Wizi ktk gari

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
Salaam , ndg zanguni , yamenikuta jana mwandani wangu alikwenda tabata kumsalimia rafiki yake, kwa bahati mbaya hakuwa na mtu ktk gari hivyo alipofika kwa mwenyeji wake aliegesha gari nje na yeye kuingia ndani. aliporudi akakuta kioo cha mbele kimeyeyushwa na tundu kubwa liko pale na pochi lake na v2 kadhaa vimetoweka. JAMANI MUWE NA TAHADHALI IKIBIDI MUWE MNAACHA M2 KTK GARI. HUYO MWIZI AMEKOMBA V2 VYA MAANA NA AMETUACHIA HEKAHEKA.
 
pole sana.
Mwambie mwandani wako hata siku moja pochi na laptop na vitu vya thamani haviachwi garini.

Mliweka alarm? Atleast ingesaidia kuwashtua, unless she ignore it.

Pole sana, wizi kwenye magari umeshamiri. Kuwa makini hata kwenye foleni wanavunja vioo na kuiba.
 
Pole sana. Yaani ukiacha kitu kama pochi,begi la laptop ama simu garini umekaribisha wezi! Hata ukibeba watu,kila kituo waambie shuleni na vilivyo vyenu! Hopefully amejifunza.
 
Mbinu mpya inayotumiaka kukamata wezi " Unapoenda mahali unapohisi kuna wezi basi jaribu kuongozana na mtu mwingine halafu ashuke kabla ya mwisho wa safari na aendelea kutembea kwa miguu kukufuata ulipo wakati huo huo wewe ukiwa tayari umeshuka katika gari. Huyo uliyemshusha atakupigia simu ikiwa wezi watavamia gari lako na utachukua hatua muafaka. Kwa mtindo huu tumekamata wezi eneo fulani hapa mjini. Kwa maelezo zaidi unaweza kuni PM.
 
wanakera sana hawa jamaa it better ukagharamia alarm kwakweli inawashtuaga sana
 
Pole sana Mkuu. Gari haikuwa na alarm? Jitahidi muweke alarm ingawa sio 100% lakini ingemshtua wakati wa kurupshani za kuvunja kio. Aidha, tahadhari ni kwamba huwa wanaiba mara tu unaposhuka kwenye gari, ukiingia ndani ya nyumba tu nao wanaanza kazi maana wanafahamu kuwa bado utakuwa unasaliana, sio rahisi utake muda huo. Mimi nilibahatika kuwaona kupitia dirisha la nyumba wakiwa wanapekecha kioo, tulipotoka wakakimbia, sasa mazungumzo yakahamia kwenye gari.
 
Mbinu mpya inayotumiaka kukamata wezi " Unapoenda mahali unapohisi kuna wezi basi jaribu kuongozana na mtu mwingine halafu ashuke kabla ya mwisho wa safari na aendelea kutembea kwa miguu kukufuata ulipo wakati huo huo wewe ukiwa tayari umeshuka katika gari. Huyo uliyemshusha atakupigia simu ikiwa wezi watavamia gari lako na utachukua hatua muafaka. Kwa mtindo huu tumekamata wezi eneo fulani hapa mjini. Kwa maelezo zaidi unaweza kuni PM.

This is too analog technique !!

We unaweza kumtembeza mwandani wako kwa mguu usiku kisa kulinda wezi kwenye kumbi za starehe ??
 
Pole mwenye kuibiwa! Hilo limetokea Dar ila nawaambia hapa Arusha ndiyo imewaka nyakati hii yani raia wanavunjia vioo,mara unakuta gari limefunguliwa matairi unawekewa juu ya tofali,kuna best wangu wa karibu kabisa anaendesha gari ya kampuni lakini juzi night kali kakuta landcruiser imefunguliwa mkonga ya nje.
 
Naomba mhusishe huyu mwenyeji wako uliyemtembelea atajutafutia hao wezi wanajulikana tu wawekee dau na uwe mpole kwani Passport na vitambulisho hawana pa kuvipeleka

Ulitaka nao wakale wapi. Lazma tugawane umaskini wetu.

Pole sana.
 
Mbinu mpya inayotumiaka kukamata wezi " Unapoenda mahali unapohisi kuna wezi basi jaribu kuongozana na mtu mwingine halafu ashuke kabla ya mwisho wa safari na aendelea kutembea kwa miguu kukufuata ulipo wakati huo huo wewe ukiwa tayari umeshuka katika gari. Huyo uliyemshusha atakupigia simu ikiwa wezi watavamia gari lako na utachukua hatua muafaka. Kwa mtindo huu tumekamata wezi eneo fulani hapa mjini. Kwa maelezo zaidi unaweza kuni PM.
Hii nimeipenda nashukuru kwa hii mbinu
 
Na umuwekee tinted kali! Manake wataogopa kuchungulia ndani incase kuna mtu.

Kuliko uweke tinted bora uache manake kama hawawezi kuona ndani huwa wanavunja kubahatisha kama kuna kitu, wanajua magari yenye tinted watu wanapenda kuacha vitu ndani kwa vile havitaonekana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom