Wito kwa watanzania wote: Ili CCM na serikali zake wajue hatuwataki, 2025 wote tususie uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi

Mkuu mimi zizungumzii vyama vya siasa tu,vyama na wananchi wote.I believe if that happens,it will be hard to swallow for CCM.Legitimacy inatoka kwa wananchi,hawajawapa,mtajiwekaje madarakani?Hilo ndilo tunalotaka litokee.
Sasa ili kufikia hilo bosi wangu lazima watu wetu wawe na:
1. Nguo za kutosha ili wakihongwa t.shirt na kofia wakatae
2. Wawe na shibe ya kutosha ili wakihongwa msosi wasikubali.
Taunzie hapo.
 
Ni miaka 63 sasa CCM ipo madarakani. Kimsingi hakuna maendeleo ya maana waliyotuletea, isipokuwa kuturudisha nyuma kimaendeleo miongo kadhaa.

Kila serikali iliyoingia madarakani ilileta usanii wa kisiasa na kiuchumi na hatimaye kuturudisha nyuma decades.Wanayojisifia kwamba ni maendeleo si lolote kabisa ukilinganisha na rasilimali nyingi tulizo nazo. Tuamke Watanzania.

Comrade Magufuli katika awamu yake moja alijitahitahidi kubadilisha taswira ya Tanzania kwa kutuletea maendeleo kiasi fulani, lakini juhudi zake zilifishwa prematurely, inasikitisha sana.

Kwa jinsi hali ya kisiasa ilivyo nchini mwetu, hatuna jinsi yeyote ambayo kama Watanzania tunaweza kujinasua kwenye mkwamo wa kimaendeleo na kisiasa tulio nao sasa.Katiba haiheshimiwi kabisa na sioni uwezekano wa Bunge au hata wana siasa kutusaidia.

Mwito wangu kama Mtanzania ni huu, kama mpaka 2025 tusipokuwa na Katiba mpya, wala Tume Huru ya Uchaguzi, siku ya uchaguzi wote tubaki nyumbani.Sisi wananchi ndio tunaowapa wanasiasa legitimacy ya kutawala, kama wasipotupa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi tubaki nyumbani,simply tuwanyime legitimacy ya kututawala.It is now or never, tushirikiane wote.
Wataenda kupiga kura wale wenye hali nzuri ya maisha tu.

Ila sisi tunaoganga ganga aisee tushirikiane tusiende
 
Mkuu, unayosema ni sahihi kabisa, lakini pia nikukumbushe, hata hiyo Katiba Mbovu iliyopo, hakuna mahala popote inaporuhusu uvunjifu wa sheria za uchaguzi. CCM wanachofanya ni kufanya uhalifu, wanavunja sheria.
Imeruhusu kiaujanja ujanja sema wewe ndio huelewi.

Inapompa mamlaka Rais kuteua msimamizi wa uchaguzi yeyote anayemtaka huku na yeye akiwa bado ni mgombea ujua Katiba Ni Mbovu sana na inahimiza maovu.
 
LOOoh!

Aisee, unanisikitisha sana kwa kweli; kama unaamini uwepo wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi", hapo ndipo CCM itashindwa uchaguzi.

Mbona maswala haya hujadiliwa mara nyingi sana humu JF, yaani wewe hata siku moja hujatokea kusoma chochote kuhusu ufinyu wa mambo hayo katika kuizuia CCM isiendelee kuharibu chaguzi zinazofanyika hapa nchini?

Halafu, wakati huo huo unahimiza waTanzania wakasusie uchaguzi, wakati ukijua wazi kuwa hiyo ndiyo njia bora kabisa wanayoitegemea CCM?

Umeshuka toka sayari gani, mkuu 'Mathanzua', ambako habari za CCM na nchi hii hazifiki kabisa? Hata kama ungekuwa umejificha pangoni pasipofikiwa na mwanga, ingewezekana siku moja moja ukasikia habari za hili zimwi (CCM) lililoiteka Tanzania.
1.Tukiwa na Tume Huru,itakuwa vigumu CCM kuiba kura kwa kuwa hakutakuwa na vijeba vya CCM.CCM mbinu yao kubwa ya kushinda Uchaguzi ni kuiba kura.
2.Katiba tuliyonayo inafanya iwe vigumu matokeo kuhojiwa.Hii ni mbinu pia wanayoitumia kushinda uchaguzi.
3.Times have changed,2015 sio sawa na 2025.
 
Wataenda kupiga kura wale wenye hali nzuri ya maisha tu.

Ila sisi tunaoganga ganga aisee tushirikiane tusiende
Wewe unayeganga ganga ndo utakuwawa kwanza kupiga kura kwa kuwa huna nguo za kutosha utapigwa t.shirt moja ya kijani na utawahi fasta kupiga kura kiulaini.
 
Wataenda kupiga kura wale wenye hali nzuri ya maisha tu.

Ila sisi tunaoganga ganga aisee tushirikiane tusiende
Hata wenye h.ali nzuri ya maisha wengi wanaichukia CCM mkuu,labda wale ambao kula yao inategemea uwepo wa CCM madarakani.
 
Imeruhusu kiaujanja ujanja sema wewe ndio huelewi.

Inapompa mamlaka Rais kuteua msimamizi wa uchaguzi yeyote anayemtaka huku na yeye akiwa bado ni mgombea ujua Katiba Ni Mbovu sana na inahimiza maovu.
SAWA.
Tukubali "imeruhusu kiujanja ujanja", kupitia kwenye kumpa rais madaraka makubwa; lakini kumbuka haimpi rais ruhusa ya kuvunja sheria, na bado anavunja sheria.

Sasa nieleze, hiyo "Mpya", ambayo na mimi naililia sana, itazuia vipi "uvunjifu wa sheria" toka kwa hawa hawa wasioheshimu hata hii iliyopo sasa.

Kumnyima rais uteuzi pekee, hakuzuii kuvunja sheria kunakofanywa siku zote na CCM.
 
1.Tukiwa na Tume Huru,itakuwa vigumu CCM kuiba kura kwa kuwa hakutakuwa na vijeba vya CCM.CCM mbinu yao kubwa ya kushinda Uchaguzi ni kuiba kura.
2.Katiba tuliyonayo inafanya iwe vigumu matokeo kuhojiwa.Hii ni mbinu pia wanayoitumia kushinda uchaguzi.
3.Times have changed,2015 sio sawa na 2025.
Haya unayoyaeleza hapa ni kuwa Katiba Mpya, itatekelezwa kwa usahihi kabisa na vyombo vyote vilivyomo serikalini, hali ambayo tunajua siyo kweli chini ya CCM.

Sasa mimi ngoja nikupe pendekezo mbadala wa hayo unayoyahimiza wewe; hasa hilo la kususia uchaguzi.

1. Mimi nahimiza watu wengi sana wanaolitakia mema taifa hili wajitokeze kwa wingi sana wakati wa kupiga kura, na wapige kura za kuikataa CCM.

2. Badala ya kutegemea Katiba Mpya kulinda kura za wananchi zisiibiwe na CCM (kwa kufanya uhalifu), mimi nawahimiza wananchi hawa wakatae uhalifu na kuvurugiwa kura zao (kuzuia uhalifu). Kinachotakiwa sasa hivi, si kuwahimiza wananchi wasusie uchaguzi, bali ni kuweka mikakati sahihi ya kuzuia uhalifu huo. Wananchi waelimishwe, na wapewe njia sahihi za kukataa kura zao kuharibiwa.
Swala linalojitokeza hapa ni nani atakayefanya kazi ya kuwapanga wananchi,... wewe mkuu 'Mathanzua', na wengine wengi tuliochoshwa na hujuma za CCM, ni wajibu wetu kuwa sehemu ya kuzuia uovu unaofanywa na CCM, kwa kuelimishana. Vyama vya siasa na taasisi za kijamii, ni wajibu wao kusaidia katika kuwapanga wananchi watimize wajibu wao

3. Hiyo namba tatu uliyoweka hapo, sioni maana yake hata ndogo katika kuzuia yanayofanywa na CCM.
Hali ni mbovu kiasi kwamba kuna watu wanajiita kwa sifa kubwa kuwa wao ni "CHAWA"? Haya hayajawahi kutokea hata siku moja katika historia ya nchi hii.
 
SAWA.
Tukubali "imeruhusu kiujanja ujanja", kupitia kwenye kumpa rais madaraka makubwa; lakini kumbuka haimpi rais ruhusa ya kuvunja sheria, na bado anavunja sheria.

Sasa nieleze, hiyo "Mpya", ambayo na mimi naililia sana, itazuia vipi "uvunjifu wa sheria" toka kwa hawa hawa wasioheshimu hata hii iliyopo sasa.

Kumnyima rais uteuzi pekee, hakuzuii kuvunja sheria kunakofanywa siku zote na CCM.
Kw akuwa kuna loophole kwamba Mteule wa Rais hawajibiki kwa mtu yeyote mpaka kwa Rais mwenyewe tu so wateule hawa wanavunja sheria sababu wana Kinga moja kwa moja kutoka kwa mteuaji.

Sasa basi ikiwa Mahakama mamlaka yake haitoki moja kwa moja kwa rais pekee akina Makonda et al wasingekuwa wanadharau wito wa mahakama na kufanya wanayotaka.

Huo ni mfano tu ktk mingi.

Njia tunazopata viongozi wengi ni kwa njia ya Uchaguzi sasa tazama uovu na uvunjaji sheria unaofanyika wakati wa Uchaguzi huku aliyewatuma wafanye hivyo ni Mgombea ambaye bado yuko madarakani na ndiye kawateua hao wavunja sheria ili aliyewateua wamlinde kwenye Ushindi wa mezani.

Hizi loopholes ndio ubovu wa katiba yenyewe.

Tumeona Ripoti ya CAG ilivyoivua nguo serikali. Lakini Dr Tulia Ackson kwa kuogopa kuaibisha Mama akaamua kuitupilia mbali yasije kumkuta Yale ya Ndugai....
 
Hakuna hata moja kati ya uliyoyaeleza hapa ninalokataa, umeandika ukweli mtupu hapo.

Lakini, pamoja na ukweli huu, mimi naamini, dawa sahihi kabisa ya kuwakomesha hawa watu wa CCM ni wananchi wenyewe, na siyo lazima iwe Katiba Mpya.

Tukipata watu wa kutosha, watakaokuwa tayari kukataa uhalifu, CCM hawawezi kufanya uhalifu wao waliozoea kuufanya.

Huhitaji raia milioni kumi, wote kuwa mstari wa mbele kukataa uhujumu huu. Tukipata watu kuanzia laki tano tu, walioelimishwa vizuri, na kuelewa wajibu wao wa kuzuia uhalifu, hapatatokea uhalifu kamwe.
Hawa wakishapatikana, hapo ndipo utakapotambua kuwa kumbe waTanzania wengi wamechoshwa na haya madudu wafanyayo CCM, kwa maana utaona nchi nzima inalipuka kukataa kuharibiwa kwa kura. zao.

Sasa kazi ipo tu hapo pa kuwapa elimu, na kuwaandaa hawa watu wa mwanzo wawe tayari kwa kila hali kutimiza wajibu wao.
Hii ndiyo kazi tunayo waomba CHADEMA waisimamie, kuweka mikakati na kuratibu juhudi zote za kufanikisha zoezi hili.

Nchi hii haiwezi kukosa watu laki tano waliotayari kulinda sheria ili uhalifu usifanywe dhidi ya wananchi.
Hata vyombo vya dola sivioni vkishiriki kuwaumiza wananchi hawa wanaolinda maslahi ya nchi.
Hata CCM wenyewe wataona aibu ya kufanya uhalifu wao. Sasa hivi hakuna anayenyanyua kidole, ndiyo maana wanafanya ionekane kama ni hali ya kawaida tu.
 
1. Mimi nahimiza watu wengi sana wanaolitakia mema taifa hili wajitokeze kwa wingi sana wakati wa kupiga kura, na wapige kura za kuikataa CCM.
Watu walipiga sana tu 2015 na 2020. Unakumbuka Internet ilizimwa. Vituo binafsi vya kuhesabu kula vilivamiwa na watu kibao waliumia.

All that to threaten watu wenye mapenzi mema wasithubutu kuji organize
 
Sasa hapo jambazi ninani hasa mkuu 'Bush Dokta'.

Nami ngoja nikukumbushe kama ulishasahau, au pengine tukio hilo lilitokea unagli mdogo sana kutambua maana yake hasa ilikuwa ni nini:

Kama uliwahi kusikia habari ya CHADEMA kupata wabunge wengi kwenye uchaguzi wakati wa utawala wa Kikwete, uliwahi kujiuliza wabunge wale walipatikana kwa njia zipi?

CCM ilikuwa ni hii hii, tunayoizungumzia sote hapa, lakini walidhibitiwa kwelikweli wakati huo.
Sasa anza kufikiria hali hiyo ingekuwaje leo hii wakati ambapo waTanzania wengi sana wanazo hasira za kila namna na chama hiki chini ya utawala wa kiongozi anayediriki kutuuza kabisa kwa vitaifa vya hovyo kabisa, kwa vile tu vinayo pesa ya kutununua!

Ninakusihi sana mkuu Daktari, usibeze wazo hili, wala kutafuta visababu vya kutupoteza akili tusiweke bidii katika mambo tunayoweza kuyafanya kwa ufanisi kabisa.

Weka mawazo yako kwenye kuwapata, kuwaelimisha, na kuratibu juhudi nzima za kuwezesha hawa watu wanaoweza kuzuia uhalifu wa CCM wakati wa uchaguzi.
Hili ni jambo linalowezekana kabisa kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Tena hayo ya "kuzima intaneti/kuvamia" kama unavyoeleza hapa; hiyo ndiyo chachu nzuri ya kuwa na kundi hili la wananchi walioandaliwa vizuri kabisa kuzuia uharamia kama huo. Hao watashughulikiwa na wananchi kama vibaka wote wanavyoshughulikiwa.
Huko nyuma waliweza kufanya hivyo siyo kwa sababu wananchi walipenda na kufurahia vitendo hivyo. Wananchi walikuwa 'helpless' wasijue la kufanya, kwa sababu hawakuandaliwa kukataa uharamia wa namna hiyo.
 
Kwa mtazamo huu, wa kususia, upo uwezekano kuna shida pahali. Na pahali hapo, sio kwenye Katiba,sio kwenye Sheria, bali kwa Mazuzu.

Naamini huu sio wakati wa Kususia Uchaguzi. Huu, nadhani, ndio wakati muafaka wa kuenda kupiga kura. Huu ni wakati wa mapinduzi.

Kwa heshima zote kwa Bwana Mathanzua , siungi mkono hoja.
 
Ni miaka 63 sasa CCM ipo madarakani. Kimsingi hakuna maendeleo ya maana waliyotuletea, isipokuwa kuturudisha nyuma kimaendeleo miongo kadhaa.

Kila serikali iliyoingia madarakani ilileta usanii wa kisiasa na kiuchumi na hatimaye kuturudisha nyuma decades.Wanayojisifia kwamba ni maendeleo si lolote kabisa ukilinganisha na rasilimali nyingi tulizo nazo. Tuamke Watanzania.

Comrade Magufuli katika awamu yake moja alijitahitahidi kubadilisha taswira ya Tanzania kwa kutuletea maendeleo kiasi fulani, lakini juhudi zake zilifishwa prematurely, inasikitisha sana.

Kwa jinsi hali ya kisiasa ilivyo nchini mwetu, hatuna jinsi yeyote ambayo kama Watanzania tunaweza kujinasua kwenye mkwamo wa kimaendeleo na kisiasa tulio nao sasa.Katiba haiheshimiwi kabisa na sioni uwezekano wa Bunge au hata wana siasa kutusaidia.

Mwito wangu kama Mtanzania ni huu, kama mpaka 2025 tusipokuwa na Katiba mpya, wala Tume Huru ya Uchaguzi, siku ya uchaguzi wote tubaki nyumbani.Sisi wananchi ndio tunaowapa wanasiasa legitimacy ya kutawala, kama wasipotupa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi tubaki nyumbani,simply tuwanyime legitimacy ya kututawala.It is now or never, tushirikiane wote.
Sahiii
 
Kwa mtazamo huu, wa kususia, upo uwezekano kuna shida pahali. Na pahali hapo, sio kwenye Katiba,sio kwenye Sheria, bali kwa Mazuzu.

Naamini huu sio wakati wa Kususia Uchaguzi. Huu, nadhani, ndio wakati muafaka wa kuenda kupiga kura. Huu ni wakati wa mapinduzi.

Kwa heshima zote kwa Bwana Mathanzua , siungi mkono hoja.
Wewe ni wazi ni li-CCM.Bila Katiba Mpya na Tume Huru ya uchaguzi unakwenda kupiga kura ya nini mkuu,kwa kuwa mfumo huo ndio ulio-wawezesha CCM kubaki madarakani miaka yote.Ni ujinga kufanya jambo hilo hilo tena na tena kwa njia hiyo, halafu utegemee matokeo tofauti.Hapana,nakuomba usipotoshe Watanzania.Hatuwezi kuirudisha serikali kwa Watanzania kwa Tume iliyoteuliwa na Chama na Serikali hiyo hiyo tunayotaka kuitoa madarakani na wasimazi
wa Uchaguzi walioteuliwa na serikali hiyo hiyo,it will take us >1000years.Tuwasusie Uchaguzi,vyama vya siasa na wananchi wote.Tusiwape mamlaka kabisa ya kututawala.
 
Back
Top Bottom