Yaani mwanangu umenilaza chooni!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Jamaa mmoja alimpokea baba yake kutoka kijijini.Baba yake toka kuzaliwa hakuwahi tia mguu mjini.Jamaa alikuwa akiishi mjini katika chumba kimoja na mkewe na mtoto wao mmoja hivyo ikawa vigumu kumpokea mzee nyumbani.Kuona hivyo jamaa akamtafutia chumba guest,kizuri kabisa{self contained} kila kitu mpaka choo ndani.Mzee hakulijua hilo mpaka alipodiriki kufungua mlango wa pili wa kile chumba na kukumbana na tundu la choo.Mzee kwa hasira alichukua mizigo yote na kwenda kulala reception.Jamaa alipofika asubuhi alimkuta mzee analia kwa uchungu huku analalama;'yaani mwanangu wa kumzaa mwenyewe unanilaza chooni!',haina shida mi nipe nauli nirudi kwa mama yako kijijini,mi sio babako tena!
 
Back
Top Bottom