Wizi wa CCM Muleba wadhoofisha miundombinu ya wilaya

Mchumba

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
277
261
Chama ambacho kinashindwa kulinda rasilimali za nchi hakifai kuchukua dola. Wakati Chadema tunasema People's Power tunamaanisha nguvu ya umma. Anayeiua Muleba ni CCM hatupaswi kumlaumu yeyote.

Hiki chama kimechooka ni chama ambacho kinashindwa kuisimamia serikali na kujisimamia chenyewe.

Kuna mkandarasi yuko Muleba ambaye anaitwa Josefati Rweyemamu JR miaka yote ndio huchukua tenda za Muleba za kujenga miundombinu mibovu lakini hajawahi kuchukuliwa hatua. Mkandarasi huyo miaka kumi iliyopita Naibu Waziri MH Mwari alimkataa unaweza kuona kwenye link hapo chini.



Mkandarasi huyo kaishika Halmashauri ya wilaya ya Muleba. Wakija wakuu wa wilaya na mikoa wote huwa anawaweka mifukoni hakuna wa kumgusa. Kisa ni Mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa CCM.

Wananchi wa Muleba walilamika juu ya taa hafifu alizofunga barabarani wakiongozwa na vijana wa Chadema. Mkuu wa mkoa baada ya kupata malalamiko alienda kukagua hizo taa.

Kilichotokea Mkuu wa Mkoa naye alilainishwa na siku hiyo mkandarasi aligawa hela kwa wananchi kama njugu ili waseme taa zipo. Na watu walitumiwa hela kwenye simu zao baadhi ya vijana wa Chadema zile hela walizirudisha na ushahidi huo upo.

Baada ya hapo Mkuu wa mkoa naye aliendelea kulalamika na wananchi nao wanalalamika maana kashindwa kufanya hatua zozote. Link ya Mkuu wa mkoa kukagua taa iko chini:

 
Hii issue ipo complicated. Huenda na mkuu wa mkoa kaingizwa chaka. Niliona video wakimpimia kila kitu wanasema kipo sawa na wamezidisha specs zaidi mara mbili. Nikajiuliza. Hizi zama za vitu kuwa ghari hivi, inawezekanaje mkandalas akazidisha specs alaf apate faida. Specs za Taneps kupitia tarura hizi hapa. WanaMuleba wanataka wapime hatua kwa hatua waone kama tender ya taa imeenda kiharali
 

Attachments

  • Screenshot_20230311-221652_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20230311-221652_WhatsApp.jpg
    61.1 KB · Views: 4
Mkandarasi ni Muhaya mwenzenu.

Msikilizeni vizuri Chalamila atawasaidia. Acheni majungu, fitina na majivuno.
 
Back
Top Bottom