Wizara ya Madini na mfumo wa leseni kwa wachimbaji wadogo unavyoneemesha wachache na kukamua mitaji ya wanyonge

Jorowe

Member
Jun 9, 2018
85
195
Maeneo mengi ya uchimbaji yanamilikiwa na watu wanaojulikana ndio wenye leseni za uchimbaji kwa eneo husika...

Hii njia ni ya kinyonyaji na inaneemesha wachache wenye connection na wakubwa ndio maana nahisi haipigiwi kelele sana maana inaowaumiza ni wale wasio na sauti.

IKO HIVI
Ifahamike maeneo mengi yanayochimbwa na wazawa yanagudurika na wachimbaji wale wadogowadogo....

Wenye pesa wakishaona eneo limeanza kuchimbwa na linatoa wenyewe hata hawahnagaiki kuchimba

Wanachofanya wanakimbilia madini kwa ajili ya process za kukataa leseni kwenye eneo husika

Wakishakapata leseni wanaenda kujenga kibanda vile vya mabati juu na chini hiyo ndio inakuwa ofisi yao.....

KINACHOFUATA BAADA YA HAPO
Ni kila mwenye duara kuwa anatoa asilimia 30% ya mifuko ya mawe anayozalisha kumlipa yule mwenye leseni.

Yaani hiyo asilimia 30% unamlipa hajachangia kitu chochote anakuja kuchukua tu!

Haikomei hapo bado unatakiwa utoe asilimia 7% kwa tume ya madini then asilimia 0.3 kwa Service Levy

Ileweke hizi kodi zote zinatozwa mlimani hata kabla hujabeba mzigo kwenda kuchenjua, Hapa ni sawa na ulipe kodi ya kuvuna mazao kabla hata hujayapeleka sokoni!

Ukijumlisha hapo mchimbaji mdogo anakatwa kodi ya zaidi ya asilimia 37.3% hayo makato yote ni kutoka kwenye mzigo ghafi ukiwa mlimani hata dhahabu bado haijapatikana.

Bado mchanga uliokatwa kodi ya 37.3% ukiwa mlimani dhahabu ikishapatikana ukienda soko la dhahabu kuuza unakutana tena na rungu la kodi hizi

Madini 7%
Services Levy 0.3%

Ukijumlisha kodi zote hadi sasa ni Asilimia 44.6%

Kwa kifupi ni hivi
Ukitenga bajeti ya mtaji tuseme 100M asilimia 37.3% zaidi ya 37m utazikabidhi kwenye leseni atachukua 30M akiwa amekaa bila jasho! Hizo zingine tume madini watachukua.

Swali ni je
Wizara ya madini haioni huu mzigo aliorundikiwa mchimbaji mdogo ?!

Kwanini serikali wizara isiwapunguzie asilimia hao mabwanyenye wanaojiita wenge leseni ikawa wanachukua hata asilimia 10?!

Ukichunguza kwenye kila eneo lenye leseni unakuta kuna jina moja kati ya wenye leseni ambalo liko either badala ya kigogo au ndugu wa kigogo kwenye wizara ya madini huwezi ukamuona yeye..

Ila utasikia hapa wakurugenzi wa mlima ni flani na flani ila flani anasimamia jina la flani..HAPA NDIPO ULIPO MZIZI KWANINI HII ASILIMIA 30% ya wenye leseni haipigiwi kelele!

Wizara ya madini pamoja na tume madini tupunguzieni huu mzigo tutamaliza mitaji fanye mwenye leseni awe anachukua asilimia 10% maana hakuna anachokifanya !.

Alternative nyingine ambayo itaongeza mapato kuliko hata hiyo hela inayolipwa kwa ajili ya mwenye leseni ni kila duara iwe inalipa kodi direct hata kama ni kila mwezi hii itapunguza maumivu kwa mchimbaji mdogo.
 
Mwenye leseni achukue 5% tu. Ama achague kufanya kazi. Ama walipwe kwa masaa. Let say mwenye shimo kachimba wiki nzima, baada ya hapo anampisha mwenye leseni anachimba kwa masaa 24. Ili aone ilivyo kazi
 
Mwenye leseni achukue 5% tu. Ama achague kufanya kazi. Ama walipwe kwa masaa. Let say mwenye shimo kachimba wiki nzima, baada ya hapo anampisha mwenye leseni anachimba kwa masaa 24. Ili aone ilivyo kazi
Fact kabisa
Inauma umechanga ukajikusanyia mifuko yako anakuja mtu hajachangia hata mfuko mtu wala mtendakazi anabeba mifuko 30 kwenye 100
 
Back
Top Bottom