Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,497
113,592
Wanabodi,
Kitendo kilichofanywa na Naibu Spika, hakiwezi kuachwa hivi hivi, hivyo natoa wito kwa wabunge wetu, wenye mapenzi mema na taifa hili, kuanzisha vuguvugu la kuzifumua kanuni zote zinazompa spika/ naibu spika mwanya wa kuliendesha Bunge kwa udikteta kadri nafsi zao zinavyoona inafaa!,badala ya kuliendesha Bunge kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni.

Hakuna ubishi kuwa Mhe. spika, kuna wakati analiendesha bunge kibabe na kidikteta ila udikteta wa Spika unatokana na hulka za Uhehe na mazingira ya spika mwanamke kuliongoza Bunge lililotawaliwa na mfumo dume.

Mazingira ni kwa vile Mhe. Spika ameupata uspika sio kwa kuupigania na kumshinda spika Sitta, bali ameukwaa uspika kutokana na huruma tuu ya kijinsia kuwa, Spika Sitta ni mzuri na amefanya kazi nzuri, ila sasa CCM, imeamua kuitumia karata ya jinsia yake na sio kutokana na uwezo hivyo to prove she is able and capable, kujikuta analazimika aonyeshe uwezo na makucha, hivyo ku over do.

Kwa upande wa hulka yeye Spika ni mtu wa Iringa, Mhehe, Wahehe wako very serious, hawataki ujinga ujinga, hivyo they are always wako very emotional na hot tempered, hivyo Madam lady Speaker anakuwa easly provoked hivyo kupandisha hasira na morali kirahisi na kutoa maamuzi ya kibabe na kidikteta huku akiyatetea kwa hoja japo nyingine ni hoja dhaifu!, ila baada tuu ya muda mfupi, hasira hizo za Kihehe hupoa na kutulia hivyo mkikutana nje mtacheka tuu as if nothing happened!.

Ila huyu Naibu Spika, yeye japo ni mtu mtulivu, makini na mtaratibu sana kwa nje, ila kwa ndani ndie dikteta mbaya na hatari zaidi kuliko hata Madam Spika, huyu ni ile type ya watu kama alivyo simba mwenda kimya!

Hili nimelishuhudia leo bungeni wakati akiizima hoja ya dharura ya kuujadili mgomo wa madaktari kwa dharura iliyoibuliwa na wabunge wawili akiwemo Mhe. JJ Mnyika.

Hoja imeombwa kwa mujibu wa kifungu cha kanuni No. 47 ambapo Naibu Spika akaizima hivi hivi juu kwa kwa juu kwa macho makavu kabisa bila hata kupepesa macho wala ku blink jicho as if mgomo wa madaktari is nothing, kwa hoja rahisi na dhaifu kabisa kuwa hoja hiyo haikuungwa mkono!.

Kitendo tuu cha madaktari kugoma ni very serious issue kwa sababu kazi ya udakitari, inaambatana na kiapo cha kulinda uhai wa binadamu no matter what!. Kitendo tuu madaktari kugoma ni kitendo cha kushtusha taifa, hivyo kitendo cha hoja hii kuibuliwa bungeni na waheshimiwa wabunge wawili kwa mpigo ni uthibitisho tosha kuwa hoja hiyo tayari imeungwa mkono na wabunge wawili, sasa huyu Naibu Spika alitaka mpaka iungwe mkono na wabunge wangapi ndipo iwe hoja valid?.

Takwa la kanuni ni hoja kuungwa mkono na angalau wabunge wawili. Naibu Spika alipaswa kwanza kuuliza kama hoja hiyo inaungwa mkono lakini hakuuliza ili kama kuna wabunge wengine wanaounga mkono wajitokeze, yeye aliamua tuu kuizima jumla juu kwa juu!.

Watu kama hawa wanafikiri kwa kuzima hoja za msingi kama hizi ni kuwakomoa wapinzani kwa kudhani ndio wanaisaidia serikali bila kujijua hawaisaidii serikali, hawamsaidii rais wa JMT na hawalisaidii taifa kwa kuzuia hoja tete kama hii kujadiliwa na Bunge.

Kitendo cha Bunge kukataa kuujadili mgomo wa madaktari kutapelekea watu kupoteza maisha, waziri wa afya kupoteza kibarua chake na mwisho siku kitamlazimisha rais wa JMT kuja mbele ya umma, kwanza kwa kumtimua msaidizi wake, Waziri wa Afya as a scapegoat move, kisha kuwapigia magoti madaktari hawa kuwaomba wasitishe mgomo wao na warejee kazini.

Hivi seriousness ya mgomo wa madaktari inahitaji uungwaji wa mkono wa aina gani kuonyesha hili jambo ni dharura?!.

Mhe. Naibu Spika na ile height yake, na smilling face yake ndio type ya wale ambao wana ku stab on your face infront huku anakuangalia akismile as if nothing has happened!, wakati kwa kawaida stabbing hufanywa kwa nyuma on your back ili anaye ku stab asikuone usoni, ndio maana inaitwa backstabbing!.

Lengo la kanuni za Bunge ni kutoa muongozo kwa viongozi wa Bunge na Wabunge kuendesha Bunge letu, hivyo kanuni hizo zinapotumika ndivyo sivyo kuminya hoja za msingi, Wabunge wetu hakikisheni mnajenga hoja ya kubadili kanuni ili kuzuia madikteta wa type ya Spika na Naibu wasiabuse powers vested on them na kanuni haswa katika kutoa ufafanuzi jambo la dharura la kujadiliwa na bunge ni lipi?!.

Kama mgomo kama huu madaktari nchi nzima ambao, peoples life at stake, anaibuka mtu na kuuona sio dharura, jee mpaka kutokee nini ndipo lionekane hili ni jambo la dharura?, ua kusubiri kwanza watu wafe ndipo tuone sasa ni dharura?!.

Kwa haya yanayotekea bungeni sasa, yananifanya nimkumbuke sana Spika Sitta, kulikuwa hakuna ujinga ujinga kama huu tunaoushuhudia ukiendelea sasa kwenye hili Bunge letu tukufu.

Paskali
 
Pasco nakubalina na wewe kabisa. Sikuamini hata chembe kama Ndugai anaweza kusema aliyosema. Watanzania ni kama tuko yatima. wawakilishi wametugeuka. Cha kuhuzunisha ni pale Ndugai alipokubali kwamba hoja iliyotolewa kweli ina ya msingi na ina maslahi kwa wananchi, sasa kwa nini akatae isijadiliwe? Mimi nadhani Spika ameshatoa maelekezo mgomo wa madaktari usijadiliwe. Hatuna bunge maana bunge la Makinda liko chini ya serikali. Spika na naibu wake wamekuwa wasemaji wa serikali.
 
walishaambiwa hao mkuu wasijadili suala la mgomo wa madaktari kwa sababu upo mikononi mwa raisi kwa sasa!
 
Wanabodi,
Kitendo kilichofanywa na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai, hakiwezi kuachwa hivi hivi, hivyo natoa wito kwa wabunge wetu, wenye mapenzi mema na taifa hili, kuanzisha vuguvugu la kuzifumua kananuni zote zinazompa spika/ naibu spika mwanya wa kuliendesha bunge kwa udikteta kadri nafsi zao zinavyoona inafaa!

Hakuna ubishi kuwa Mhe. Makinda kama spika, kuna wakati analiendesha bunge kidikteta ila udikteta wa Makinda unatokana na mazingira na hulka.

Mazingira ni kwa vile kaupata uspika kutokana na jinsia yake na sio kutokana na uwezo hivyo to prove she is able lazima aonyeshe uwezo.

Kwa upande wa hulka yeye Mama Makinda ni emotional na hot tempered lady hivyo anakuwa easly provoked hivyo kupandisha hasira kirahisi na kutoa maamuzi ya kidikteta huku akiyatetea kwa hoja japo nyingine ni dhaifu!.

Ila huyu Naibu Spika Mhe. Job Ndungai yeye ni mtu mtulivu, makini na mtaratibu sana ila ndie dikteta mbaya zaidi kuliko Mama makinda kama alivyo simba mwenda kimya!.

Hili nimelishuhudia leo bungeni wakati akiizima hoja ya dharura ya kuujadili mgomo wa madaktari kwa dharura iliyoibuliwa na wabunge wawili akiwemo Mhe. JJ Mnyika.

Hoja imeombwa kwa kifungu no. 47 ambapo Dugai akaizima hivi hivi juu kwa kwa juu kwa macho makavu kabisa bila hata blink ya jicho kuwa hoja hiyo haikuungwa mkono!. Kitendo tuu cha kuibuliwa na wageshimiwa wabunge wawili kwa mpigo ni kuungwa mkono tosha, alitaka mpaka iungwe mkono na wabunge wangapi!.

Hivi seriousness ya mgomo wa madaktari inahitaji uungwaji wa mkono wa aina gani kuonyesha ni dharura!.

Mhe. Ndugai na smilling face yake ndio type ya wale ambao wana ku stab on your face infront huku anasmile as if nothing happened, wakati kwa kawaida stab hufanywa on your back!.

Wabunge wetu hakikisheni mnajenga hoja ya kubadili kanuni ili kuzuia madikteta wa type ya Ndugai na Mama Makinda wasiabuse powers vested on them na kanuni!.

Hapo kwenye red ndio unapokosea, wabunge wanawatumikia waliowapatia posho ya siku 200,000/=.
 
Hilo litawezekana iwapo wabunge wa CCM wataamua kukaidi maagizo wanayopewa na chama kwa maslahi ya chama
 
Katika hili nakuunga mkono Pasco bunge kwa sasa linaendeshwa kitemi na udikteta unaoongozwa na Makinda na mwenzie Ndungai. Bunge letu limepoteza mwelekeo sio tena bunge la kumtetea mwananchi, inasikitisha kuona kwa sasa hatuna tena watetezi. Imenitia hasira sana
 
wao haiwagusi kwani wakiumwa wanakwenda apollo ingekuwa madaktari wa apollo wamegoma ungeona kelele zake wangeongea hadi mapovu ya watoke mdomoni lakini kwa sababu muhimbili ni ya walala hoi wao kwao ni uchafu haiwagusi hivyo kuizima ni kawaida, ila wakumbuke one day yes watajua kuwa watanzania ni watu waina gani..... kwani kwa mbali naona makundi yanasogea kuipinga serikali yetu midundo ya ngoma na sauti za walala hoi wasiokuwa na matumaini na serikali yao inakuja wako kwambaliiiiii.....
 
Nimelitafakari hili suala la mgomo wa madaktari na kile kinachoendelea ndani ya serikal na uongozi wa juu wa bunge,ni dhahiri serikali inaonyesha kuwa ni mpango wa kutupunguza watanzania tulio zaid ml 45 angalau kufikia ml 20 wakiamini ndio idadi wanayoweza kuimudu.ni hatari kwa taifa na inasikitisha sana ndugu zangu.ila hili ni bomu likifikia kulipuka litalipuka tu.
 
wataanzisha vuguvugu wapi? bado bunge lina watu wale wale akina Juma Nkamia wataunga mkono hoja?
 
Tunaiondoaje SERIKALI Bungeni? Ukiondoa Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar wengine wote waliobaki kwenye CABINET ni WABUNGE au sehemu ya Bunge. KATIBA yetu ya JMT imetufikisha hapa. Mbaya zaidi SPIKA ni mjumbe wa CC ya CCM. Katika hali kama hii BUNGE litabaki kuwa hivo lilivo hadi tupate katiba mpya yenye akili.
 
nimelitafakari hili suala la mgomo wa madaktari na kile kinachoendelea ndani ya serikal na uongozi wa juu wa bunge,ni dhahiri serikali inaonyesha kuwa ni mpango wa kutupunguza watanzania tulio zaid ml 45 angalau kufikia ml 20 wakiamini ndio idadi wanayoweza kuimudu.ni hatari kwa taifa na inasikitisha sana ndugu zangu.ila hili ni bomu likifikia kulipuka litalipuka tu.
linatakiwa lilipuke sio lita maana tumechoka
 
Jamani rais wetu ni mtaalmu wa mazishi na kutembelea wagonjwa , hivyo huu mgomo una maslahi kwani wanapokufa watu wengi atakuwa anaitumia vema taaluma yake.
 
Tunaiondoaje SERIKALI Bungeni? Ukiondoa Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar wengine wote waliobaki kwenye CABINET ni WABUNGE au sehemu ya Bunge. KATIBA yetu ya JMT imetufikisha hapa. Mbaya zaidi SPIKA ni mjumbe wa CC ya CCM. Katika hali kama hii BUNGE litabaki kuwa hivo lilivo hadi tupate katiba mpya yenye akili.

Vyema mzee.
Kwa katiba hii inayotumika, ni vigumu sana kwa wabunge kubadili kanuni hizo kama anavyoshauri mzee Pasco.
 
Katika hili nakuunga mkono Pasco bunge kwa sasa linaendeshwa kitemi na udikteta unaoongozwa na Makinda na mwenzie Ndungai. Bunge letu limepoteza mwelekeo sio tena bunge la kumtetea mwananchi, inasikitisha kuona kwa sasa hatuna tena watetezi. Imenitia hasira sana

mkuu tatizo sio kanuni,makinda,ndugai au ccm hapa tuwe wakweli tu wabunge wengine wote wa cdm waliokuwa bungeni leo isipokuwa mnyika ambaye alianzisha hoja hawakusimama kuunga mkono hoja.wabunge wa cdm tuna mkataba nao sisi wanyonge kwa nini hawkuunga mkono? naomba majibu kutoka kwa hawa ambao niliwaona wakiwa bungeni.l.nyerere,sugu,mdee,kahigi.wengine akina lema ,wenje,msigwa,zito,arthi na silinde sikumbuki kuwaona bungeni leo.mnyika,ukiwa kama kiongozi wao toa taarifa na hatua watakazochukuliwa,wamekiabisha chma na kusaliti maslahi ya wanyonge.
 
Jamani mbona makamba jr alivoibua ishu ya mafuta kwa mtindo wa dharura hakuna wabunge waliosmama na palepale mjadala ukaanza. Hii ya leo ni usanii mtupu
 
Kwa ukweli, Naibu spika nadhani alikuwa tayari kabisa kulifanya jambo hili lizungumzwe. Lakini kwa vile taratibu hazikufuatwa za wabunge kusimama na kuunga mkono, ndiyo maana akasema hivyo. Lakini pia ikubukwe kuwa, wabunge wote wa CCM wameshapigwa stop kuliongelea hilo mpaka Serikali yao iliyoshindwa kazi itoe tamko. Lakini kama ulimsikiliza Ndugai, mwishoni alisema, Misri ambako wabunge walikuwa likizo, jana mara baada ya kutokea mauaji ya watu zaidi ya 75 ktk uwanja wa mpira, Bunge limeitwa kwa ajili ya kuja kudiscuss issue hiyo tu. Nadhani alikuwa anaonyesha wazi kuto kukubaliana na wakubwa wake. Lakini akasema mpaka kesho kama Serikali haijatoa taarifa, ataliwasha bungeni kesho.
 
Wabunge njaa unategemea wajadiri jinsi wapiga kura wao wanavyo jinyea mahospitalini kwa kukosa huduma thubutu
 
Pasco usitegemee wabunge hawa hawa wanaolilia posho na wameongezewa hadi 200,000/- watatia neno.Hawa wanafikiri kwa kutumia matumbo mkuu.
 
Back
Top Bottom