Wito: "wanaoua Albino na wenyewe muwaue!" - Pinda

...mzee mwanakijiji unataka kuanza Impeachment process nini? :D
 
Utanitumia audio ya Waziri Mkuu Pinda akitangaza operesheni "jino kwa jino" ambapo inadaiwa alitoa kibali kwa UVCCM kushiriki katika mauaji ya watu wanaoamini kuwa ndio wauaji wa maalbino. Kama unayo sehemu ya hotuba hiyo wasiliana nami haraka iwezekanavyo.

Wa kwanza kutuma ndiye atakayepata kifuta jasho hicho: Hata kama iko kwenye tape za kawaida.

Wasiliana nami: mwanakijiji@mwanakijiji.com
Nikii-upload hapa vipi mkuu?
 
itakuwa safi mkulu invisible,tupate kuisikiliza kutokea hapa.BTW ni kweli alitoa kauli hiyo? duuuh Mh.Pinda atakuwa ameudhiwa na hilo mpaka anashindwa kuzizuia hisia zake (emetions).

Lakini hili jambo linachukiza sana kuwafanya watu wasiishi kwa amani na kufurahia uwepo wao duniani ni jambo baya sana.
 
nimesikia kipande kidogo cha hiyo hotuba ya kuhusu wauaji wa maalbino nao kuuwawa kupitia ulimwengu wa BBC leo Jioni. Mh. PM alikuwa akibainisha kuhusu mob justice.
 
Hata mie nimesikia kipande hiki aliposema Mkuu Pinda nanukuu" watu wamekumbiza na kiungo cha albino halafu ukafika bondeni na ukakitupa halafu wakakukamata je wakufanyaje?" namaliza nukuu. Nadhani Mwanakijij kama utaweza kuwasiliana na BBC wanaweza kukupatia hii tape au watakusaidia zaidi jinsi ya kuweza kuipata.
 
Exactly Mtu wa Kawaida,

Nilichotaka kufanya ni kuwasiliana na BBC wanipe nakala. Mwanakijiji, simply wasiliana na kina Hassan Mhelela wanaweza kukurahisishia kazi na bila gharama kubwa. Nawakubali vijana wetu pale BBC Swahili (London na Dar) na naamini wanaweza kukupa ushirikiano kwani daima wako mstari wa mbele!

BTW: Hii inanikumbusha kijana wa UDSM aliyesema "Tanzania haitakalika..."
 
Nadhani Waziri Mkuu alikuwa na hasira sana kutokana na kuendelea kwa mauaji ya Albino. Anayo haki ya kuwa na hasira hivyo kwa maana kwa kweli inatisha na kusikitisha sana. Tatizo ni kuwa inawezekana alisahau kuwa yeye ni Waziri Mkuu na anatakiwa kuongoza kwa kutumia sheria badala ya maoni yake binafsi. Vile vile anatakiwa ajue kuwa kauli yake ina nguvu nyingi sana.

Ina maana tutaanza kusikia mauaji ya holela kwa watu hata wasio husika na mauaji ya Albino. Nahofia kuwa, watu watauana kwa kusingizia kuwa victim alitaka kuua ua kumdhuru Albino. Sijui tutaishia wapi. Isije ikawa tutaanza kufunguliwa milango ya mauaji ya kimbari hapa nchini. Ombi langu ni aombwe atoe maelezo ya kina kuhusiana na kauli hiyo. Na itakuwa jambo la maana sana kama ataibadilisha haraka sana.
 
Washauri wa Waziri Mkuu, Pinda inabidi aongee ASAP kukanusha kauli hiyo.

Rule of Law lazima itawale NO MATTER WHAT.

Sababu kama anayemuua albino, naye wananchi wakamuua, what will stop ndugu wa huyo marehemu na wao kuwauwa waliomuua, ambao itakuwa ni mzunguko wa mauaji kila mmoja akisema analipiza kisasi.
 
mmh sasa wakanushe ukweli? hivi lini tutajifunze kuomba radhi tunapo potoka?
 
Hata mie nimesikia kipande hiki aliposema Mkuu Pinda nanukuu" watu wamekumbiza na kiungo cha albino halafu ukafika bondeni na ukakitupa halafu wakakukamata je wakufanyaje?" namaliza nukuu. Nadhani Mwanakijij kama utaweza kuwasiliana na BBC wanaweza kukupatia hii tape au watakusaidia zaidi jinsi ya kuweza kuipata.

Nukuu hii ndio iliyozaa stori ya mwananchi leo kuwa Pinda amesema wanaoua albino wauawe?
 
Mimi siamini kuwa maneno hayo yamesemwa na Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mbunge na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambae kitaaluma, ni Mwanasheria aliyebobea!. Atakuwa amenukuliwa vibaya!.

mstari kwa mstari, neno kwa neno, nipo pamoja na wewe mkuu
 
- Kwa kweli hata mimi ninampa Pinda, benefit of the doubt sidhani kama anaweza kukurupuka namna hii, something is not right hapo haijakaa sawa hii!
 
nimesikiliza BBC hata hivyo na wao wameweka kipande kidogo sana na wala hakikaribiani na hiyo nukuu ya Mwananchi. Naamini kuwa hotuba nzima si rahisi kupatikana.
 
Utanitumia audio ya Waziri Mkuu Pinda akitangaza operesheni "jino kwa jino" ambapo inadaiwa alitoa kibali kwa UVCCM kushiriki katika mauaji ya watu wanaoamini kuwa ndio wauaji wa maalbino. Kama unayo sehemu ya hotuba hiyo wasiliana nami haraka iwezekanavyo.

Wa kwanza kutuma ndiye atakayepata kifuta jasho hicho: Hata kama iko kwenye tape za kawaida.

Wasiliana nami: mwanakijiji@mwanakijiji.com

Kama ilitoka katika BBC nikueleza ilikuwa siku gani na wakti gani itapatikana tu
 
Yale Yale ya Mh. Mwinyi na Mrema kuua vibibi vizee huko Shinyanga kwa kusikiwa kuwa ni WACHAWI!..
 
Back
Top Bottom