Wito wa mpito kwa DPP: Wakili aliyemwandaa ACP Kingai aondolewe jopo la Mashtaka la akina Mbowe

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Jana nilikuwepo Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi. Sikwenda pale kwa minajiri ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Nilikwenda kufuatilia mambo ya mwanangu anayesoma pale Law School of Tanzania. Kwakuwa nilimaliza kilichonipeleka mapema na niliwaona hata marafiki zangu wakijumuika kuhudhuria kesi ya akina Mbowe, niliamua kujumuika nao. Ni katika viunga hivyohivyo vya Law School of Tanzania.

Jana, upande wa Mashtaka (Jamhuri) ilianza kuleta mashahidi. Shahidi wa kwanza, na nilishajua na kumtegemea, akawa ni ACP Ramadhani Kingai ambaye kwasasa ni RPC wa Kinondoni. Kama shahidi wa kwanza na wa muhimu wa Jamhuri, Kingai alieleza mengi kwenye kesi ya msingi na hata kwenye kesi ndogo iliyoibuka baada ya mapingamizi yaliyotolewa na upande wa Utetezi uliokuwa ukiongozwa na Wakili Msomi Kibatala.

Katika uga wa kisheria, shahidi yeyote huandaliwa na Wakili anayemleta mahakamani. Kuandaliwa si kufundishwa cha kusema ila ni kuunda mtiririko na mueleweko wa ushahidi wa shahidi husika. Pia, maadalizi hujumuisha upembuzi wa kipi cha kuanza; kipi cha kumalizia; kipi cha kusemwa na kipi cha kutokusema mahakamani kwenye kesi husika. Hata ACP Kingai aliandaliwa na Wakili au Mawakili wa Jopo la Mashtaka.

Kuna mambo ya wazi kabisa ambayo yameleta mkanganyiko badala ya muunganiko kwenye ushahidi wa Kingai. Mkanganyiko usio na tija. Kuhusu mtiririko wa matukio; kilichotokea na kilichofanyika na polisi. Nitatoa mifano michache kwakuwa mambo yenye mkanganyiko yalikuwa mengi mno. Kwanza, Kingai hakutaja kwenye ushahidi wake kuhusu watuhumiwa kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni. Aliishia kusema walifikishwa Central Dar. Kwanini hakuandaliwa kuhusu hilo?

Pili, Kingai amesema kuwa watuhumiwa walikutwa na bastola moja na risasi tatu. Ni tofauti na Hati ya Mashtaka inayotaja risasi moja. Tatu, amezungumzia watuhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya. Kwanini hakuandaliwa kuacha kuzungumzia kitu kisicho sehemu ya mashtaka ya akina Mbowe? Nne, Kingai amesema kuwa alipokuwa akiongoza timu ya upelelezi na ukamataji alikuwa Regional Criminal Officer (RCO) wa Arusha. Hakuandaliwa kueleza kwanini alifanyia kazi mikoa ya wengine kwenye ma-RCO na askari wengine?

Au Kingai naye alikuwa Sabaya wa pili? Tena, Kingai ameeleza kuwa kuna mashahidi walichukuliwa maelezo yao Moshi. Hapohapo akasema watuhumiwa walichukuliwa maelezo yao Dar es Salaam kwakuwa ndiko jalada lilipokuwa limefunguliwa. Kwanini wahusika wa jambo moja watofautishwe mahali pa kuchukuliwa maelezo yao? Hapa pia hakuandaliwa vyema. Kingai amefanya kadiri ya uwezo wake kuelezea. Lakini, hakuandaliwa vyema.

Halafu, kama mkamataji hakupaswa kushiriki kwenye kuwachukua maelezo washtakiwa. Hivi Wakili aliyemwandaa hakulijua hata hilo? Maana Kingai amekuwa akirudiarudia mahakamani kuwa aliwachukua maelezo washtakiwa ambao yeye mwenyewe ndiye aliyewakamata. Kufanya hivyo si kuandika stori yake mwenyewe anayetaka wengine waiamini na kumpongeza kwa uandishi wa stori tamu kuwahusu washtakiwa?

DPP Mwakitalu, chukua hatua mapema. Ondoa Wakili au Mawakili waliomuandaa Kingai. Kama Kingai amejikanyaga vile, watakaofuata wataanika madudu mapya na yakutisha zaidi.

Chief Hangaya, nasi tuanze kampeni chamani?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Kwa maoni yangu Kingai kuacha kutaja Kituo cha Mbweni haikua bahati mbaya. Walikusudua kuficha kitu

Kitendo cha kuhamisha hamisha vituo watuhumiwa ni ili polisi wahalalishe kuendelea kuwashikilia na pia kuwapa kibano(utesaji). Wasingeweza kusema hivyo
 
Nyie jipeni matumaini tu hizo ni hoja mrenda mrenda sana mbowe lazima ale mvua yaani kumbe ni kweli jamaa ni gaidi na aliznza zamani
 
Vuta, uongo si rahisi kuu-maintain consistently during narrations and when you are on mental tension. Ndicho kilichotokea.

Utajichanganya tu maana Ni vitu vya kutunga. Huwezi kusahau ukweli wa kitu ambacho umekifanya physically, utausahau uongo mtiririko wake wa kutungwa. Na wengine watakuwa vituko zaidi.
 
...Halafu, kama mkamataji hakupaswa kushiriki kwenye kuwachukua maelezo washtakiwa. Hivi Wakili aliyemwandaa hakulijua hata hilo? Maana Kingai amekuwa akirudiarudia mahakamani kuwa aliwachukua maelezo washtakiwa ambao yeye mwenyewe ndiye aliyewakamata. Kufanya hivyo si kuandika stori yake mwenyewe anayetaka wengine waiamini na kumpongeza kwa uandishi wa stori tamu kuwahusu washtakiwa...
Wakili wa Serikali; unayatambuaje Maelezo yako?

Shahidi; nayatambua kwa mwandiko wangu, sahihi ya Adam na sahihi yangu

Ameihakikishia mahakama mbele ya Mtukufu Jaji kwamba yale maelezo ni yake mwenyewe (ACP Kingai; mkamataji)!
 
Back
Top Bottom