Wizara ya miundo mbinu....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,886
Hivi hili neno miundombinu maana yake hasa ni nini?????

Kila mara ukisikia viongozi wetu wakizungumzia miundombinu
utakuta wanazungumzia barabara.....
Sasa mpaka watu wa kawaida wameshazoea kuwa miundombinu
maana yake ni barabara.....

Halafu tazama tuna wizara ya madini na nishati,maji na mifugo,teknolojia na mawasiliano,ambazo ukizitazama utaona
zinahusika na miundombinu

kama neno miundombinu linatokana na neno infrastructure....

Basi inawezekana kuna makosa yanafanyika mahali....
Kenya wao wanaita miundomsingi wakimaanisha infrastructure

mimi naona tuwe na wizara za miundo mbinu badala ya miundombinu au wizara moja iundwe ya mundo mbinu ikihusisha yote.maji,nishati,mawasiliano,barabara,reli, n.k

wenzetu wakisema wanaimarisha miundombinu wanazungumzia
vitu vingi sana,bandari,airport,reli,simu,umeme,maji na kadhalika....

Sisi ukisikia neno miundombinu ujue wanazungumzia barabara..

Sijui tatizo liko wapi.....
 
...
 
wamegawanya hivyo ili iweze kutimiza mahitaji yake, kama ikiunganishwa na hizo nyingine hakutakua na ufanisi, ni mawazo yangu tu lakini sijui wengine watasemaje mkuu
 
sawa.
Lakini mi nafikiri hili neno miundombinu
hawalielewi vizuri...
Labda wabadili hili neno..
 
Usisahau holi neno ni jipya..
Limeanza kutumika wakati wa mkapa.
 
Back
Top Bottom