Wizi mtandao wa Vodacom

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
11,157
29,166
Wadau poleni na majukumu ya kila siku.
Kampeni hii ni maalumu kabisa ili kuweza kumwokoa Mtanzania anayeibiwa na kampuni hii ya mawasiliano inayowaibia wananchi mchana kweupe kabisa wizi wao ni huu, ukiweka salio labda 500 kabla haujajiunga wanakata kama shilingi 20 hadi 40 , unaweza kuweka pesa ili ujiunge na Kifurushi halafu pesa ipo wanakueleza haitoshi lakini pia kukuunganisha na huduma zao za kulipia kwa lazima bila hiyari yako hivyo tuwahamasishe ndugu zetu wahame hii Kampuni hawana adabu kwa wateja wao.
 
Huduma zao kwa wateja ni mbovu sana na unaweza piga simu isipatikane na hata ikipatikana wanakujibu wanavojisikia wao
 
Wizi mwingine ni wao kupunguza pesa kwenye M PESA bila ridhaa ya mteja hivo lazima mpaze sauti na wizi wa hawa matapeli msiumie tu moyoni wahameni
 
Sijutii kuwa mteja wa kampuni yoyote ya simu Tanzania,HASAHASA VODACOM

Hayo matatizo munayapata kwa kutokuwa makini.

Mods futa hizi pumba muende ofisini kwao si mnapajua, mumetuchosha Arrghh
 
Mi niliishalalamika kwa kuandika email TCRA baada ya vodacom kuniibia laki moja ndani ya masaa 24. Sikuwahi kujibiwa email yangu nikajua hii ni kampuni ya "wakubwa". Watakuja mwakani kuomba kura zako uwape urahisi.

Ilitakiwa fedha yoyote tunayokatwa na vodacom kwa sababu zozote lazima ije na notification au niulizwe kwanza but wao wanakata bila ridhaa ya mwenye fedha, huo ni wizi
 
Voda ni wezi wakupindukia nikwambie yaani mie ndo nilihama kitaaambo sana yaani wanakuwekea mihuduma yao hata hujaitisha ukiweka pesa unaambiwa haitoshi washenzi sana hawa Voda. Tigo wanaudhi na sms nyiiingi za kudaiwa lakini si wezi kama Voda
 
Sijutii kuwa mteja wa kampuni yoyote ya simu Tanzania,HASAHASA VODACOM

Hayo matatizo munayapata kwa kutokuwa makini.

Mods futa hizi pumba muende ofisini kwao si mnapajua, mumetuchosha Arrghh

Kunyamaza ni busara sana........
 
Voda ni wezi wakupindukia nikwambie yaani mie ndo nilihama kitaaambo sana yaani wanakuwekea mihuduma yao hata hujaitisha ukiweka pesa unaambiwa haitoshi washenzi sana hawa Voda. Tigo wanaudhi na sms nyiiingi za kudaiwa lakini si wezi kama Voda

Ht mm nimehama rasmi tangu juzi na niko kwenye kampeni ya kushawishi watu wengine 10 wahame na hd sasa nimeshafanikiwa kwa watu 6.
 
Ni kweli hawa jamaa ni wezi sana, hata kwenye vifurush vya internet. Ukiwa na MB100 na unatumia smartphone utashangaa ndani ya dakika 5 wanakutumia msg eti kifurush kimeisha! Mbona wenzao Tigo na Airtel ukiwa na MB100 unatumia mda mrefu??
 
Wadau poleni na majukumu ya kila siku.
Kampeni hii ni maalumu kabisa ili kuweza kumwokoa Mtanzania anayeibiwa na kampuni hii ya mawasiliano inayowaibia wananchi mchana kweupe kabisa wizi wao ni huu, ukiweka salio labda 500 kabla haujajiunga wanakata kama shilingi 20 hadi 40 , unaweza kuweka pesa ili ujiunge na Kifurushi halafu pesa ipo wanakueleza haitoshi lakini pia kukuunganisha na huduma zao za kulipia kwa lazima bila hiyari yako hivyo tuwahamasishe ndugu zetu wahame hii Kampuni hawana adabu kwa wateja wao.

Mbona unahamasisha watu waihame kampuni kwani ukihama wewe peke yako utapungukiwa nini? Awali ya yote ni kwamba una papara,umeshawahi kufika katika ofisi za Vodacom ukauliza swali lako? Kabla hujaenda huko fanya hili: Kabla ya kuweka salio hakikisha mobile data iko OFF katika simu yako,inawezekana unapoweka hela huwa zinaanza kuliwa kama Internet Charges. Tafakari kabla ya kuchukua hatua!
 
Exactly! Km unatumia smartphone yoyote hakikisha kabla hujaweka salio ume-SWITCH OFF MOBILE DATA. Ukiacha ON lazima ukatwe tu as internet charges.
 
Hakuna siku utaishinda voda mahakaman,ilo sahau kabisaaa.Ni kampuni iliyojipenyeza kwa njia ya rushwa kubwa kwa wanasiasa ktk nchi za africa.

Wanahuduma nyingi za makato kwa wateja na hazina maana/umuhimu.Udhalim wanaofanya ni kuingia mkataba na kampuni nyingine (third parties) ambazo wateja hawazijui.Hata ukifungua kesi, kampuni zinazotoa huduma hizo kupitia voda ndizo zinazohusika!Mfano ni starfish mobile~wanahusika na kutoa sms za michezo,mapenzi,nyota.NI ZANTEL PEKEE HAITUMII T/PARTIES.
 
Wanakera hawa balaa...nililipia DSTv kupitia huduma yao ya M Pesa. Nikaletewa notification na risit. Kwa mshangao DSTv hela hawajapata. Pamoja na kwenda kwenye ofisi zao mara likuki mpaka danadana. Gharama za kufuatilia nikaona inataka kuzidi premium amount niliolipa DSTv nikaamua kuacha. Wezi wakubwa.
 
Mi niliishalalamika kwa kuandika email TCRA baada ya vodacom kuniibia laki moja ndani ya masaa 24. Sikuwahi kujibiwa email yangu nikajua hii ni kampuni ya "wakubwa". Watakuja mwakani kuomba kura zako uwape urahisi.

Ilitakiwa fedha yoyote tunayokatwa na vodacom kwa sababu zozote lazima ije na notification au niulizwe kwanza but wao wanakata bila ridhaa ya mwenye fedha, huo ni wizi

Kimsingi TCRA ndiyo waliopaswa kuhakikisha wananchi wanatendewa khaki na makampuni ya mawasiliano yaliyosajiliwa na wa na kuhakikisha usalama wa fedha za wateja. Yapo matatizo mawili makubwa; kwanza ni lile la viongozi na familia zao kuwa na hisa katika makampuni haya - kitendo kinachowapa kiburi cha kufanya watakavyo; na pili rushwa wanazotoa kwa viongozi waandamizi wa TCRA zenye matokeo ya kuwadhoofisha wasiwe na hata chembe ya ujasiri wa kuwachukulia hatua!
Izingatiwe kwamba pamoja na dhambi zote makampuni haya hayalipishwi kodi stahiki kwa mapato yao na Vodacom pamoja na kuwa kampuni kubwa ya mawasiliano zaidi ya zote hapa nchini si mojawapo ya walipa kodi 20 bora! Inapitwa hata na kampuni cha ulinzi ya Group 5!
Kisiasa hata ndiyo matokeo ya CCM kufuta Azimio la Arusha lililokataza viongozi kuwa na hisa katika makampuni makubwa na kuruhusu hata maraisi na watendaji wakuu serikali ni kumiliki hisa. Unawezaje kuhoji utendaji mbovu kwenye kampuni ambayo we ye his a ni pamoja na kina Mkapa, Kikwete, Lowasa, Kinana na viongozi kibao toka chama "tawala" cha CCM? Kwa mtaji huu kina Kinana wataendelea kumaliza tembo wetu, Voda kumwibia hata mkulima wa kule Pandagichiza, na nyara na madini kutoroshwa nje. Sasa pekee ni kuwatema vibaka hawa mwakani ili tuanze upya. Vinginevyo tuendelee kuandika maumivu.
 
Sijutii kuwa mteja wa kampuni yoyote ya simu Tanzania,HASAHASA VODACOM

Hayo matatizo munayapata kwa kutokuwa makini.

Mods futa hizi pumba muende ofisini kwao si mnapajua, mumetuchosha Arrghh

utakua na matatizo ya akili sio bure huwezi ukajisifu wakati mamilioni ya watanzania wanaibiwa na Vodacom kila siku na mamlaka zimelala au wanafanya makusudi
 
Watanzania amkeni hakuna uhusiano wa kua online halafu MB zikiisha bado wakate pesa mfano mzuri ni MTN ya Uganda ukiwa online hata kama unatumia SmartPhone hawakati salio la ziasa na huduma ya internet baada ya kuisha bundle wanaisitisha
 
Kwa taarifa ni kua wanakata pesa hadi kwa wanaotumia simu za tochi hawafai tuwahame haraka sana na nashukuru binafsi nimehamisha watumiaji 30 mpaka sasa
 
Mbona unahamasisha watu waihame kampuni kwani ukihama wewe peke yako utapungukiwa nini? Awali ya yote ni kwamba una papara,umeshawahi kufika katika ofisi za Vodacom ukauliza swali lako? Kabla hujaenda huko fanya hili: Kabla ya kuweka salio hakikisha mobile data iko OFF katika simu yako,inawezekana unapoweka hela huwa zinaanza kuliwa kama Internet Charges. Tafakari kabla ya kuchukua hatua!

Mkuu, ukitaka kupoteza siku yako nenda ofisi za Vodacom, wadada wapo busy na smartphone zao wanachat tu pia wakali km pilipili kichaa.

Wa kaka na suruali zao zinazotaka kudondoka, wanajifanya wapo busy na wanajiskia km watu walowin maisha, ukitoa shida yako kuwa umekatwa sh 50/- hakuelewi anaona km vile wa kuja maskin wa kutupa.

Bora tuwapotezee tuu ibaki kuwa story km Kampuni ya Tritel
 
Sijutii kuwa mteja wa kampuni yoyote ya simu Tanzania,HASAHASA VODACOM

Hayo matatizo munayapata kwa kutoekuwa makini.

Mods futa hizi pumba muende ofisini kwao si mnapajua, mumetuchosha Arrghh
Msafara wa kenge hawakosi mijusi,Mwizi anajulikana kwa kauli zake
 
Back
Top Bottom