OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Uchumi wa Tanzania kwa asilimia kubwa upo kwa wageni. Yes! Matajiri wengi waliopo Tanzania sio watanzania kwa asili, wengi wana asili za nchi nyingine. Hii ni kwasababu hatuna akili za biashara kabisa. Niliposoma gazeti hili la majira kuhusu sakata linaloendelea ndio nikaona shida zaidi.
Agha Khan moja kati ya hospitali inayotumiwa na wengi wenye hela zao inasifiwa kwa huduma bora, sasa mtu anataka the so called "Utu" kwa gharama ya nani?. Nadhani tunakwepa jukumu msingi au hatutaki kuona shida iko kwa anayepaswa kulipa.
Niseme tu, sisi (wananchi) tunachangia hela ya kutosha, NHIF waangalie fedha wanazowapa hospitali ili kuweka mambo sawa na sio kutaka wananchi wadhani wanaonewa wakati NHIF inaweka fedha kidogo kwa watoa huduma.
Lazima tujue ili kutoa huduma nzuri, kunahitaji gharama, maisha ya Dkt wa Agha Khan huwezi fananisha na maisha ya Dkt kwenye zahanati ya kijiji ambayo siku zote dawa hawana. kwa hili wananchi tulishwe matangopori kwa jina la "UTU". Hizi hospital zinahitaji fedha kujiendesha, sisi tumeshatoa fedha kupeleka NHIF, hivyo NHIF waache uhuni.
Kingine, tusifikirie kwamba afya yako ni jukumu la fulani, watu wanafanya biashara, kama wananchi kweli mnataka mfanyiwe utu, fungueni hospitali zenu jitibieni bure. To hell with philanthropism.
Signed!
OLS