Wivu siyo asili yetu afrika, Bali ni janga linalotutafuna kuliko bangi

Samico Tanzania

JF-Expert Member
Feb 6, 2022
276
792
Kuna misemo na nahau nyingi sana tuliwahi kujifunza huko shule ya msingi ambayo ilitosha kutupatia msingi wa maisha yetu hata leo! Mfano wa msemo!

"Kutokujua kutumia kilicho bora; ni mwanzo mzuri wa kutumia kibovu"

"Watu wengi huangamia kwa kukosa maarifa"

"Mkataa pema, Pabaya panamuita"
"Chanda chema, Huvikwa Pete"

" Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu" n.k

Misemo na Maneno mengine kama hayo ukiyasikia unaona kama yaliwahusu wengine!

Lakini ukweli ni kwamba hayo ndiyo msingi halisi wa maisha na pengine ndiyo maana yanasomwa msingi!

Kwa maana hiyo tulitakiwa tuboreshe hapo kwenye masomo ya msingi tuongeze na somo la mila na desturi ili tusipoteane mbeleni!

Wivu siyo asili yetu afrika!

Tamaduni na maisha ya wazee wetu inaonesha wazi hapo zamani afrika hapakuwa na wivu!

Hapo zamani Mme, alipokuwa akitoka safari hakwenda nyumbani moja kwa moja ghafla! Ilikuwa lazima kutuma kwanza ujumbe kama ishara, ili mke aweke mambo sawa!

Wazee walikuwa wanatuma vijana wapeleke koti, au fimbo au chochote kinachotambulisha mzee anardi!
Hiyo haikuwa na maana kwamba ni vizito bali ilikuwa ni kuepusha fumanizi!

Hivi leo Ingizo la teknolojia ya simu lilitakiwa lifanye vizuri zaidi sasa kwa maana tungekuwa tunaenzi tamaduni hiyo tungelikuwa tunapiga simu kabisa kwamba mama nichemshie maji nakuja! (Hakuna fumanizi lingetokea)

Tamaduni za zamani za wamakonde na wazaramo zinadhihilisha wazi hakukuwa na wivu ndiyo maana wake waliruhusiwa kwenda ngomani wala haikuwa nongwa!

Naomba kutolea mfano tamaduni za wairaki, wamang'ati na wamburu zamani!

Makabila hayo kabla ya wivu kuwakumba hawakuruhu wivu wa kijinga! Mfano!
1. Mwanamke ambaye mimba imeharibika alitengwa na kufanyiwa tambiko kwa imani kwamba ule mkosi wa mimba kutoka lazima utolewe kwanza ili usije kujirudia!

Baada ya elimu ya wazungu hilo halipo tena kwasasa!
Lakini ukisoma hata maandiko Leo unaona kumbe walewazee walikuwa sahihi kufanya ibada zao za tambiko la kuondoa mkosi huo!

Mwanamke aliyeharibikiwa na mimba au kufiwa wakati wa kujifungua walimtenga kando hadi pale atakapopata mimba nyingine ndipo arudi kwa boma!

Walikuwa wanatafta kijakazi (manamba) kutoka mikoani wakumhudumia akiwa huko shambani, hata vyombo vyake havikutakiwa kugusana na vya bomani (ilikuwa ukimpelekea maji unamiminia ukiwa umbali wa mita mbili kando ili msigusane!

Yule mama ilikuwa akishapata mimba nyingine, ndipo aliruhusiwa kurudi kwa boma wakiamini ule Mkosi umeondoka na huyo mtia mimba!

Na mtoto aliyezaliwa alihesabika ni mali ya bomani! (Hakuna wivu ilikuwa fresh)

Mfano 2.
Mama wa boma, alikuwa anamtaftia mzee msaidizi yaani mwanamke!
Na ikitokea mzee hajaridhika alitoa taarifa kwa bibi ya boma kuonesha kwamba huyo msaidizi aliyeletwa ni goi goi! Hivyo alitafutwa mwingine! ( na hayo yalifanyika kwa weledi siyo kienyeji kama tunavyowaza mm na wewe) kuna vitu walivyovitumia kupima kama hafai! (Wivu haukuwa na nafasi)

Mfano wa 3
Mwanaume ilikuwa marufuku kuuliza mkeo alikopata mimba, ukiona ana mimba hiyo ni yako shukuru!
Wanaume walevi, wavivu na wakarofi ambao ni kero ndani ya boma walifukuzwa nyumbani na wake zao kwa dawa maalum ya mkiwa wa...
(Hakukuwa na wivu kabisa)

Kiufupi tamaduni zetu nyingi hazikuendekeza wivu wa hovyo kama leo!

Kama ilivyo kawaida ya wazungu walichofanya kwa mababu Walipokuta mababu zetu wanachezea alimasi kwenye bao wakawapa goroli!

Ndivyo ilivyo kwenye tamaduni zetu, Tulipaswa kuziboresha tu kimaandishi zitambulike, lakini rasmi tumeziacha sasa tunataka mapenzi ya tamthilia, mapenzi ya ulaya!

Tunaoana hovyo pasipo kufuata tamaduni zetu

Makabila yenye mila tofauti yanaoana tutarajie nini?

Watu wanatoa mimba hovyo wakiamini hakuna madhara tena kiimani yatayowaandama!

Watu Tunaoana Leo kwa mamilioni ya fedha na kuachana kesho yake kwa kosa la wivu!

Mahusiano mengi yanavunjika siku hizi kisa wivu wa kujitaftia!

Mauaji mengi chanzo ni wivu!

Watoto wa mtaani wamekosa malezi ya baba na mama kisa wivu!

Wivu ni kero kubwa sana unaomfanya binadam awe chini ya ulinzi kisaikolojia!
(Yaani unaolewa au kuoa halafu unakuwa chini ya ulinzi)

Kuna wamama wanajuta kuolewa kisa wivu wa hovyo, kuna wababa wanajuta kuoa kisa wivu!

Wivu umewatoa watu kwenye wajibu wa ndoa wanageuka wapelelezi!

"Janga la wivu linaharibu pakubwa sana kuliko madhara ya bangi"

Bomu la wivu likiripuka linasambaratisha familia watu zaidi ya 10

Ambaye hujamuumba wewe hutakiwi kumwonea wivu! Fanya kila uwezaro usije kuingia kwenye wivu!

Ajabu waliotufundisha haya mapenzi ya wivu kuwa ndiyo maisha wamekuja kuyapinga tena kupitia dini zao!

Kuna mtu anauliza fundi Samico unaongea nini?

Nasema hivi kwenye dini zao wazungu wivu umepigwa vita!

Hii inadhihilisha wazi babu zetu walikuwa sahihi kabisa kutokuwa na wivu, tungeboresha tu!

Ebu Soma yakobo 3:16 (Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya)

Pia soma! Mithali 6:34
(Maana wivu ni ghadhabu ya mtu; Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi.)

Kama hujaelewa soma hili andiko pia:

Matendo 13:45
(Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa WIVU, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana).

Kuna mtu bado ana WIVU Mahali ebu soma;

Wagalatia 5:19-20,21

Ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, WIVU, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

ANAEHUKUMU NI MUNGU! Ficha sana na jitenge mbali sana na mambo yatakayoibua wivu!

Ukienda kumtembelea Mwenzako Dodoma usipekenyue mambo yanayo amsha WIVU!

Hata wewe bosi usirudi toka safari kimya kimya maana usipomkuta nyumbani WIVU utakuwakia!

Kitanda hakizai haramu; Tuishi Humo kwa upendo Jaman, Mengine Tumwombe Mungu!

Wivu siyo asili yetu!
 
Upo sahihi ila bangi haijawahi tafuna mtu.
Bangi iheshimiwe tafadhali.
Vinavyotafuna watu:-
No 1:
Elimu mbovu yakitumwa inayofanya watu kukariri km kasuku.
Tumefikia watu wanaojiita wasomi ndio wamekuwa mwiba mchungu kwenye jamii. Huwezi kutofautisha kati ya profesa na kichaa.
No 2:
Imani za kidini ni mwiba hatari sana kuliko shetani mwenyewe.
 
"When what's done cannot be undone"
 
Back
Top Bottom