Ushauri kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP, Mameya, ma-OCD na ma-RPC: Kwa kuwa ukahaba sio kosa la jinai, basi misako ya makahaba ikomeshwe mara moja

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
1701450354975.png

Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Tanzania

I. Utangulizi

Mheshimiwa Hamad Masauni,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Tanzania,

Msako wa makahaba jijini Dar-es-Salamaa uliosababisha Mauaji ya Razak Azan, Mlinzi wa Baa ya Boardroom huko Sinza, Wilayani Kinondoni, sio sawa na tukio la mgonjwa aliyefia hospitalini kutokana na mapenzi ya Mungu, kama alivyoripotiwa kusema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Badala yake hili ni tukio linalotutaka kujichunguza, kujikosoa na kukosoana. Tukiwa tunatekeleza jukumu letu la kuwaongoza viongozi kwa njia ya kusanifu hoja za kitafiti, barua hii ni kwa ajili ya kulikosoa Jeshi la Polisi na kulishauri ipasavyo.

Hasa tutashauri kwamba, kwa kuwa ukahaba sio kosa la jinai, basi misako ya makahaba ikome mara moja, na badala yake serikali ielekeze nguvu zake katika uwezeshaji wa kiuchumi wa makundi ya vijana na wanawake yaliyotelekezwa katika jamii.

II. Msako wa makahaba na mauaji ya Mlinzi wa Baa Jijini Dar es Salaam

Tunafahamu kwamba, tarehe 31 Oktoba 2023 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, aliagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuanza msako wa makahaba, kufunga biashara za masaji zinazotumika kama madanguro, na kuvunja nyumba zinazotumiwa kama madanguro.

Kisha, tarehe 04 Novemba 2023, Chalamila alikwenda Mwananyamala kuongoza operesheni ya kubomoa baadhi ya nyumba alizosema ni madanguro. RC Chalamila alisema operesheni hiyo ni endelevu katika mkoa mzima wa Dar es Salaam.

Na hatimaye usiku wa tarehe 29 Novemba 2023, mapolisi wawili wa kituo cha Mabatini, Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam, walianza kutekeleza maagizo ya RC Chalamila kwa kuvamia baa ya Boardroom iliyoko Kata ya Sinza, eneo la Sinza Mapambano, Mtaa wa Nginana, wakisaka makahaba.

Kigezo walichokuwa wanatumia ni uvaaji wa nguo fupi au nguo zinazobana. Mlinzi wa baa hiyo, Razak Azan, aliingilia kati akiwakataza mapolisi kuingia kwenye baa na silaha za moto maana ni kinyume cha taratibu za kiusalama kwenye maeneo ya starehe.

Walimpiga risasa, sasa amekufa, na kwa mujibu wa taarifa ya polisi mwili wake uko hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi. Vide clips zifuatazo zinaonyesha sehemu ya tukio la uvamizi wa baa husika.





III. Matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia defender za polisi

Lakini, tatizo kubwa zaidi ni kwamba, msako wa makahaba unachochewa na kitu kingne. KUna matumizi mabaya ya madaraka ndani ya Jeshi la Polisi.

Baadhi ya Magari ya Defender yanayotumiwa na Jeshi la Polisi kuwakamata watuhumiwa wa ukahaba yanaonekana kufanya hivyo, wakati mwingine, kwa ajili ya kutimiza agizo haramu la wakubwa.

Agizo hilo ni kwamba timu ya mapolisi wanaopewa gari aina ya defender kuzunguka nayo, baada ya mzunguko, wanapewa sharti ya kukabidhi fedha ipatayo TZS 200,000/= kwa bosi aliyeidhinisha gari.

Haya ni mapato ya siku moja. Bila kufanya hivyo, kesho yake defender husika inakabidhiwa kwa watu wengine "wanaojua kuitumua," na hawa wengine wanakaa benchi.

Kwa ajili ya kutimiza sharti hili akikamatwa mtuhumiwa wa ukahaba hapelekwi mahakamani, maana mapolisi wanajua fika kwamba ukahaba kama ukahaba sio kosa la jinai, na kwamba hata yale makosa ya jinai yanayohusiana na ukahaba hayathibitiki mahakamani kirahisi.

Badala yake polisi huwekwa watuhumiwa wa ukahaba rumande. Kisha watuhumiwa hulazimishwa kuwapigia simu wateja wao watume fedha kati ya TZS 30,000/= na 60,000/=. Baada ya malipo haya kufanyika mtuhumiwa huachiwa huru.

Yote haya yanafanyika wakati hakuna kifungu cha sheria za Tanzania kinachosema kwamba kitendo cha kufanya ukahaba kama ukahaba (prostitution per se) ni kosa la jinai.

Kwa mujibu wa vifungu vya 145, 146 na 148 vya Sheria ya Kanuni za Adhabu (Sura ya 16, Toleo la 2002), kama vikisomwa pamoja na sheria ya kuzuia biashara ya kusafirisha watu na kuwaingiza kwenye utumwa wa kikahaba (Anti-trafficking in Persons Act No. 6/2008), matendo yaliyo haramu kisheria ni:
  • Kuendesha biashara ya danguro,
  • Kuishi kwa kutegemea mapato yanayotokana na ukahaba (na hii maana yake ni kwamba kama mama akiamua kufanya ukahaba kwa ajili ya kutafuta fedha za kumhudumia mtoto wake mchanga sio kosa kisheria),
  • Kumwingiza mtu baki katika biashara ya ukahaba, na
  • Kusafirisha watu na kuwaingiza kwenye utumwa wa kikahaba.
Hivyo ndivyo sheria za Tanzania zinavyosema. Na hii ndio sababu inayoeleza kwa nini tangu 2018 mpaka 2022 taarifa za kipolisi za kila mwaka zinazochapishwa na NBS kwenye Ripoti ya "Tanzania in Figures" hazitaji ukahaba kama mojawapo ya makosa ya jinai nchini Tanzania. Kiambatanisho hapa chini kinathibitisha kauli hii.

Wabunge wetu na Vigogo wengi wa Jeshi la Polisi wanaufahamu ukweli huu. Wanasheria katika ofisi za ma-RC na ma-DC wanayafahamu haya pia.

Pamoja na haya bado kina Chalamila wanaangukia pua katika namna ambayo inaivua nguo serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika milenia ya tatu hakuna serikali ya Taifa linaloongozwa na katika inayotambua kanuni za demokrasia ya kiliberali na kisekulari (liberal and secular constitutional democratic state) inayokimbizana na makahaba hadi vyumbani wanakowahudumia wateja wao wanaonunua "upendo" kwa hiari yao.

IV. Aina tano za sera za kidunia kuhusu namna ya kudhibiti ukahaba

1701470109137.png


Kwa ujumla, kila nchi inazo sheria zake kuhusu namna ya kudhibiti biashara ya ukahaba. Kwa mujibu wa utafiti wetu, sheria za nchi zote zinagawanyika katika makundi matano kama ifuatavyo:

(1) criminalize buying and selling of sex, as well as related activities such as street walking, kerb crawling, pimping, and brothel-keeping (the policy in most U.S. jurisdictions except Nevada State).
(2) criminalize buying and brokering of sex, including brothel-keeping, but not the people who sell sex (i.e. prostitutes). (the policy in Sweden, Norway, Iceland, Finland, Northern Ireland, Canada, and, most recently, France).
(3) criminalize prostitution-related activities such as living on earnings of prostitution, streetwalking, kerb crawling, pimping, and brothel-keeping, but don’t criminalize the buying or selling of sex as such (the policy in England, Wales, Scotland, India and Tanzania)
(4) criminalize pimping and brothel-keeping, but don’t criminalize the purchase or sale of sex as such or other activities by sellers (the policy in Denmark and Israel); and
(5) don’t criminalize any prostitution-related activities other than trafficking and forced prostitution, but license, impose age limitations and regulate matters of health and safety (the policy in Germany, the Netherlands, New Zealand, and Nevada).

V. Jinai zinazohusiana na ukahaba, madanguro, na madalali wa ukahaba

1701495560377.png

Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali


Hapo juu tumesema kwamba, kwa mujibu wa vifungu vya 145, 146 na 148 vya Sheria ya Kanuni za Adhabu (Sura ya 16, Toleo la 2002), kama vikisomwa pamoja na sheria ya kuzuia biashara ya kusafirisha watu na kuwaingiza kwenye utumwa wa kikahaba (Anti-trafficking in Persons Act No. 6/2008), matendo yanayohusiana na ukahaba yaliyo haramu kisheria ni manne.

Yaani: Kuendesha biashara ya danguro, Kuishi kwa kutegemea mapato yanayotokana na ukahaba, Kumwingiza mtu baki katika biashara ya ukahaba, na Kusafirisha watu na kuwaingiza kwenye utumwa wa kikahaba.

Hapa chini tunathibitisha tamko hili kwa kuambatanisha vifungu husika vya sheria za Tanzania ili kuthibitisha mtazamo kwamba ukahaba sio kosa la jinai.

Kielelezo A: Vifungu vya sheria kwa lugha ya Kiswahili

145(1)(a) Mwanaume ambaye kwa kufahamu anaishi kwa kutegemea kipato au sehemu ya
kipato chake anakipata kutokana na biashara ya ukahaba... anafanya kosa.
146A. Mwanamke ambaye akiwa anafahamu anaishi akiwa akitegemea kipato chake au sehemu ya kipato chake kutokana na ukahaba, kwa ajili ya kuishi, ana mamlaka, au anashawishi juu ya mwenendo wa kahaba kwa namna hiyo ili kuonyesha kuwa anasaidia, anashawishi au kumlazimisha mwanamke huyo kufanya ukahaba na mtu yeyote, anatenda kosa.
148. Mtu yeyote ambaye ametenga nyumba, chumba, vyumba au sehemu yoyote kwa nia ya ukahaba, anatenda kosa.

Kielelezo B: Vifungu vya sheria kwa lugha ya Kiingereza

145 (1) (a) A male person who knowingly lives wholly or in part on the earnings of prostitution ... commits an offense;
146A. A woman who knowingly lives wholly or in part on the earnings of prostitution or who is proved to have, for the purpose of gain, exercised control, direction or influence over the movements of a prostitute in such a manner as to show that she is aiding, abetting or compelling her prostitution with any person, or generally, is guilty of an offence.
148. Any person who keeps a house, room, set of rooms or place of any kind whatsoever for the purposes of prostitution is guilty of an offence.

VI. Hitimisho

Tunapendekeza kwamba, ukweli huu uwaweke huru makahaba na mapolisi kwa kukomesha misako ya makahaba katika sehemu yoyote nchini Tanzania.

Na kubwa zaidi ni kwamba Community Development Officers wetu waelekeze nguvu katika uwezeshaji wa kiuchumi wa makahaba na vijana wanaonyemelewa na ukahaba.

Mfuko wa kuwawezesha vijana na wanawake unahitajika kuelekezwa kwenye eneo hili haraka.

Baada ya kusema haya, tunatanguliza shukrazi za dhati tukiwatakia uwajibikaji mwema katika mipaka ya sheria za Bunge na sio vinginevyo.

VII. Vimbatanisho muhimu

Kiambatanisho Na. 1. Kauli ya RC Chalamila ilivyoripotiwa na mitandao ya kijamii

1701455821466.png


Kiambatanisho Na. 2. Takwimu za jinai kwa mujibu wa Ripoti ya Tanzania in Figures ya 2022

1701464818757.png


Kiambatanisho Na. 3. Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu mauaji ya Sinza

1701506278537.png


Mama Amon,
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu,
Dawati la Uchunguzi la Mama Amon (DUMA),
SLP P/Bag
"Sumbawanga Town"

Sumbawanga.

CC: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwalimu Albert Chalamila.
 
Sawa Prof

Nimeanza kuwaona Makahaba pale Mwananyamala A tangu nikiwa shule ya Msingi hadi sasa ni mstaafu

Ngoja tuone nguvu ya Songoro maana yeye mwenyewe kajenga Bwawani 😂
 
Sawa Prof

Nimeanza kuwaona Makahaba pale Mwananyamala A tangu nikiwa shule ya Msingi hadi sasa ni mstaafu

Ngoja tuone nguvu ya Songoro maana yeye mwenyewe kajenga Bwawani
Tena siku hizi makahaba wanafanya mambo yao kidigital
Enzi zile za magot au uwakute pale ohio St,na Tunisia Road kinondoni
Ilikuwa balaaa
Makahaba wako kila sehemu wanaenda kutega Serena,sea cliff, golden tulip kwenyewe kuna makahaba wanaenda kutega pale sasa utawazuia
Hiyo dodoma yenyewe makahaba kibao wanajaaga wanaenda wakati wa vikao vya bunge na serikali na viongozi hao hao tunawqona wakijivinjari na makahaba

Ova
 
Madanguro walipishwe kodi
Yawe na utaratibu maalum
Viongoz wenyewe ndiyo wadau
Wakubwa wa hao
Hebu tuache unafiki

Ova
 
Na usije kushangaa hata RC huyu (Albert Chalamila - na kumbe ni School teacher by professional) naye ni kahaba au hulipa pesa kahaba ili apate ngono..!

Na bila shaka sasa naelewa, kumbe huo hata sio msako wa kusaka makahaba bali ni msako wa kusaka pesa kwa njia ya "kusingizia watu makosa"..

Kwa hiyo kumbe huu ni mradi wa kutafuta fedha wa maafisa wa polisi wa wilaya, mikoa na hata IGP..

Na yaweza kuwa kweli Kwa sababu, kuna wakati hawa maaskari polisi hufanya ujinga hata kuua kwa kisingizio cha "kurushiana risasi na wahalifu".

Na kwa sbb hii watu hubaki midomo wazi tukijiuliza hawa ni mapolisi au majambazi yaliyovaa uniform za polisi tu?

Asante sana Mama Amon
 
Ni vyema tukaitafakari kwa kina nukuu hii kutoka katika kipande cha Injili. "Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu basi na awe wa kwanza kumtupia jiwe mwanamke huyu aliyefumaniwa akizini"
View attachment 2830641
Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Tanzania

Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Tanzania,

Msako wa makahaba jijini Dar-es-Salamaa uliosababisha Mauaji ya Mlinzi wa Baa ya Boardroom huko Sinza, Wilayani
SRUV

YOHANA 8

3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.

4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.

5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake kama hawa; nawe wasemaje?

6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika ardhi.

7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika ardhi.

9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.

10 Yesu akainuka asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Nenda zako; wala usitende dhambi tena.
 
Ni vyema tukaitafakari kwa kina nukuu hii kutoka katika kipande cha Injili. "Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu basi na awe wa kwanza kumtupia jiwe mwanamke huyu aliyefumaniwa akizini"SRUV

YOHANA 8

3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.

4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.

5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake kama hawa; nawe wasemaje?

6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika ardhi.

7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika ardhi.

9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.

10 Yesu akainuka asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Nenda zako; wala usitende dhambi tena.
... ila mwanaume aliyekuwa akizini naye hakuletwa! Hayo mafarisayo yalikuwa manafiki hakunaga duniani!
 
... ila mwanaume aliyekuwa akizini naye hakuletwa! Hayo mafarisayo yalikuwa manafiki hakunaga duniani!
Ni sawa tu na huyu RC Chalamila...

Yaani anatafuta makahaba wa kike lakini makahaba ya kiume (akiwemo yeye Chalamila na polisi wake) ambao hufanya ngono na hao wanawake aliowabatiza jina tu la "makahaba", akiwaacha...!!

Huu ni unafiki wa ajabu na ni tabia ya kujihesabia haki isiyoelezeka..!!
 
Ni sawa tu na huyu RC Chalamila...

Yaani anatafuta makahaba wa kike lakini makahaba ya kiume (akiwemo yeye Chalamila na polisi wake) ambao hufanya ngono na hao wanawake aliowabatiza jina tu la "makahaba", akiwaacha...!!

Huu ni unafiki wa ajabu na ni tabia ya kujihesabia haki isiyoelezeka..!!
Wanafki tu

Ova
 
Ukahaba ni kama ushoga

Naunga mkono hoja kwamba sio kosa la jinai

Kardinali wa Ghana kasema juzi ushoga sio kosa la jinai wazee wa KUHUKUMU wamemparamia bila kumuelewa😁
 
Back
Top Bottom