katika Ushahidi wako ulisema Askari wawili walifika wakawaambia Mpo chini ya Ulinzi na Wakawatajia Makosa yao

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Kwenye Maelezo yako hapo, hayo Maneno Yapo au hayapo

Shahidi: Hayapo

Mtobesya: Nilikusikia Unasema hawa Vijana waliokamatwa wao walikuwa wanakunywa wakati wewe unafanya usafi katika Eneo lako la Biashara

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Kwenye Maelezo yako hiyo Taarifa ipo

Shahidi: Haipo

Mtobesya: Nilikusikia Ukisema Kwamba afande Jumanne alikuja kwako akatoa Kitambulisho

Shahidi: Ndiyo alitoa Kitambulisho

Mtobesya: Hayo Maelezo ya kutoa Kitambulisho yapo kwenye Statement yako

Shahidi: Hayapo

Mtobesya: kwenye Maelezo yako nilikusikia watuhumiwa Waliposimamishwa kabla ya Upekuzi walijitambulisha Majina yao kwa Polisi aliyekuwa anafanya Upekuzi Nitakuwa sahihi nikisema Statement Yako inasema Uliwajua Majina Baada ya Upekuzi

Shahidi: Niliwajua Majina kabla ya Upekuzi

Mtobesya: Soma sehemu inayosema nilishuduia wakipekuliwa........ Mpaka inaisha Jina la Afande Jumanne, Soma kwa Sauti

Shahidi: Nilishuhudia Kupekuliwa kwa Vijana hao, na Kupekuliwa Mmoja wao alikutwa na Bastola yenye namba A5340 pamoja na Magazine yanye Risasi 3 .......pia alikuwa na Madawa ya Kulevya Ambae nilimfahamu kwa Jina baada ya Kuulizwa baada ya Upekuzi.

Mtobesya: Kwa hiyo Statement Ulifahamu Kabla au Baada

Shahidi: Baada ya Kupekuliwa

Mtobesya: Nitakuwa sahihi, kwenye Ushahidi wako ulielezea ulisaini Nyaraka Nne za Kushuhudia Upekuzi

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Nenda Sasa baada Upekuzi huo,

Shahidi: Nilijaza Hati ya Upekuzi na Hati ya Kuzuia Mali ilionyesha Upekuzi Umefanyika, ambao tulisaini wote tulioshuhudia pale.

Mtobesya: Ishia hapo, Nitakuwa sahihi nikisema Nyaraka hiyo Uliyosoma inaonyesha ulisaini Nyaraka Moja..? Na siyo Nne kama Ulivyosema Asubuhi ya Leo

Shahidi: kwa Mujibu wa Mstari huu ni Kweli

Mtobesya: Isaidie Mahakama sehemu nataka Usome Kwa Sauti, Soma baada ya Neno Watuhumiwa wale wawili

Shahidi: Baada ya Upekuzi huo na Kusaini Hati ya Kuzuia Mali ambapo tukisaini wote.

Mtobesya: Wakati Wakili Wa Serikali Esther anakuongoza Ulisema aliyekuongoza hapo ni Jumanne

Shahidi: Nilisema ni Afande ambaye sikujua Kwa Jina

Mtobesya: Ipo Kwenye Rekodi, Jaji ataona

Shahidi: hapana

Mtobesya: Ungependa hayo Maelezo Yawe sehemu ya Ushahidi Wako Siku ya Leo

Shahidi: Ndiyo ningependa uwe Ushahidi Wangu Siku ya Leo

Wakili wa Serikali: Hatuna Pingamizi

Jaji: Mahakama imeyapokea Maelezo hayo Kama Kielelezo namba 02 kwa Upande wa Utetezi

Mtobesya: Kwa Ruhusa yako Mheshimiwa naomba Kuendelea

Mtobesya: Ulielezea Mahakama Ulisaini Nyaraka za Uzuiaji wa Mali, zaidi ya Nne

Shahidi: Ndiyo

MTOBESYA: ieleze Mahakama Hati hizo zilijazwa na nani Mpaka Nyie Mkasaini

Shahidi: Zilijazwa na Askari Jumanne

MTOBESYA: na wewe Unakumbuka ulisaini kwenye Hati zote

Shahidi: Ndiyo

MTOBESYA: Unaweza Kuisaidia Mahakama Ulisaini Upande gani

Shahidi: Pale Mwisho Kwa Pembeni

Mtobesya: Naomba Nimuonyeshe Shahidi ID 1 Nitakuwa Sahihi Nikisema Nyaraka zote Nne ulisaini hapa Kwenye Jina lako

Shahidi: Siyo zote sehemu hii, Zingine Nilisaini Upande wa Kushoto na Zingine Upande wa Kulia.

Mtobesya: Unaweza Kutuambia Ulizosaini Upande wa Kushoto zinaruhusu nani na Kwaajili ya Vifaa Vipi

Shahidi: NilizoSaini Upande wa Kushoto zilikuwa zinamhusu Adam

Mtobesya: Hizo Ulisaini Upande wa Kushoto

Shahidi: Nilisaini Upande wa Kulia

Mtobesya: na Zilizomuhusi Mohammed Ulisaini Upande gani

Shahidi: Upande WA Kushoto

Mtobesya: Ulisaini Baada au Kabla ya Jina lako

Shahidi: Nilisaini baada ya Jina langu

Mtobesya: Na Ni Ushahidi wako Mbele ya Mahakama zote Ulisaini wewe Mwenyewe na kwa Mwandiko wako

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Na Kwa Ushahidi Wako Saini zako umesaini wewe Zikiwa zinafanana

Shahidi: Kuna zingine zilikuwa hazifanani kwa sababu nilikuwa na Hali tofauti

Mtobesya: Mweleze Mheshimiwa Jaji Sasa ni hali ipi Ulikuwa nayo ikapelekea Saini zako Kutofautiana

Shahidi: Kuna saa, wakati wa Ukamataji Nilisaini wakati nimesimama na Zingine nimesaini wakati nimekaa kwenye Meza.

Mtobesya: Unaieleza Mahakama Ukisaini ukiwa umesimama na Wakati Umekaa saini lazima zitofautiane

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Nilisikia wakati anakuongoza Dada Yangu Wakili wa Serikali Kuwa Mlisaini wakati Wa Tukio

Shahidi: Wakati natoa Maelezo Nilisaini Nikiwa mezani lakini Zile zingine Nilisaini nikiwa nimesimama

Mtobesya: Ni Signature zipi sasa zinazofanana ukiwa Umekaa au Umesimama

Shahidi: Nikiwa Nimekaa ndiyo zinafanana

Mtobesya: Ukiwa Umekaa umesaini Mara Ngapi na Nyaraka zipi

Shahidi: Zile ambazo nilikuwa kituoni kutoa Maelezo.

Mtobesya: Zote ambazo ulisaini Ukiwa Umekaa Zina fanana..?

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Zote ulizoSaini Ukiwa Umesimama Zinafanana au hazifanani

Shahidi: Zinafanana

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba Kuishia Hapo

Mtobesya: naomba Kurudisha Kielelezo

Jaji: Wakili Malya unahitaji Muda gani

Mallya: Nusu saa hivi

Mallya: Bado unauza Mbege

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Mbege unayouza wewe inalewesha

Shahidi: Kuna Inayolewesha na Isiyolewesha

Mallya: Una Ndugu au Mume ambaye ni Polisi

Shahidi: Hapana

Mallya: Ulitambuaje kuwa hiki ni Kitambulisho cha Polisi?

Shahidi: Niliona Chapa ya Taifa

Mallya: Kitu gani Kingine Uliona

Shahidi: Niliona Jina lake

Mallya: Lilikuwa limeandikwaje

Shahidi: kwa kweli hapo Sikumbuki

Mallya: Umesema Wakati Unafanya Shughuli zako za Usafi na Vijana walikuwa wanakunywa Bia, Ni hatua ngapi

Shahidi: Ni hatua 10

Mallya: Napiga hatua Mahakamani

Mallya: Hapa Kuna Hatua Saba tu

Mallya: Umbali wa Hatua 10 Macho yako yanaona Vizuri

Shahidi: Yanaona Vizuri

Mallya: hapa Kuna Umbali Wa Hatua 7 tu Unasema Mtu Amevaa Tshirt yenye Rangi Nyeusi wakati ni Dark Green Je unataka Mahakama iamini kwamba unaona Vizuri?

Jaji: umeelewa swali..?

Shahidi: ..natumiaga Miwani, Sema Leo nimesahau Miwani

Mallya: Ulielezea Kuwa siku ya Tukio ulivaa a Miwani

Shahidi: Hapana

Mallya: Siku ya Tukio ulikuwa Umbali wa Mita 10 Leo Mshitakiwa yupo hatua 10 tu hakuna aliyevaa Tshirt Nyeusi, unataka Kumwambia Mheshimiwa Jaji unaona Vizuri?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

JAJI: umelielewa Swali

Shahidi: Ndiyo

JAJI: Jibu Basi

Shahidi: Kuna saa Macho yanashida.

Mallya: Wakati Unatoa Maelezo Leo Uliomba Miwani uweze Kuangalia Vizuri.?

Shahidi: Sikuomba

Mallya: Ni sahihi Kuwa Usajili wa Simu unafanya kwa Kitambulisho?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: na wewe Uliwaona watu waliopo Mahakamani walikuwa wanasajili Line za simu

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwenye Maelezo Yako kuna sehemu umesema Wanasajili lini?

Shahidi: Hakuna

Mallya: pale Rau Bia wanauza au Bure?

Shahidi: Wanauza

Mallya: Wakati mnawapekua Mliwakuta na Bastola na Siyo Pesa

Shahidi: Hakuwa na Pesa

Jaji: Watakuwa walishalipaaaaaa

MAHAKAMA kichekoooooo

Mallya
: zoezi la Kufanya usafi Lilichukua muda gani?

Shahidi: Kwa muda wa Kufanya Usafi kama Dakika 10

Mallya: Wakati Tukio linatoka Ulishamaliza Usafi au Ulikuwa unaendelea

Shahidi: nilikuwa naendelea ikabidi Nisimame

Mallya: Tukio la kukamatwa lilichukua Muda gani?

Shahidi: Rudia swal?

Mallya: Kitendo Cha Kukamatwa hawa watu Mpaka unaitwa kushuhudia ilichukua muda gani?

Shahidi: kama Dakika 03

Mallya: Kwa hiyo tukijumlisha Dakika 10 za Usafi na Dakika 3 wakakuita wewe Zoezi la Kusachiwa lilidumu kwa a muda gani?

Shahidi: Kwa Dakika 45

Malya: Saa Nane ilikuwa imefika

Shahidi: Kama saa Nane Kasoro

Mallya: Kwa Maelezo Yako wewe yalitolewa Umesaini Ukiwa polisi saa 7 kamili Je, tukuamini wewe au?

Shahidi: Muamini Maneno Yangu

Mallya: Tuchukue Yote.?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kabla ya kwenda Kwenye Tukio Siku hiyo ulikuwa wapi na wapi

Shahidi: Nilitoka Nyumbani baada ya Usafi, Nikaenda Kwa Mgonjwa na Baadae Saloon

Mallya: Umeulizwa aliyekuchukua maelezo Yako ni nani

Shahidi: Simfahamu Kwa Majina

Mallya: Hakukuonyesha Kitambulisho ndiyo Maana Humkumbuki?

Shahidi: Hapana alinitajia nimemsahau

Mallya: Kwa kutazama Kwa Macho yako sahihi yako uliyosaini Hapa na Hapa Kwenye Exibit 02 zinafanana

Shahidi: Hazifanani lakini ni sahihi zangu

Mallya: Kwenye Maelezo Yako umeeleza Mahali Kiongozi wao, Afande nani

Shahidi: Afande Jumanne

Mallya: akitokea Mtu akisema yeye ndiyo Kiongozi aliyekwepo atakuwa Muongo

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Unamfahamu Kingai

Shahidi: Hapana

Mallya: na Ulisema Mapolisi walikuja kujitambulisha kwako.?

Shahidi: alikuja Mmoja

Mallya: Askari waliowakamata watuhumiwa walikuwangapi

Shahidi: Walikuwa watano

Mallya: Mheshimiwa Jaji ni hayo tuh

Jaji: Mnasemaje Tubreak au tuendelee

Wakili wa Serikali: Tubreak

Jaji: kwa Muda gani

Peter Kibatala: Kwa Sababu tulisha Kaa Dakika 30 tupumzike Kwa Dakika 45

Jaji: Mnasemaje Serikali

Wakili wa Serikali: Sawa

Jaji: Shahidi Tunapumzika, tunywe Maji tutarudi baadae Kidogo

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 inatajwa Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe

Jaji anaandika Kidogo

Wakili wa Serikali: Kwa Upande wa Jamhuri

Upande Wa Utetezi: tupo tayari Kuendelea

Matata: Shahidi nitakuhoji Maswali Machache utajibu kwa Sauti

Matata: Umesema wewe ni Mwenyeji Wa Miaka 08 pale Rau Madukani

Shahidi: Katika Biashara

Matata: Lakini pia Umesema Unaishi Pale pale

Shahidi: Ndiyo

Matata: Umesema Pale Rau Madukani ni Kata, Kijiji au Kitongoji

Shahidi: Kata ya RAU Madukani

Matata: Utakubaliana na Mimi Hukusema Pale no Kata ya RAU Madukani

Shihidi: Ndio

Matata: Utakubaliana na Mimi hujatutajia Unatoka Mtaa Gani hiyo Kata Ya Rau

Shahidi: Sikuulizwa

Matat: Hujatutajia Hata MwenyeKiti wa Mtaa wako

Shahidi: Sijaulizwa

Matata: hujatuambia pia Kuwa unaishi kwenye Nyumba yako au Nyumba ya Kupanga

Shahidi: Sikuulizwa

Matata: Unaishi Nyumba yako au Umepanga

Shahidi: Nimepangisha

Matata: Kuna Mkataba Ulileta hapa Kwamba wewe Umepanga Rau

Shahidi: Sikuleta

Matata: umetutajia Umepanga Nyumba ya Nani

Shahidi: Sijaulizwa

Matata: Umesema Unafanya Shughuli Ya Kuuza Mbege

Shahidi: Ndiyo

Matata: hujasema kama Mbege Unanunua au Unaitengeneza

Shahidi: Sijaulizwa

Matata: Umesema Pale Rau Una eneo la Biashara

Shahidi: Ndiyo

Matata: Umeonyesha Hati wala mKataba wa Pango

Shahidi: Hapana

Matata: Umesema Wakati wa Maelezo Yako Una Glocery, Stationary, Kibanda Cha Simu

Shahidi: Ni sahihi lakini sasa....

Matata: Inatosha

Matata: hujatutajia Mtu Yoyote zaidi ya Huyo Esther ambaye ni Shahidi

Shahidi: Sijataja

Matata: hujatutajia Hata Saloon au Mtu aliyekuosha Hizo Nywele

Shahidi: Sijaulizwa

Matata: Wakati Ukiwa eneo lako la Biashara uliona Vijana wangapi wakiwa wanakunywa Bia

Shahidi: Niliona watatu

Matata: Ukasema Walikuwa wanasajili laini za Simu

Shahidi: ndiyo

Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili Mallya Ukasema hawasajili laini

Shahidi: walikuwa wamekaa Meza Moja na Kijana anayesajili laini

Matata: Mahakama Ichukue Lipi walikuwa Wanakunywa Bia, Wanasajili Laini au Walikuwa waMekaa Mezani?

Shahidi: Ichukue Yote kwa sababu yalikuwa yanafanyika kwa Pamoja

Matata: Mtu anaweza Kuwa anakunywa Bia, anasajili Line na wakati huo huo amekaa mezani..?

Shahidi: Ndiyo

Matata: ulielezea Mahakama Kwamba Mlifika Saa ngapi Polisi

Shahidi: Hapana Sikuulizwa

Matata: naomba Exhibit P2

Matata: Shika Maelezo Yako

Matata: Wakati Unaulizwa na Wakili ulisema aliyekuwa anashuhudia ni wewe na Esther Sasa iambie Mahakama Katika Maelezo yako ni wapi Esther ametajwa

Shahidi: Hajaandikwa


Matata: Mheshimiwa ni hayo tu

Kibatala: Shahidi saa hizi ni Saa ngapi?

Shahidi: Saa 9 Kasoro

Kibatala: umeona wapi

Shahidi: Kwenye Saa

Kibatala: unaona yake Magari pale Nje

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Rangi gani

Shahidi: Ni Pink, Nyeupe na Blue

Kibatala: na Hapo hujavaa Miwani

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mallya alipokuuliza kwa sababu ya kutomtambua Mshitakiwa Ukasema Unatatizo la Macho na Sababuhujava Miwani

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ila Kwa Sasa wakati nakuuliza hujava Miwani

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na wala hujamuomba Mheshimiwa Jaji Uvae Miwani

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Umekuja Hapa ukitokea wapi

Shahidi: Gesti

Kibatala: Mara ya Mwisho Kuwa Rau Madukani ni lini?

Shahidi: Ijumaa

Kibatala: Ulikuwa Unaendelea na Kuuza Mbege Rau..?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: aliyekuuzia Mbege Mwezi wa 05 ni nani?

Shahidi: Mama kazi Moto na Mmoja anaitwa Paulo

Kibatala: Wewe Majina Mengine ni Mama Pendo..?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: na Ni kweli husimami wewe Peke yako kuna Mtu anakusaidia

Shahidi: Wakati upi

Kibatala: Ni Kipindi Kipi Binti yako alikuwa anauza pale

Shahidi: Alianza Juzi Jumamosi

Shahidi: ananyoosha Kidole

Kibatala: Unataka Kurekebisha Jibu

Shahidi: Kuna Binti yangu ananisaidiaga Usafi

Kibatala: anaitwa Nani

Shahidi: Naitwa Pendo

Kibatala: katika Ushahidi wako Ulizungumza Lolote kuhusu huyu Pendo

Shahidi: Sikuzungumza

Kibatala: pale Rau Madukani Karibu na Tukio lilipotokea kuna Mtu anaduka la Vipodozi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kuna Mtu ana Duka la Jumla

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na Mtu huyo Mwenye Duka la Jumla Ndiyo yenye fremu za Vipodozi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na Pana Flemu 4 kwa Upande Mmoja

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na Upande wa Pili ndiyo wanauza Vinywaji

shahidi: ndio

Kibatala: Anayeuza Duka la Vipodozi anaitwa Athima

Shahidi: Sijui Jina lake

Kibatala: ila Unajua ni Mmama au Mdada

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na ndiyo anakaa Mbele ya Duka lake

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Picha hii tunayozungumza, ulimchorea Jaji hiyo Picha

Shahidi: Hapana


Kibatala: Unajua kuwa kwanini unajua kwanini Ujamchorea Jaji

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ni Kwasababu wewe Ni Shahidi wa Kupanga

Shahidi: Hapana Kabisa

Jaji: Naliondoa hilo Swali

Kibatala: Twende kwenye Bastola

Kibatala: Ulikuwa unampekua

Shahidi: Hapana

Kibatala: ulijuaje Kuwa kulikuwa na Vitu vigumu

Shahidi: Baada ya kutoa kwenye mfuko

Kibatala: na Ulishuhudia MADAWA ya Kulevya

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unga ni kitu kigumu

Shahidi: Kitu kilaini

Kibatala: Kuna sehemu uliona namba za Bastola CZ 100

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mpaka unamaliza Zoezi la Kuulizwa na Serikali hakuna aliyekutajia hizo namba

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unakumbuka ulisema zilipatikana Risasi tatu na Magazine

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: hapa Mahakamani Umeonyeshwa hizo Risasi

Shahidi: Hapana

Kibatala: kwa hiyo hujamsaidia Mheshimiwa Jaji Kuwa kutambua Risasi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Umesema Kuhusu Magazini, unajua magazine inakaa wapi kwenye Bastola

Shahidi: Upande wa Chini

Kibatala: Umemwambia Mhe. Jaji Kwa Kufafanua Kuwa Magazine inakaa hapa

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wakati Umetoa maelezo yako ambayo yapo katika D2 kwamba Kuna Afisa Wa Askari Alichomoa Magazine Ukaona Risasi 03

Shahidi: Nilisema

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naomba Kielelezo Namba D2

Kibatala: Nionyeshe ni wapi

Shahidi: Hakuna Sehemu Kama hiyo

Kibatala: Kwa hiyo tunakubaliana Jibu la Kwanza ni Uongo

Shahidi: Hapana siyo Uongo, Makosa ya Mwandishi

Kibatala: Nichukie lipi sasa

Shahidi: Chukua Yote

Kibatala: ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuna Kitu Mwandishi amekiacha ambacho Mimi nilikisema. Ulimwambia Mheshimiwa Jaji

Shahidi: sikumwambia

Kibatala: Ni sahihi Kuwa Kielelezo D2 haitaji Jina la Askari yoyote isipokuwa Jumanne

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: kwa sababu walijitambulisha ukajisahau

Shahidi: Ndiyo walijitambulisha Nikasahau

Kibatala: Unatatizo la Kumbukumbu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Soma Kuanzia Neno baada ya Upekuzi huo

Shahidi: Nilishuhudia na Kusaini Fomu za Upekuzi

Kibatala: Mwambie Mhe. Jaji hapo kwenye watu wawili kama Umefafanua

Shahidi: Hapana

Kibatala: Pia Mlisaini Wote

Shahidi: Ulifafanua, Neno Watu wote

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wakati yanaandikiwa Uliambiwa ni Maelezo ya Kisheria au Mapambo

Shahidi: niliambiwa ni Maelezo Yangu

Kibatala: Kwa Mujibu wa maelezo haya Adam Kasekwa Ulifahamu Jina Lake Baada ya Upekuzi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unafahamu Mshitakiwa tuliye naye ni Adam Kasekwa Maarufu Kama Adamoo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unakubali Hakuna Sehemu uliyotaja Adamoo

Shahidi: Ndiyo Sikutaja

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji ni kweli au siyo Kweli Kwamba Katika Kielelezo ukichosema hapo Hakuna Adamoo

Shahidi: Hakuna Adamoo

Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kwamba Unatakiwa Kusema Ukweli ndiyo Maana Unaapishwa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Jaji akupime Ukweli au Uongo wako kwa hilo Soma hapa

Shahidi: Adam Kasekwa Adamoo

Kibatala: awali ulisema ipo au haipo

Shahidi:Nilisema Haipo

Kibatala: Sasa wewe ni Muongo au Mkweli

Wakili wa serikali: OBJECTION Pius Hilla Swala la Kweli au Uongo aiachie mahakama

Jaji: Naona Shahidi anaweza Kujibu yeye ni Mkweli au Muongo

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa

Kibatala: Swali langu lipo palepale Kutokana na Mgongano wa Majibu, Mwanzoni Ulisema jins ls Adamoo Haipo na baadae tukasema Kwa pamoja Ukaona Ipo, Wewe ni Shaidi wa Ukweli au Uongo

Shahidi: Mimi ni Shahidi wa Ukweli

Wakili wa Serikali: Robert Kidando Hiyo sehemu ichukuliwe kwa makini

Kibatala: Sijaona Objection na Shahidi amejibu

Jaji: Mimi sijasikia Swali

Kibatala: Unakumbuka ulisema uligundua namba ya Bastola..?

Shahidi: afande Jumanne

Kibatala: Na ndiyo Unavyosema Katika Maelezo yako

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Hakuna mahala Umesema Kuwa "Mimi ndiye niliyesoma na Kugundua Namba za Bastola

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo

Shahidi: Kwenye hiyo Fomu Hakuna

MAHAKAMA kichekoooooo

Kibatala:
Wacha Nirudie tena

Kibatala: Kuna Mahala Umesema wewe Ulisema namba za Bastola

Shahidi: Kwenye maelezo haijaandikwa

Kibatala: Katika MAELEZO yako kuna Mahala au Kuna sehemu Yoyote Kuna Jina Luger..?

Shahidi: Lipo

Kibatala: hii fomu alijaza nani?

Shahidi: afande Jumanne ndiyo alijaza

Kibatala: ulimfafanulia jaji tofauti ya Kielelezo Kimoja kina Luger na Kingine hakina

Shahidi: Hapana sikumfafanulia

Kibatala: Katika Maelezo Yako E2 ulitaja Aina za simu, Je Namba ya Simu Uliweka Kwenye Kielelezo Chako

Shahidi: Hapana Sikuweka

Kibatala: na wala hiyo Tofauti hukufafanua

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Shahidi Unafahamu IMEI namba za Simu ya Adama Kasekwa?

Shahidi: Hapana

Kibatala: na wala hukufahamu kuwa kuna IMEI Moja wala 02

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikal hukufafanua kuhusu IMEI Moja au Mbili kwa Mtu anayeitwa kasekwa

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wala Hukuomba Ujikumbushe labda kwa Sababu Namba ni Nyingi, Ulifanya hilo zoezi

Shahidi: Hapana

Kibatala: katika hiyo Karatasi Kuna Maneno kama CZ 100 ya Kufafanua hiyo Bastola

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Walikwambia Karatasi hii Ndiyo inatakiwa kumtia Hatiani Mshitakiwa bila Kuacha Shaka yoyote

Shahidi: Niliambiwa

Kibatala: Twende Simu Card ya Vodacom

Kibatala: Unafahamu Kwanza hiyo ICCD namba

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwa hiyo Unakubaliana nami kwamba hizo ICCD Namba ambazo ndiyo Utambulisho katika Ushahidi wako hazijaingia

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: hata namba ya Adam Kasekwa ya Hallotel kuhusu ICCD namba, hukutaja hivyo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: wala hukufafanua

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: wala hujazungumzia Kabisaaaa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: katika Ushahidi wako ulitambua huyu kama nani

Shahidi: Kama Mohammed Ling'wenya

Kibatala: Katika Ushahidi Wako ulimtambua Mtu anaitwa Mohamed Abdilah Ling'wenya

Shahidi: Hapana Sikutaja Ling'wenya

Kibatala: Kwenye Statement D2 Ulimtaja huyu Kama nani tunakubaliana tutakachokipata pia tukitumie

Shahidi: ndiyo

Kibatala: Naomba D2 Kibatal:a Taja huyo Mtu humo Umemtaja Kama Mohammed Abdalahi Ling'wenya

Shahidi: Ndiyo Mohamed Abdilah Ling'wenya

Kibatala: Mwanzoni Umesema Halipo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulifafanua Kuwa Katika Utambuzi hapa Mahakamani na ile Hati yako ya maelezo pamoja Na kutofautiana, Ulifafanua Kwa Jaji kwamba huyo ni Mtu Mmoja

Shahidi: Shapana

Kibatala: Katika Ushahidi Wako Kuna Mahala Popote umezungumzia Kuna Afisa Wa Polisi anaitwa Ramadhan Kingai

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wakati Maafisa Wa Polisi wanajitambukisha ulikwepo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala Hakuna Mahali Umezungumzia Kuhusu Kingai, Kwamba alikwepo ila hujamtaja

Shahidi: Sijazungumza hilo

Kibatala: Wakati Unaulizwa Maswali na Mtobesya kuhusiana na Saini zako na Kuna Mazingira zinatofautiana na Kwamba Kuna fomu ulisaini Ukiwa Umesimama

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Wakati Jumanne anajaza hii fomu pia alikuwa amesimama?

Shahidi: Ndiyo alikuwa amesimama

Kibatala: mara zote wakati Unatoa Ushahidi wako Ulikuwa Unatoa Maneno "Glocery" Mwambie Mheshimiwa Jaji Katika Maelezo yako kuna Neno Glocery?

Shahidi: hakuna

Kibatala: Maneno gani uliyatumia

Shahidi: Bar

Kibatala: Ulifafanua kwa Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulikuwa unalenga Kitu Kimoja hicho hicho

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Kati yako wewe na Fremu 4 za Jumla na Vipodozi na Upande wa Pili Ndiyo Glocery na Kwamba Sehemu yako ya Mbege ni Nyuma kabisa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kutoka Kwenye Fremu 4 Duka la Vipodozi hadi eneo la Tukio ni hatua ngapi?

Wakili wa serikali: Objection Shahidi ameshasema hamfahamu Athma

Kibatala: Kutokaa kwenye Flemu 4 Mpaka waliokamatwa hawa ni Kama Hatua ngapi

Shahidi: Kama 10

Kibatala: Bado Unasisitiza Ushahidi wako waliwaacha hawa wa kwenye Fremu hatua Tatu wakakufuata wewe wa Hatua 10

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Shahidi Unafahamu au hufahamu Mmlilki wa hilo Duka la Jumla na Duka la Vipodozi ni Dada yake Ling'wenya.?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: hilo eneo lina Kiongozi wa Mtaa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: anaitwa nani

Shahidi: Sigfrid Malewa

Kibatala: Katika hizi Hati hapa unaona Jina la Sigfrid Malewa

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Msaidizi Wake anaitwa nani

Shahidi: Namjua Kwa Jina Moja la Temba

Kibatala: anaishi wapi na eneo hilo

Shahidi: anaishi Mbali

Kibatala: katika Kielelezo chako Namba 02 Mnamo tarehe 05/08/2020 nilikuwa naenda Saloon hapo Rau Madukani

Shahidi: Ni kweli nilisema hivi

Kibatala: Kwamba Saa 7 Kamili Mchana

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulitoa Ufafanuzi kwamba Ulikuwa ni Muda wa Makadirio

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Huko Saloon Ulikaa Muda gani?

Shahidi: Kama Robo Saa

Kibatala: Na Ukamwambia Mallya Ukarudi Sehemu ya Biashara Kwa muda gani

Shahidi: Kama Robo saa

Kibatala: kwa hiyo kama Saa Saba Na Nusu

Kibatala: kwa hiyo kama Saa Saba Na Nusu

Kibatala: Na Katika Kielelezo Chako D1 Maelezo uliyoyatoa Ulisema ni Saa Saba, Si Unaona kuna tatizo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Tatizo ambalo hukulitolea Ufafanuzi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Nani atutatulie hili tatizo

Shahidi: Mimi Mwenyewe

Kibatala: Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali nilikusikia ulisema, hawa washitakiwa wawili walipigwa Pingu, ulimwambia Mheshimiwa Jaji Sasa Kama baada ya Kupigwa Pingu nini Kiliwatokea

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Mlifika central police Kwa usafiri gani

Shahidi: Watuhumiwa WALIENDA kwa Gari Nyingine na sisi tukaenda na Gari Lingine

Kibatala: na ukamwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba na hilo gari lina Maofisa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Aliwahi Kukwambia Kesi Mama ipo Dar es Salaam

Shahidi: Hakuwahi kuniambia

Kibatala: Wewe ulikuwa unajua kesi na Kila kitu kipo Moshi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: ulisikia hao Maaskari wanaongea na Mtu yoyote kuhusu washitakiwa Kukamatwa

Shahidi: Hapana

Kibatala: ulisikia Maofisa Wa Askari, Kwamba Yupo wapi Moses Lijenje

Shahidi: Nilisikia akimuuliza Mwenzenu

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji huyo Mwenzao Katika Statement Yako D2 umezungumza Walikuwa wangapi

Shahidi: Watatu

Kibatala: Maelezo yako chini ya Kiapo, Kielelezo D2 ulizungumzia kuhusu Vijana watatu

Shahidi: Hapana

Kibatala: we Umezungumzia wangapi

Shahidi: wawili

Kibatala: palikuwa na Vijana wawili wanakunywa pale, Ndiyo ukivyosema

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji huyo Kijana wa tatu, umezungumzia Nini Kilitokea huyo Kijana wa tatu.?

Shahidi: Hapana

Kibatala: zoezi la Kusajili laini ya Simu, uliona kwamba wanasajili Simu

Shahidi: Ndiyo niliona

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji walikuwa wanasajili Laini ya kampuni Gani

Shahidi: Sijui sasa Kibatala: Unafahamu iwapo Ndiyo au Lah kwamba hii laini ya Hallotel au Airtel ndiyo zilikuwa zinasajijiwa Siku hiyo

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mlivyofika pale Polisi Central Station Moshi Iwapo Ulimwambia Chochote Kuhusu Kushuhudia Vile Vifaa Vikiingizwa Kwenye Daftari rasmi

Shahidi: Hapana

Kibatala ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Iwapo hawa washitakiwa wawili walikuwa na vitu kama Wallet au Kitu Kingine anavyobeba Kijana wa Kiume.

Shahidi: Sijazungumzia

Kibatala: Wewe Kama shahidi Huru, Kama Ulishuhudia MALI Binafsi za Washitakiwa Kuingiziwa kwenye Daftari Maalum pale Kituoni

Shahidi: Si kumwambia

Kibatala: nimesikia mara kadhaa unataja DADA Esther ulifafanua Kwa namna yoyote ile

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba huyu Dada Esther Unamfahamu anaishi wapi

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu Watu wenye Biashara Ndogo Ndogo hupewa Kitambulisho Maarufu Kama Kitambulisho cha Wamachinga

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: ulimuonyesha Mheshimiwa Jaji ili ajue Kuwa Unakitambulisho

Shahidi: Hapana

Kibatala: ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Biashara yako inaitwaje kama vile Mama Mbege

Shahidi: Hapana

Kibatala: hata kumwambia Mheshimiwa Jaji kwamba Umesahau kutaja Jina la Biashara yako ulisema

Shahidi: Sikusema

Kibatala: ulisema hapa kwamba Mohamed Abdilah Ling'wenya Alikuwa amevaa Nguo gani wakati anakamtwa

Shahidi: Sikusema

Kibatala: na Adamu Kasekwa ulisema amevaa Nguo gani

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama Ulisema ulishuhudia kielelezo Namba Moja kilijazwa Kwenye Fomu tatu na Fomu Moja akapewa Adam kasekwa

Shahidi: Hapana

Kibatala
: Ulisema Kwamba Ulisikia Afisa wa polisi akisema Unahaki ya kupata fomu Moja ya Hati za Kuchukulia hiyo Bastola

Shahidi: Hapana

Kibatala: unasema Ulifanya Kazi na Afisa wa Askari Wa a Polisi Jumanne, na baadae wakakuonyesha Afisa Mwingine wa Polisi aliyekuchukua maelezo Je ulitolea Ufafanuzi kwa Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Hapana

Kibatala:
Leo umesema Kwamba Bastola Ina Rangi Nyeusi, Je katika Maelezo yako Kuna Sehemu Umetaja Rangi ya Bastola

Shahidi: Hapana

Kibatala:
kwa hiyo Rangi umetaja Leo

Shahidi;
Ndiyo

Kibatala: ulifafanua Kwa Mheshimiwa Jaji kamba wewe kabla Ulikuwa Unaifahamu kabla

Shahidi: Hapana

Kibatala:
Pamoja na Kwamba Wakati Ule ndiyo Ulikuwa na Kumbukumbu, Maana umesema wewe Tukio la Muda Mrefu, Mpaka unasahau, Lakini wakati Ule Hukusema Rangi ya bastola.

Kibatala: nimesikia umesema Vitu vinavyodhaniwa kuwa Madawa ya kulevya, Je kuna Mtu yoyote alimtuhumu baada ya Kupatikana kwa Madawa ya kukevya

Shahidi: Hapana?

Kibatala: kwa Ushahidi wako wewe unasema Adam Kasekwa alipatikana na Madawa ya Kulevya

Shahidi: Sikufahamu hatima yake

Kibatala:
Kuhusu Saini ya D01 na D02 ulifafanua kabla ya Wakili Mtobesya Kuuliza maswali

Shahidi: Hapana Sikufafanua

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Shahidi Huyu naomba Kuishia hapo

Jaji anaandika

Wakili wa Serikali: Tunaomba Hairisho ili tuweze Kumalizia Asubuhi

Jaji:
Kuna Kama Dakika 50 hivi ilituweze Kuhitimisha Leo

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa Ngoja tuendelee

Jaji: Wakili wa Serikali Esther Martin

Wakili wa Serikali: Umeulizwa Mahakamani na Malya Kuhusiana na Rangi za Tshirt na ukasema siyo Nyeusi Bali Rangi ya Dark Green, Wewe ulikuwa Unaona nini

Shahidi: Nyeupe, Kijani na nyeusi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia Maswali Kwenye Kielelezo D2 ukaambiwa Vitu mbalimbali Kwenye Maelezo hayo uliyoandika Polisi Watuhumiwa hawakujulishwa Makosa yao, Na Mengine Mengi fafanulia mahakama ni Vipi hayo yamejitokeza

Shahidi: Rudia Swali

Wakili wa serikali: Swala la Watuhumiwa baada ya Kuambiwa Kaa chini kama walijulishwa Makosa yao, Mahakamani umesema lakini humu hayapo

Mtobesya: samahani, Shahidi anaenda kujazia Statement

Jaji: tungemuacha ajibu kwanza

Wakili wa Serikali: Nasema wakati wakili anamuuliza Maswali akakuuliza kuhusu Maswali Ambayo Hapa Mahakamani umesema ila Kwenye Maelezo Hakuna, Ni kwa vipi hayo yamejitokeza

Shahidi
: Yamejitokeza kwa sababu ni uandishi tu

Wakili wa Serikali: Kivipi Shahidi: Katika Kutoa......Maelezo niliyoandika na maelezo ya hapa mahakamani.

Wakili wa Serikali:
Uliulizwa pia Kuhusu Maelezo haya, pia kwamba Fomu iliyosainiwa eneo la Tukio ni Moja lakini Mahakamani umesema Fomu nne

Shahidi: Kimetokea tu Lakini fomu zilikuwa Nne

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kwamba Ulijuaje kwamba Ulichokiona ni Kitambulisho Cha Polisi, Ukasema Ukaona Chata ya Taifa

Jaji: Siyo Chata Bali Chapa

Shahidi:
Nilikuwa namaanisha Chapa ya Kipolisi

Wakili Malya: Tunapinga hilo Jibu

Jaji: sahihi, Hakujibu hivyo

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kama Ulionyesha CZ 100, Fafanunua Mahakamani wewe Uliona nini

Shahidi: Niliona A5340

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia Kwamba Kwenye Maelezo haya Uliyasoma na Uliyajua Majina Baada ya Upekuzi lakini Mahakamani Umesema Kabla ya Upekuzi

Shahidi: Niliyajua hayo Majina Kabla ya Upekuzi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Mimi nimemaliza namuachia Mwenzangu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Uliulizwa Kama Vijana wawili pale Rau Uliwaona Wakisajili laini na Baadae Ukasema Walikuwa na Kijana anayesajili laini

Shahidi: Mimi niliwaona na Kijana anayesajili Laini

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kwamba hao Vijana walikuwa wawili na Baadae Ukasema watatu. Wakati gani Uliwaona wakiwa watatu

Shahidi: Wakiwa wanasajili laini

Wakili wa Serikali:
Wakati gani walikuwa wawili

Shahidi: Wakati wa Ukamatwaji

Kibatala:
Objection anasema Jina la Amelifahamu lini it's a New fact

Jaji:
hili swali limezungumza Katika Mazingira Matatu Kama alitaja, Kama ALIJAZA fomu na Kama alitaja kabla Hili Jibu la Lini alimfahamu nafikiri siyo Fact Mpya

Wakili wa Serikali:
Uliulizwa Kwenye Fomu kuhusiana na Neno Adamoo Kama Ulikuwa umelisema, Fafanua Hapa Mahakamani Jina la Adamoo Umelifahamu lini

Shahidi:
Nimelifahamu Leo

Wakili wa Serikali:
Uliulizwa swali Kuhusiana na Ukamataji kuhusiana na Lile Neno CZ100 Halipo, elezea Kilichoandikwa kwenye Hati hiyo ni nini

Shahidi:
Iliandikwa namba A5340

Wakili wa Serikali:
Uliulizwa pia na Kuhusu Hati yako Kuhusu Glocery na Huku ni Bar, Kwa Mujibu wa Ushahidi wako walikuwa kwenye eneo lipi

Shahidi: walikuwa kwenye Glocery ya Dada Esther

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusiana na maeneo waliokamatwa watuhumiwa haswa tarehe 05 Mwezi 08 Ukasema Duka la Jumla na Vipodozi na ulipokuwa wewe Eneo lipi walikuwa karibu

Shahidi:
eneo waliokamatwa ni Karibu na Sehemu yangu ya biashara.

Wakili wa Serikali
: kwanini jina Sweetfred Malewa Halipo kwenye Hati ya Upekuzi

Shahidi:
Sikuulizwa

Wakili wa Serikali:
Kuhusu wewe Kufika kwemye eneo lako la Biashara, Muda gani ulienda Saloon na Muda wa Ukamataji kuwa saa Saba, Kilichotokea kilikuwa saa ngapi

Shahidi:
ilikuwa majira ya Saa Saba Mchana

Wakili wa Serikali:
Uliulizwa Kama uliona Watuhumiwa kama walipofikishwa Polisi, Kama Ulishuhudia Uandikishwaji wa vitu vyao Kwanini hukutoa Ushahidi huo

Shahidi: Sikutoa sababu Sijaulizwa

Jaji:
Jamani Mnasikia hukoooooo.? Mahakama Hatusikiiiiiii

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kwamba kama katika Ushahidi wako alikwepo Askari anayeitwa Kingai kama alikwepo Askari yupi aliyehusika Kwenye eneo la Ukamataji Kwa Siku hiyo

Shahidi:
sikumzungumzia kwa sababu Sikuulizwa ni Askari gani aliyekamata anajibu Kwa Sauti ya Chini sana

Wakili wa Serikali:
Mheshimiwa Jaji naomba Tukomee hapa

Jaji: Shahidi Nashukuru kwa Ushahidi Wako

Wakili wa Serikali:
Mheshimiwa Jaji tunaomba Hairisho Mpaka Kesho Saa 03 Asubuhi ambapo tutaendelea na Shahidi Mwingine
Upande wa Mashitaka

Kibatala: Mheshimiwa hatuna Pingamizi

Jaji anaandika Kidogo

Jaji :
basi Maombi ya hairisho yanakubaliwa hadi Kesho saa 03 Asubuhi Upande wa Mashitaka Maelekezo ni kwamba Mtatakikwa mlete shahidi Na Washitakiwa wataendelea Kuwa Rumande Mpaka Kesho saa 3 Asubuhi

Jaji anatoka
 
Naweka kambi hapa....
giphy.gif
 
Kumekucha tena, usiku wa deni ... !! Tunamsubiri shahidi numberi 4.
Mungu mkubwa atamshindia Mbowe katika kesi hii.....Asante mkuu Replica kwa taarifa na update toka Mahakamani

Habakuki 1:4​

Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu inayotolewa huwa imepotoshwa.
 
Namsubiri Shahidi wa 4, sijui ni Ijiipiii....
Hata mimi namsubiri kwa shauku kubwa kabisa. Wengine tunaifuatilia hii kesi kama vile tupo mahakamani kabisa.

Sikuamini yule shahidi wa tatu aliyekuwa akijidai ni mtaalam msomi, alipoulizwa mara mbili kuwa terrorism ni nini na yeye kujibu ni masuala ya utalii!😂🤦🏾‍♂️

Pia pale walipotumia neno terrorist, “conspiracy to terrorist”, ilitakiwa watumie neno terrorism. Kuna vya kusikitisha, maajabu ya kushangaza, pamoja na vya kuchekesha haswa.

All in all, maisha ya wengine kina Mbowe yako kwenye msitari.
 
Sikuamini yule shahidi wa tatu aliyekuwa akijidai ni mtaalam msomi, alipoulizwa mara mbili kuwa terrorism ni nini na yeye kujibu ni masuala ya utalii!😂🤦🏾‍♂️
ina maana alifanya uchunguzi wote ule kumbe alijua ni wa mambo ya utalii 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Leo sijui kuna sarakasi zipi zitakazojiri. Hii nchi haiishiwi vituko. Mara Utalii mara terrorist, mara tourist. Mhh. Ngoja tusikie
 
Kumekucha tena, usiku wa deni ... !! Tunamsubiri shahidi numberi 4.

Habakuki 1:4​

Kwa sababu hiyo sheria imelegea, wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo hukumu inayotolewa huwa imepotoshwa.
Neno la bwana liimidiwe🙏🙏
 
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii Kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa ni kweli, kweli tupu Eeeh Mungu nisaidie
Hapa ndipo kwenye shida, maana imeandikwa !!


Kut 20:7​

Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
 
Back
Top Bottom