Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Ijumaa Tarehe 21 Machi 2014 - Hotuba ya Rais, Uzinduzi wa Bunge Maalum

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Habari wadau wote wa JamiiForums. Naamini kwamba hamjambo na Mwenyezi Mungu, muweza wa kila kitu amewajaalia kuamka salama. Kwa wale ambao kwa bahati mbaya siku ya leo wameamka vibaya kutokana na maradhi au sababu nyingine, basi tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wawe na subira.

Pia tuwaombee wagonjwa wote wapone ili waungane nasi kuweza kufuatilia yanayojiri bungeni leo jioni. Pia kwa wale waliofikwa na mauti, basi tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu ili wawe na makazi bora huko Akhera. Pia tuwaombee wafiwa wote wawe na utulivu na subira katika kipindi hiki kigumu

Wadau, kama tulivyotangaziwa juzi na jana kwamba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Kikwete, leo atazindua Bunge Maalum la Katiba hapa Dodoma kuanzia saa 10 kamili jioni. Katika uzinduzi huo, Rais Kikwete ataambatana na ujumbe mzito kwani kutakuwa na Marais Wastaafu wa pande mbili za Muungano, wake wa waasisi wa taifa, na mawaziri wakuu wastaafu.

Wanaotarajiwa kuwemo kwenye msafara huo ni Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Dr Salmin Amour, Aman Abeid Karume, Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume. wengine ni Jaji Joseph Sinde Warioba, Cleopa Msuya, John Malecela, Dr Salim Ahmed Salim, Friedereck Sumaye na Edward Lowasa. Mbali na viongozi hao, pia Rais Kikwete ataambatana na Rais wa Zanzibar, Mr Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Seif Sharif Hamad na viongozi wengine ambao ni wajumbe wa bunge la katiba.

Pia kutakuwa na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii, wawakilishi wa mashirika ya kitaifa na kimataifa, mabalozi wa nchi mbalimbali na wengineo.

Imeripotiwa kuwa viongozi wakuu wa vyama vya Upinzani, Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wamepongeza uamuzi huo wa Rais kuambatana na msafara huo. Pia wamewaomba wabunge wenzao hasa wa upinzani kuonesha hali ya utulivu wakati wote wa tukio hilo muhimu la kihistoria.

Nasi kama kawaida yetu tutawaletea kila kinachojiri wakati wa tukio hilo. Niwaombe pia wadau woote wa JF ambao tumekuwa pamoja tangu tulipoanza utaratibu huu kushiriki kwenye mjadala huu.

------------------------
Kilichojiri Bungeni
------------------------

- Wabunge wanaingia kwa wingi ukumbini. Naona leo hali ya mahudhurio imekuwa nzuri
- Kwa mujibu wa Ratiba ni kwamba kikao cha abunge kilipaswa kuanza saa 9.10. Ila ratiba itachelewa kidogo.mwageni waliofika ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji Mkuu wa Tanzania na Zanzibar
- Mzee Karume naye yupo nje ya viwanja vya bunge
- Naam namuona Mheshimiwa Freeman Mbowe anawasili na sasa anateta jambo na James Mbatia
- Naam, kule nje namuona Makamu wa Rais, Gharib Bilal
- Hakika ukumbi wa Bunge umependeza sana leo. Wabunge wengi wamejitokeza na kuna wageni wengi pia
- Naaam sasa Rais JK anaingia Ukumbini kwa kupitia ule mlango wa VIP
- Mheshimiwa Abeid Amani Karume sasa Anaingia
- Mzee Ruksa, Ali Hassan Mwinyi anaingia sasa
- Jaji Mkuu wa Zanzibar, Jaji Makungu anaingia Bungeni sasa
- Jaji Mkuu, Mohamed Chande aorhman anaingia sasa
- Makamu wa Kwanza wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad anaingia ukumbini
- Anayefuata ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Mohamed Shein
- Anayefuata ni Makamu wa Rais, Dr Mohamed Ghalib Bilal
- Wageni wote muhimu wamewasili na sasa anayesubiriwa ni Mheshimiwa Rais kuingia Bungeni
- Naam mzee wa Speed and Standard anamsindikiza Rais JK kuingia ukumbini. Mayowe yanapigwa kuashiria furaha ya wabunge. Namuona mheshimiwa mnyaa anapiga meza muda wote
- Mzee Malecela naye yumo. Pia kuna Pius Msekwa, mama Maria Nyerere na wake za viongozi


============================
HOTUBA YA RAIS KIKWETE (KWA UFUPI):
============================

Jakaya Kikwete said:
- Wajumbe mhakikishe mnatunga Katiba itakayodumisha Muungano wetu

- Tunahitaji Katiba itakayodumisha Amani na Usalama wa nchi yetu!

- Ni mara ya TATU kwa Tanzania kuwa na mchakato wa kutunga Katiba Mpya! 1965, 1977 na sasa 2014!

- Tofauti na awamu zilizopita za michakato ya kutunga Katiba, awamu hii imewahusisha wananchi kwa ukaribu zaidi!

- Mchakato wa sasa utaishia kwenye Kura ya Maoni ili wananchi wachukue maamuzi wenyewe!

- Katiba ya sasa ya Tanzania imefanyiwa mabadiliko kwa takribani mara 14 tokea mwaka 1967!

- Serikali imekuwa tayari kufanya mabadiliko ya Katiba kila ilipoonekana kuwepo uhitaji wa kufanya hivyo!

- Wapo watu walioifananisha Katiba yetu na nguo yenye viraka vingiiiii

- Wapo waliodai kuwa 'Tukipata Katiba Mpya tutaiondoa CCM Madarakani'

- Madai ya Katiba Mpya yaliibuka baada ya kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi Tanzania

- Mwaka 2010 mwezi Disemba nilisema 'Tutazindua Mchakato wa kupata Katiba Mpya'

- Mchakato wa Katiba Mpya utahitimishwa kwa wananchi kupiga Kura ya Maoni ili kuikubali au kuikataa Katiba Mpya!

- Kitendo cha Warioba kuwasilisha Rasimu mbele ya Bunge kinahitimisha rasmi kazi ya Tume. Kazi inayofuatia ni ya Bunge!

- Niliwaagiza Tume kuiweka Rasimu ya Katiba Mpya kwenye Tovuti ili wananchi waweze kusoma na kutoa maoni yao!

- Nawapongeza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kazi nzuri waliyoifanya. Haikuwa kazi rahisi

- Tume ya Mabadiliko ya Katiba imepokea maoni 772,211 toka kwa wananchi na kuyafanyia uchambuzi wa kina!

- Tume imefanya kazi nzuri, yenye manufaa kwa watanzania. Rasimu imeandikwa vizuri na mapendekezo yanayofaa!

- Rasimu ya Katiba ni kitabu chenye kurasa 106, sura 17 & Ibara 271. Wajumbe wa Bunge msome na kuelewa kila kilichoandikwa!

- Ni vema wajumbe wafanye uamuzi wenyewe sio wa kuambiwa na wenzao! [Akiwataka wasipelekeshwe]

- Wajumbe mjiridhishe na vifungu vyote kama vimeandikwa sawa; dhana zilizomo kwenye rasimu. Ni dhamana mliyopewa

- Tunachotaka watanzania ni KATIBA BORA! Msipofanya hivyo, kuna hatari ya kupata Katiba isiyotekelezeka!

- Bunge Maalum la Katiba lina wajibu wa kuliepusha Taifa na ulazima wa kufanya mabadiliko ya Katiba baada ya kutungwa!

- Yapo mambo mengi kwenye Rasimu Katiba ambayo yanahitaji wajumbe kueleweshwa ili waweze kufanya maamuzi sahihi

- Huwezi kudai PEPO ambayo huna uwezo nayo! Lakini kujipa matumaini ya Pepo ambayo huna uwezo nayo ndio uungwana...

- Ibara ya Pili ya Rasimu ya Katiba inayohusu MIPAKA ya nchi ina maelezo mazuri lakini haijagusia MAZIWA na MITO!

- Kama asemavyo Mtikila "Wakati wenyewe ndio huu!" (akiongelea mipaka ya nchi kuhusisha maziwa na mito)

- Mfumo wa Serikali 3 unaopendekezwa na Tume; mambo yanayohusu uchumi yapo chini ya mamlaka ya serikali za nchi husika!

- Suala la Kilimo na Pembejeo katika Rasimu ya Katiba kuachwa bila kutolewa ufafanuzi kwny Serikali 3 yataleta migongano

- Akili za kuambiwa, changanya na za kwako! #KatibaMpya ;)

- Kama wajumbe mkiamua kuendelea na serikali mbili, bado mambo yaliyopendekezwa na Tume yanatekelezeka bila tabu!

- Katika uandishi wa Rasimu, orodha ya Mambo ya Muungano suala la Utumishi halikuelezwa kama suala la Muungano!

- Katika Rasimu hii kuna mambo mapya ambayo yanabadili namna ya uendeshaji wa Serikali. Wajumbe muangalie kama yanafaa

- Ibara ya 128, ibara ndogo ya pili D. "Mbunge kuweza kupoteza ubunge endapo atashindwa kufanya kazi ya ubunge kwa miezi 6" iangaliwe

- Mbunge kuugua miezi 6 mfululizo na akapoteza nafasi yake ni kama ukatili wa hali ya juu!

- Itumiwe hekima kuviangalia vifungu kadhaa vyenye kuwa na matatizo na vinavyoweza kupelekea usumbufu usio na sababu

- Dhana ya Ukomo wa vipindi vitatu kwa Ubunge (tena bila kusema ni kwa mfululizo) nayo inahitaji kuangaliwa vema.

- Ni vema kuwa na ukomo kwa urais (akisema mtu anaweza kuigeuza nchi shamba), lakini ukomo kwa wabunge uangaliwe vema

- Dhana ya kwamba mbunge aliyepoteza nafasi yake chama chake ndicho kijaze nafasi yake iangaliwe kwa umakini isilete misuguano!

- Dhana ya Mawaziri kutokuwa wabunge ni nzuri lakini inahitaji kuangaliwa kwa umakini!

- Suala lililovuta hisia za watanzania wengi ni suala la Muungano wa Tanzania. Serikali 2 au Serikali 3!

- Nawaomba wajumbe mnapojadili aina ya Muungano unaofaa Tanzania muwe watulivu! Epukeni jazba!

- Madai ya Serikali Tatu si jambo jipya! Mwaka 1984 ilikuwa hoja iliyopelekea machafuko huko Zanzibar.

- Suala la Serikali Tatu Wajumbe mlizungumze limalizike. Kama zinakubaliwa, zikubaliwe; kama kukataliwa ijulikane!

- Kuna rai zinatolewa kuwa kwenye mjadala wa aina ya Muungano yasitumiwe majina ya Nyerere/Karume! Nadhani si sahihi

- Tume imedai Muundo wa Serikali 3 ndiyo matakwa ya watanzania walio wengi na imetoa sababu zake!

- Wapo wanaodai kuwa Takwimu za Tume yenyewe hazionyeshi ukweli kuwa watanzania wengi wanataka muungano wa serikali tatu!

- Inadaiwa kuwa 86.4% ya watanzania waliohojiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba hawakuwa na tatizo na muundo wa Muungano!

- Inadaiwa katika maoni yote ya Tume, ni 10.4% iliyoongelea muundo wa Muungano!

- Kuhusu usahihi wa hoja za wanaoikosoa Tume ya Mabadiliko ya Katiba juu ya aina ya Muungano, nawaachia wajumbe!

- Wapo wanaolalamika kuwa Zanzibar ina bendera yake, Katiba yake, Wimbo wake n,k

- Nimeeleza niliyoeleza kwa muhtasari; ninyi wajumbe ndio mna maamuzi juu ya aina ya muundo wa Serikali unaotufaa!

- Kuhusu muundo wa Serikali Tatu, Jaji Warioba alitutoa hofu kuwa "Gharama si kubwa sana za kutisha!"

- Wajumbe mjipe nafasi ya kulitafakari kwa undani suala la aina ya Muundo wa Muungano wa #Tanzania

- Katika kujadili kwenu wajumbe, mtafute majibu muafaka ya matatizo yanayoweza kutokana na Muundo wa serikali tatu!

- Muundo wa Serikali tatu hautapunguza matatizo bali utaongeza matatizo kuliko ya sasa!

- Wapo wanaotaka Tanzania iingie OIC, wakisema kama Bara haitaki basi Zanzibar iachwe iingie...

- Wapo wanaotaka Zanzibar ijiunge na Umoja wa visiwa vya Bahari ya Hindi ili wanufaike huko, lakini wanaona wanabaniwa!

- Serikali zetu mbili zikiamua kuwa zinataka kutatua kero kubwa tatu za Muungano zilizobakia, zinatatulika!

- Kuna Mtanzania alitumia SMS akidai nimekula njama na Warioba na tunawatumia wapinzani kujiongezea muda hadi 2018!

- Serikali zetu mbili hazina kigugumizi cha kupunguza kero zinazoweza kupunguzika. Hakuna mwenye hila wala dhamira mbaya!

- Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964; mambo 11 ndiyo yalikuwa ya Muungano (kayataja)!

- Mwaka 1968 suala la mafuta, petroli na gesi asilia liliwekwa rasmi kwenye masuala ya muungano!

- Mwaka 1973 Baraza la Mitihani la Taifa liliingizwa kwenye orodha ya mambo ya Muungano

- Mwaka 1992 tulikubaliana kuwa Vyama vya Siasa viwe vya kitaifa, suala hilo likaingizwa kwny Orodha ya Mambo ya Muungano

- Tulikubaliana (Kikwete na Karume Jr) kuwa suala la Mafuta na Gesi asilia liondolewe kwenye mambo ya Muungano...

- Sisi kama CCM tunaweza kufanya mabadiliko muhimu katika Muungano bila kuhitaji serikali ya tatu!

- Mkitaka serikali tatu, ni lazima mtengeneze mazingira! Serikali ya Tatu ijulikane chanzo cha mapato yake.

- Hapa tunatengeneza nchi yetu, tutengeneze kitu kilicho thabiti!

- Serikali ya Muungano (katika serikali 3) inategemea majeshi ya Tanganyika na yale ya Zanzibar!

- Endapo majeshi ya Tanganyika na ya Zanzibar yakiigomea Serikali ya Muungano utekelezaji wa shughuli utakuwaje?

- Serikali ya tatu (ya Muungano) ni vigumu kukopesheka! Labda idhaminiwe na Tanganyika...

- Hata wanaopenda serikali tatu natambua wanapenda serikali iwe na nguvu. Lazima tujue changamoto zitakabiliwaje!

- Ningependa kama mnaamua tuwe na serikali tatu, basi ziwe tatu zinazosimama na thabiti!

- Watanzania zaidi ya 90% wamezaliwa baada ya 1964!

- Ikishatengenezwa Tanganyika, masharti yataibuka! Watu wataanza kuwa wageni... Watakaotoka upande wa pili wa Muungano

- Ikishazaliwa Tanganyika, chuki za Utaifa zinaweza kuanza; na zitatufikisha pabaya!

- Hata Tume ya Mabadiliko hawana majawabu ya uhakika juu ya kero zitakazotokana na serikali tatu!

- Kama mnaamua tuuvunje Muungano, vunjeni lakini si wakati nikiwepo!

- Kuna kiongozi mmoja wa dini aliniuliza, "Serikali 2 zikiwa na matatizo, dawa ni kuongeza ya 3?"

- Kazi iliyo mbele yenu wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ni nzito. Hatma ya nchi yetu ipo mikononi mwenu!

- Pandu Kificho akiwa Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalum la Katiba alifanya kazi kubwa na nzuri!

- Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba walitumia muda mrefu kwa hatua ya kwanza, ni vema wajitahidi kuongeza kasi sasa!

- Hatua ya awali ya Bunge Maalum la Katiba iliwakwaza wananchi; natumaini kuanzia sasa hayatarudia yale yaliyotokea!

- Nawaomba wajumbe wote kauli mbiu iwe #TanzaniaKwanza! Misimamo inayobomoa, ikiwa ya vyama au vikundi haina maana...

- Kura za NDIYOOO au SIYOOO hazitakuwa na nafasi; zipigwe kura. Ziwe za siri au wazi, hilo nawaachia!

- Katiba Mpya inaewezekana! Timiza wajibu wako...! Mungu ibariki Tanzania

Kwa Hotuba kamili, tembelea - FikraPevu
 
Kila mtu anajua kinachoaendelea na kinachokusudiwa kutokea leo bungeni, naomba kwa pamoja tumshauri JK asijeakathubutu kumjibu Warioba kama wengi wanavyotarajia na kama ikibidi afanye hivyo basi ASITUMIE LUGHA YA KEJELI tulioyiozea,
Jaji alikuja na FACTS kwahio na yeye aje na facts sio kuja na vichekesho na hadithi za Mbayuwayu, msimamo wake leo utamjengea heshima daima au utamondolea heshima kamwe!!!.

Kama hana facts nashauri asingumzie kabisa mambo ya Jaji Warioba.....
 
Pamoja Chabruma "Waasisi wa muungano walituachia Serekali mbili nchi moja,Sasa kuna Serekali mbili nchi mbili" -Warioba.
Pamoja sana Mkuu. Hilo suala la Muungano hakika ni kaa la Moto. Wengine wanataka turekebishe matatizo yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na hilo ulilosema ili tuboreshe muungano uliopo wakati wngine wakitaka tuende kwenye mfumo mpya kabisa.
 
Sijui ni ushamba wa siasa ama ndiyo kutokufuatilia mambo ya siasa ama la, binafsi napenda sana kufuatilia habari za siasa japo sio kiundani sana na wala sina elimu ya mambo ya siasa. Kuna hili jambo ambalo ndiyo habari ya sasa kwa watanzania wote kuhusu suala la kuunda katiba mpya. Kitu ambacho ndiyo kimekuwa gumzo zaidi na kulifanya bunge maalumu la katiba mpya`kuwa na msisimko wa kipekee ni hili suala la muundo mpya wa serikali ambapo kuna baadhi ya makundi wanahitaji muundo wa serikali mbili na baadhi ya makundi wanahitaji muundo wa serikali tatu na hata wachache ingawa sina uhakika wanahitaji kuvunjika kabisa kwa muungano.

Sasa kitu ambacho kinanipa utata mpaka najihisi kuwa ni mshamba wa siasa ni hizi tetesi ninazozisikia kutoa vyanzo mbalimbali vya habari na kwenye baadhi ya vijiwe ni kwamba chama cha CCM kinapigania muundo wa serikali mbili uendelee na baadhi ya vyama vya upinzani na wadau wengine wao kwa namna moja ama nyingine wanata muundo wa serikali tatu

Je, kama kuna ukweli ndani yake kwa hizo tetesi ni kwanini CCM wanapigania muundo wa sasa uendelee kama ulivyo na pia kwanini baadhi ya wapinzani wanahitaji muundo mpya wa serikali tatu ?. Naomba wenye uelewa wa haya mambo wanisaidie kunielewesha kidogo kuhusiana na hili jambo maana mie nimeshindwa kabisa kuelewa.

Ahsante na nawasilisha
 
Kikwete akigusia serikali mbili atakuwa anajiaibisha aka kujivua nguo
Mkuu, Rais ni kama Mwamuzi wa Mpira wa Miguu au msuluhishi kwenye mgogoro. Sidhani kama atakuwa na mtazamo wa kulazimisha muundo huo. Naamini kwa vile ndani ya chama, CCM wameshaweka msimamo wao, Rais hawezi kabisa kulazimisha watu. Anajua chama chake kina wabunge wenye akili na watetezi wa serikali mbili. Anajua pia kuwa bunge ndilo lenye mamlaka ya kuamua aina ya muungano lna wala si JK au Warioba.
 
Hizo ni nyufa zilizotokana na mtikisiko hivyo jawabu lake siyo lazima kukimbilia serikali tatu, na kufanya hivyo tutakuwa tumeshindwa kuutetea muungano na kuulinda, tuna mambo mengi yanayohitajika yakijadiliwa kwa kina na wajumbe wa katiba na kupatiwa ufumbuzi yatatupeleka mbele kuliko hata hoja ya serikali tatu.

Watanzania tusivyofikiri kwa kina tunapigania na kuunga mkono katiba iliyojaa Mgawanyo wa vyeo na madaraka tuu na kuacha mambo ya msingi, unapoongelea serikali tatu huko ni kujaza madaraka tuu na matokaeo yake ndio kupanda kwa ghalama ambazo zitapelekea kuongezeka kwa kodi, Maana rasimu hii imetaja utitiri wa tume ambazo hazina maana katika nchi hii.

Katiba ni tendo la maridhiano na kuaminiana sasa kama hakuna dhamira hii sidhani yote haya yaliyoandikwa mle yatakuwa na maana au ufanisi katika utekerezaji wake. Mm nashauri wajumbe tutengeneze katiba ya Wananchi cyo katiba yenye mlengo wa kuondoa ama kuua chama chochote kiwe cha upinzani ama tawala ama kikundi chochote kilichopo kwa mujibu wa sheria na katiba, tuangalie katiba itakayo tutoa hapa tulipo na kutupeleka mbele zaidi kwa kasi. Kwa kuaminiana na kuheshimina tutapata katiba bora.
 
Pamoja
Chabruma
"Waasisi wa muungano walituachia Serekali mbili nchi moja,Sasa kuna
Serekali mbili nchi mbili" -Warioba.

Asante kwa kufungua mjadala kwa quate murua kabisa toka kwa gwiji wa sheria na kipenzi cha wananch kwa sasa ubarikiwe sana hii inaonyesha wazi kuwa mjadala umepata baraka toka kwa mtu alie tufanya tuwepo hapa(WARIOBA) Mungu amzidishie afya na amwongeze miaka mingi ya kuishi kadiri ya mapenzi yake.!
 
Wakuu heshima kwenu,binafsi bado sijajua kwa uhakika like ambacho kinakwenda kufanywa na mkuu wa kaya. Anakwenda kujibu hoja za time ya warioba au anaenda kuzindua Bunge maalum la Katiba!? Nimetishwa sana na war aka wa ccm,ambao umetolewa masaa machache tu baada ya hotuba ya kusisimua ya jaji Joseph Warioba. Km huo ndo msimamo wa ccm,mwenyekiti wake atashindwa kuitetea ajenda yao mbele ya wajumbe.!?? Au ndo maana waliamua kumtanguliza warioba!?
 
Back
Top Bottom