Je hii ni sawa?

Zombie S2KIZZY

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
823
1,613
Wakuu inakuaje,

Tano ni moja au moja ni Tano?

Anyway,

Kuna Dogo mmoja ni msela wangu sana mambo mengi sana tunashirikiana, Sasa bhana Dogo alkua mkoa X ambapo ndio kwao kabisa , Dogo akanambia oya nakuja huku dar, nataka nije nikajifunze kitu flani kwenye chuo flani cha hayo mambo flani, nikamwambia oky karibu man.

Nikamshirikisha waifu hakupinga akabless, Dogo akaanza safari na hatimae akafika tukaenda Mimi, waifu, na mwanangu kwenda kumpokea mwanangu mwingine ingawa sio mwanangu wa kumzaa Ila ni mwanangu wa kitaa.

Nikamkaribisha home,tukala, stor stor nyingi ,nikamuonesha chumba chake akapumzike. Jamaa akaanza kwenda chuoni anarud home amani ,tunakula ,hakuna noma ,siku inaisha.

Muda wa chuo ni saa tisa mchana.

Hadi saa kumi na mbili jioni.

Sasa kipengele kinaanzia hapa, juzi kaenda chuo,Mara ghfla mida ya saa kumi ananitext "oy nakuja kuchukua begi langu,nimekutana na mjukuu wa bibi kizaa mama".

Nikamjibu "shega tu utanikuta sababu Leo sijaenda studio Niko home tu ".

Bahat mbaya nkapata dharura studio ikabidi nirudi sinza, Ila nikawa nmeisha muelekeza waifu Kila kitu ,
So jamaa alivyorudi akachukua begi lake then akasepa usiku huohuo.

Baadae nikampigia nikamuuliza "oya mbona umetoka usiku hivi kama umefukuzwa man ,Kwan usingetoka kesho mapema ili hata nikuzingatie moja mbili za kutumia tumia huko unapoenda?"

Jamaa akasema"Aaah! Huyu jamaa mjukuu wa bibi mtoto wa mamdogo alkuwa ananiwahisha"
Nikamuuliza "vipi home mkoa X wanajua umeondoka Hapa kwangu na unaenda wapi?"

Jamaa akajibu "eeh wanajua,Ila nitarudi tu man,nikianza field"

Nikasema "sawa,kukiwa na shida yoyote nipigie au njoo home"

Tukaishia hivyo,

Leo kanicheki akasema alisahau viatu huku ataviijia ,

Nikamwambia "njoo ulale huku alafu jtatu unasepa"

Akasema "aaah ooh ntakuja tu jtatu asubuhi kuchukua viatu then narud huku kwa msela"

Nikamwambia basi poa man,

Nikawa na wasiwasi na huyu Dogo nikaamua niwapigie kwao mkoa X ,nkampigia bi mkubwa ake, nikamuuliza taarifa za dogo lakini akasema hajamwambia chochote.

Na pia huku dar hawana ndugu yoyote ,Duuh!

Sasa wakuu wa JamiiForums, nifanye nini hapo kuhusu huyu Dogo, kwa maana kwao wanajua Dogo yuko kwangu ,kwahiyo litakalomkuta nitaulizwa Mimi sababu wanajua yuko kwangu na msala utakua kwangu,
na Dogo akiulizwa anasema yuko kwangu, na kumbe hayupo kwangu.

Sijui yupo kwa machangu? Na kinachonichanganya kama alikua na sehemu nyingine ya kwenda,
Si angesema kwao kwamba kuna sehem anaenda, wala isingekuwa ajenda kuliko alipoamua kwenda,
Kmy kmy kama mwenda, zake?
 
Shida mingine mnajitafutia asee tatizo linapita kuleee unalikimbilia umelipata lakini bado halikutaki we unaling'ang'ania tu ushaongea na kwao bado watakaje chief huruma inapaswa kuwa na kiwango kinachofata utapigwa tukio nyumbani kwako
 
Wewe usha waambia kwao kuwa katoka hayupo kwako. Acha kumpa umuhimu mti asie kuzingatia. Upo kwako kaja na kaishi afu katoka kwako kama anatoka toilet. Wewe ushawaambia kwao huna lawama na mtu over
 
Shida mingine mnajitafutia asee tatizo linapita kuleee unalikimbilia umelipata lakini bado halikutaki we unaling'ang'ania tu ushaongea na kwao bado watakaje chief huruma inapaswa kuwa na kiwango kinachofata utapigwa tukio nyumbani kwako
Asante mkuu
 
Wazo langu ni Moja mchane dogo ....ww mtu mzimah asikupangie

Pia mbananishe na kwao akija tenah hapo kwako(Yaani unapiga simu kwao na yeye akiwepo) .....watu wanasema usijipe umuhimu kwasababu ushaongea na kwao lakini vuta picha tafsiri halisi ya maisha umeaminika kumsaidia ndugu yetu lakini unamwacha tu aharibike kizembe
 
Back
Top Bottom