TCRA tusaidie wizi wa Vodacom

WAZO2010

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,610
3,738
Jamani binafsi kila mara nimekuwa mhanga wa wizi wa Vodacom. Una unga kifurushi cha siku 7 kinaishw ndani ya muda mfupi sana.

Leo nipo safarini, saa 11:05 nika ungq kifurushi cha MB 1480 cha siku 14 kwa Tshs 3000/.

(Binafsi siyo mpenzi sana wa movie wala Youtube). Na nyie ndg zangu ni mashahidi wa hali ya Network uwapo safarini (on road) nchini Tanzania Ni ON/OFF kutokana na mapori na mawimbi safarini.

Hivyo sijatumia ku download video , wala youtube au wala nini? Ni kusoma updates tu blog, pages, nk. Hata link hakuna niliyo fungua.

Ila ilipofika leo hii hii mchana saa 8:01 ikiwa pia nili jiunga leo saa 5:05 asubuhi, Vodacom waka nitumia sms (Habari, MBs za kifurushi cha Ya Kwako Tu zimeisha. Kununua kifurushi kingine tafadhali piga 149*01#.). Nika shangaa. Ikabidi nihakiki kwa kupiga 149*60# (Ndugu J**: Salio Muda wa Maongezi: Akaunti Kuu Tsh 0.24. Kifurushi:dk 756 sek 38 mitandao yote SMS 9995 dk 756 sek 38 mitandao yote mpaka 2023-02-24 12:32:00.
SMS 9995 mpaka 2023-03-16 22:38:11).

Nimechoka na huu wizi wa makusudi.
Nimejaribu kuwapigia Customer Care Vodacom 100 waka nieleza Ujinga tupu! Mara Ohhh umetumia MBs zote, Mara Oohh Voda ina speed sana! Speed ya NYOKO! 2015 hadi 2020 internet ilikuwa vizuri tu. Ila toka 2021 ni Majanga.

Waziri Nape Nauye hana msaada wowote, kazi kuvuta posho tu. Hawa TCRA ndio buree kazi kuvuta rushwa tu.
Dunia ya sasa internet ni kila kitu iwe biashara, utendaji wa Ofisi, Ufanisi wa Mifumo mbalimbali ya taasisi, na Elimu kufikiwa kwa Wepesi. Ila Tz imekuwa tofauti.

Pia nitumie fursa hii kuiomba TISS kuchunguza Uraia wa Wakurugenzi wa Vodacom Tz, Airtel Tz na wengine, huenda ni hujuma kwa Taifa.

TISS na Vyombo vyenu fanyeni Auditing ktk mitandao hii hasa, wizi wa pesa, salio, MBs, dk,nk. Tanzania ilindwe.

Kama TCRA na Waziri mmeshindwa kuiongiza hizi mitandao ya Simu.
Leo ombi langu kwa Mama Samia Suluhu Hassan, chondechonde, kupitia hili dirisha dogo la Maboresho yako ya.

Watendaji tuondolee mizigo wa Mawaziri, Makatibu Wizara ya Habari na Mawasiliano na Mtendaji Mkuu na Katibu wake TCRA.
 
Voda ni 🚮 sema tunaishi nao kibishi..
Tar 10 nilikuwa na GB 4
Tar 14 zikaisha.. nikaunga la 10k week wakanipa GB 3. Kesho yake zikaisha 😂😂 nikaongeza za 2k.. hazijaishi nazo

And natumia only JF na Whatsapp.. mara chache sana nakonekti na PC kutuma kitu..
6BE8268F-6965-4CFF-985A-B380E916569B.jpeg
 
Voda ni sema tunaishi nao kibishi..
Tar 10 nilikuwa na GB 4
Tar 14 zikaisha.. nikaunga la 10k week wakanipa GB 3. Kesho yake zikaisha nikaongeza za 2k.. hazijaishi nazo

And natumia only JF na Whatsapp.. mara chache sana nakonekti na PC kutuma kitu.. View attachment 2521610
Daah. Wahanga ni wengi sana. Ni kama kuna setting wamefanya. Ku speed Data Leakage. TCRA waki kagua wao wataona kweli umetumia MBs zote, ilihali siyo KWELI.
 
Mtu kila muda inakubidi kuunga data ikiisha.. maana kukaa bila MB ni haiwezekani. Mwisho wa siku unajikuta una ma dk na mi sms kibaooo

Hizo Mb nimeongeza leo za 5k
Zikitoboa juma5 nitakuja kusimulia 🤣

Voda kudadeq zenu
89E1D721-1729-4219-B7CF-C118F1287B62.jpeg
 
Daah. Wahanga ni wengi sana. Ni kama kuna setting wamefanya. Ku speed Data Leakage. TCRA waki kagua wao wataona kweli umetumia MBs zote, ilihali siyo KWELI.
Kuwahama ndio ngumu
Basi wanatubania hapo hapo yan
 
Sasa eatel ndo shida nimezoea nikiwa na mb 500 naangalia mechi dakika 90 na mb zinabaki lakini siku ya mechi ya psg ns bayan niliweka mb 500 hamwezi amini ila niliangalia mpira dakika 15 tu mb zikaisha nikachoka nakuchoka kesho yake nikaweka mb350 niliishia kusikiliza miziki miwili yenye dakika 4 mb zikaisha eateli wakati juzi mechi ya man city na alsenal niliweka mb 350 kwa voda nikaangalia dakika 45 nilivyowapigia eatel wananipa maelezo yakujinga eti niangalie data usag utafikiri nimeanza kutumia simu leo hadi kero
 
Ngoja niwape ushauri,

Aisee Voda ukitumia 4G ni hatari kwa afya yako, yaani ukiunga gb 1 ukizurura kidogo tu mtandaoni wanakutumia sms Yao kua umetumia 75% ya mb zako blah blah nyingi! Ukitumia 4G alafu Uplay video yaani Voda mb zao zinayeyuka kwa speed ambayo sielewi

Shida mojawapo niliyogundua let's say upo YouTube, unaplay video Ina dakika 10, afu unaitizama baada ya dakika 2 imeku bore unaiacha una click nyingine, aisee utaumia vibaya sana! Yaani kwa speed yao ya 4g unakuta wameshaidownload ile video online mpaka mwisho(Kuna kimstari keupe hua wanaonyesha) na MB zao unakuta washazikata kabisa, hii inamaanisha hata ukizima data bado una uwezo wa Kuangalia Hio video ya dakika 10 kutoka Hio dakika ya pili mpaka mwisho, maana inakua tayari imeshapakuliwa online na mb zinakua zishaenda, sasa ukiicancel ukaweka nyingine Hawa wapuuzi wanakua washakata MB za wewe Kuangalia dakika 10!

Ukifanya mchezo wa Kuangalia video nusunusu mfano upo insta unachek reels isipokufrahisha unachek nyingine aisee utaumia sana! Hawa wapuuzi watakupa stress za Mb, nadhani umenielewa!

Mimi nawasha 4G nikiwa na download ma file makubwa tu! Nje ya hapo naiset simu itumie 3g tu maana huku mjini Iko fasta sana sioni tofauti na mtu anayetumia 4g! Tangia nianze kufanya ivo naona mb zangu kidogo zinakakaa so haba! Nikiwaza wanaotumia 5g na huu ujinga wa Voda naona watakua na Hali Tete sana

Kuna kipindi wife nilimpa huu ushauri akawa mbishi, full kujiachia na 4g alafu alikua anapenda YouTube aisee alikua analalamika sana mara Voda wanakupendelea wewe, alivyokuja kuswitch to 3g anasema afadhali kidogo

Hebu mtu ajaribu hii mbinu afu a monitor matumizi yake ataleta mrejesho! Ila Voda ukijiachia na 4g ukitegemea Mb zitakaa utakula za USO

Sioni hata haja ya ku advance kwenda 5g kama wasipoboresha Bei za bando zao
 
We tafuta hela bhana, haya mengine ni kelele tu, mb 1480 sijui unataka utumie siku ngapi even if huangalii videos.
 
  • Thanks
Reactions: Tui

Ahsante. Nita jaribu hii
 
We tafuta hela bhana, haya mengine ni kelele tu, mb 1480 sijui unataka utumie siku ngapi even if huangalii videos.
Sasa mbona una lalamika petrol lita 1 shs 3000 au mchele kg 1 shs 3000 si utulie ukamuliwe. Hii nchi ina Vijinga sna (Dr. Mollel, 2023).
 
Back
Top Bottom