Wingi wa neno upo kwenye mofimu ya mwanzo au mwisho?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Muondoke vs Ondokeni
Mje vs mjeni vs njooni
Mwende vs nendeni
Kiswahili sanifu ni hiki chenye "m" mwanzoni kama mofimu inayotaja dhana ya wingi au safu ya pili yenye mofimu "ni" mwishoni?

Tukibaki hapo kwenye mofimu "ni" je ni sahihi kuitumia kurejelea wingi kwenye maneno kama;

" Shikamooni, hamjamboni, na usiku mwemeni" Japo hii ya "usiku mwemeni" inatumiwa na mabinti wa chuo.

Hutaki vs hautaki
Huji vs hauji
Huandiki vs hauandiki
Safu ipi ni sahihi kwenye ukanushi?

Mofimu "si" imekuwa ikitumika kukanusha kama kwenye maneno; sitaki, siendi na mengineyo lakini kwenye neno "sijambo" inatumika kuyakinisha. Kanuni gani ilitumika kuliumba neno hili?
"Mbona" na "kumbe" ni aina gani za maneno?
 
Daima umoja na wingi hubainishwa na kiambishi awali. Mfano katika Neno mje mofimu "m" ndio inayobeba dhana ya wingi. Yaani ingeweza kuwa uje kumaanisha umoja. Lakini kuongeza kiambiashi "ni" imekuwa Kama mbadala wa wingi wa "M" kimazoea na kupelekea kusanifishwa mfano katika Neno imba, Muimbe- imbeni. Hivyo vyote vinatumika lakini sio katika eneo Moja Bali Kwa kubadilishana yaani inapotumika "m" "ni" haitumuki yaani huwezi kusema muimbeni na ukawa sahihi Bali utasema imbeni au Muimbe, mje na sio mjeni, hamjambo, hujamboni na sio hamjamboni,

Kuhusu Neno sijambo kuonesha uyakinishi ni kuwa kanuni iliyotumika ni udondoshaji wa viambishi. Yaani Kwa asili Neno hujambo ni "huna jambo"? Na hujibiwa sijambo ikimaanisha "Sina jambo" . Kanuni hiyo hiyo imetumika kuunda maneno mbadala hutaki na hautaki, huji na hauji,

Kuhusu Neno mbona na kumbe tunaweza kupanua zaidi mjadala Kwa kushirikisha wadau wengine wa lugha. Kwa upande wangu nafikiri tunaweza kuyaweka Kwenye vihisishi kwani hubeba hisia wakati wa utumikaji wake.
 
Muondoke vs Ondokeni
Mje vs mjeni vs njooni
Mwende vs nendeni
Kiswahili sanifu ni hiki chenye "m" mwanzoni kama mofimu inayotaja dhana ya wingi au safu ya pili yenye mofimu "ni" mwishoni?
Tukibaki hapo kwenye mofimu "ni" je ni sahihi kuitumia kurejelea wingi kwenye maneno kama;
" Shikamooni, hamjamboni, na usiku mwemeni" Japo hii ya "usiku mwemeni" inatumiwa na mabinti wa chuo.
Hutaki vs hautaki
Huji vs hauji
Huandiki vs hauandiki
Safu ipi ni sahihi kwenye ukanushi?
Mofimu "si" imekuwa ikitumika kukanusha kama kwenye maneno; sitaki, siendi na mengineyo lakini kwenye neno "sijambo" inatumika kuyakinisha. Kanuni gani ilitumika kuliumba neno hili?
"Mbona" na "kumbe" ni aina gani za maneno?
Zaidi ya neno kifo na fofofo, je ni neno gani lingine la lugha ya Kiswahili linaishia na "fo"?
 
Back
Top Bottom