Se Busca
Member
- Dec 11, 2023
- 41
- 72
Christopher Mutsvangwa Balozi wa zamani wa Zimbabwe nchini China anasema kuwa mikopo ambayo China inatoa kwa nchi zinazoendelea hususani Afrika haijawahi kuwa ya kiunyonyaji kutokana na riba zake nafuu ukilinganisha na tasisi za kifedha kutoka nchi za magharibi kama Benki ya Dunia (WB) na shirika la fedha la kimataifa (IMF).
Anasema "Hakuna nchi yoyote ya Kiafrika inayolemewa na deni la China. Mzigo wa madeni barani Afrika unasabishwa na Benki ya Dunia, taasisi za Bretton Woods za nchini Marekani na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lakini, wanataka kuishutumu China." "Nchi za magharibi zina wivu kwa sababu mikopo kutoka China inaifanya Afrika kuwa ya kisasa
Inaifikisha Afrika kwenye hatua ya uchumi wa dunia. Wale wanaoishutumu China kwa kusababisha mtego wa madeni kwa nchi za Afrika wana wivu. Tunahitaji mikopo mingi zaidi kutoka China."Christopher Mutsvangwa.
Kwa miongoni mingi nchi za Afrika zimekuwa njiapanda huku zikijaribu kutafuta washirika sahihi kutoka nchi
zilizoendelea kama China.
Marekani na Urusi ili kukuza Uchumi wao hali ambayo imepelekea kubadilisha wakoloni kila asubuhi na jioni.
Thomas Sankara aliwahi kusema kuwa " Kuikimbia Ufaransa na kwenda China sio njia sahihi ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Afrika bali ni mchezo usio wa akili unaobadilisha mkoloni mmoja kwenda kwa mkoloni mwingine atakaye endelea kukutawala, hakuna nchi ambayo inahuruma kwaajili ya nchi nyingine.
Hakuna mkopo ambao ni bora kuliko mkopo mwingine.
Je, unakubali kuwa mkopo unaotolewa na China kwa nchi za Afrika una riba nafuu kuliko taasisi zingine za kifedha za magharibi kama Benki ya Dunia na IMF?