Wito NGO's, Wanaharakati kupambana na Ufisadi

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
28
Nafikiri ni jambo jema kwa NGOs na Wanaharakati wetu sasa kujiunga kwenye mapambano dhidi ya Ufisadi.

Nafikiri jamii pia inaguswa zaidi na Ufisadi kwa njia moja au nyingine kama inavyoguswa na masuala ya ukeketaji, mauaji ya albino,masuala ya jinsia UKIWMI nk.

Ukiangalia NGO zetu nyingi na wanaharakati wetu wengi wamejikita kwenye masuala ya ukimwi na watoto yatima na kusahau kuwa Ufisadi na rushwa ndiyo msingi mkuu wa matatizo hayo, sitaki kusema kuwa wanafanya hivyo kwa sababu ya masilahi yao, hapana.

Tukiondoa ufisadi katika mahakama zetu katika wizara zetu, mabenki yetu nk, haki katika jinsia tunayoitafuta itapatikana, mauaji ya albino yatapungua kama siyo kwisha kabisa kwa maana yanasababishwa na kipato kidogo cha watu.

Kwa hiyo RAI kwa wanaharakati wetu kama akina Ananilea Nkya, Tamwa nk wageuke tuwe tunasikia angalau wamefungua kesi kwa fisadi fulani na siyo kuwaachia wanasiasa kazi ya kupambana na mafisadi papa.

Naomba mwenye mawazo zaidi kwa hoja hii.
 
Ngudu yangu, huko kwenye NGOs kuna ufisadi pia... sema tu kwasababu ya budgets zao na NGO nyingi ziliundwa kimtindo then we dont hear much about them

Si za afya, sheria, elimu, kilimo nk.... kuna madudu huko pia mazee, i wouldnt expect much from them
 
Back
Top Bottom