Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Nasikia huko dimani znz hali sio nzuri kwa wale rangi ya kabeji.
Nasikia wanacheza rafu mtindo mmoja huku wakibwebwa na yule refa wao"Polisi"
Ebu mliopo huko tupeni taarifa kamili?
 
Hadi sasa ni machafuko matupu, mawakala wa CUF wametolewa kwenye vyumba vya kupiga kura kwa makosa haya;
(a). Wamegundua baadhi ya masanduku yamejazwa kura ambazo zimeshatatiwa tiki kwa mbunge wa CCM.
(b). Wamegundua kuwa kuna watu hawamo ndani ya daftari la kupiga kura ila wamekuja kupiga kura na walipo pinga ndipo POLISI walivyoamua kuwatoa.
(c) Chumba numba 6 imegundilika kwamba masunduku yote yamejazwa kura.
(d) Mazombi wameanza kupiga watu maeneo ya Fuoni kituo cha Kibondeni
(e) Katika kituo hicho cha Fuoni mabasi yamekua yakisomba watu na kuwaleta kupiga kura. Watu hao si wakazi wa jimbo la Dimani. Picha hapo chini inaonesha moja ya mabasi yanayotumika kusomba watu na kuwapeleka vituoni kupiga kura.
Chanzo; # Hababi_CUF
picha zi wapi?
 
Hawa haramu hawa siku zinakuja na muda utasema labda watawale milele kama wanauwezo
 
Hivi kwanini ccm hawana utu kabisa. Yani kweli Mtu akizoea kula nyama ya binadam hatoacha aslan.
Yani kwao goli la mkono ni moja ya Sera na mbinu yao ya ushindi kila chaguzi.
 
Haya niliyategemea sana.Hivyo Siwezi kushangazwa nayo ila NEC ndiyo ya kulaumiwa na Wapinzani Wenyewe hawachulii issue ya Uchaguzi kama sensitive issue.
 
hata kama wa2mie ccmpolisi dimani nikichapo tu coz WAZANZIBARI co akina duhu tabu na amini hata hao kwa awam hii wanataka mabadiliko ,
 
Kila siku tunawaambia dawa ni kudai tume huru otherwise tutakalia kulalamika tu haya maccm ni makatili mno hayana mishipa ya aibu,
 
Wapinzani wakisusia uchaguzi kama shinikizo la kudai uhuru na uhaki katika kupiga, kuhesabu na kutangaza matokeo kina zitto kabwe wanaingia kwenye uchaguzi na kuvuruga mpango mzima.
 
Haya niliyategemea sana.Hivyo Siwezi kushangazwa nayo ila NEC ndiyo ya kulaumiwa na Wapinzani Wenyewe hawachulii issue ya Uchaguzi kama sensitive issue.
Wakati mwingine zile hatua wanazochukua watu wanaoonewa na kunyanyaswa kwa kusababisha damu ina mwagika kumbe sio dhambi. Kenya ilikuwa hivyo lakini sasa wanaheshimiana hakuna mjinga awezaye kufanya mambo ya hovyo namna hiyo kabla hawajamkamua tumbo!
Ulofa ukizidi kila mtu mjinga atakudharau akidhani yeye ni mjanja.
 
Wakala wa chadema aliyepo Kituo cha uchaguzi kijichi B Mh. CCaro Kazinza kakamatwa na polisi, na kituoni kwake hakuna wakala kwa sasa. Wakala wa akiba dada Salma Sharif alitaka kwenda kusimamia lkn naye amefukuzwa. Watu katika eneo hilo wanakimbizwa na kukamatwa ovyo. Katika pitapita yangu nimekutana na watu ambao wanasadikiwa kuwa ni wana CCM walikuwa wakisema hawatakubali kushindwa kwani watatumia hata goli la mkono.

Haya waangalizi na washabiki wa demokrasia tunaomba mliangalie hili kwa jicho la pekee. Kwani huu ni uchaguzi mdogo tu wa udiwani, je wa ubunge na urais itakuwaje?
 
Back
Top Bottom